Mkurugenzi wa Ofisi ya Zanzibar-TMA, Ndugu, Mohamed Ngwali akizungumza katika kikao kazi cha kujenga uelewa na mkakati wa utelezaji wa sheria ya Mamlaka ya Hali ya Hewa kilichofanyika Kibaha, Tarehe 27-28 Desemba 2019. |
Mkurugenzi wa Huduma za Utabiri-TMA, Dkt. Hamza Kabelwa akizungumza katika kikao kazi cha kujenga uelewa na mkakati wa utelezaji wa sheria ya Mamlaka ya Hali ya Hewa kilichofanyika Kibaha, Tarehe 27-28 Desemba 2019. |
Mkurugenzi wa Utafiti na Matumizi-TMA, Dkt. Ladislaus Chang'a akizungumza katika kikao kazi cha kujenga uelewa na mkakati wa utelezaji wa sheria ya Mamlaka ya Hali ya Hewa kilichofanyika Kibaha, Tarehe 27-28 Desemba 2019. |
Mkurugenzi wa TEHAMA na Huduma za Ufundi-TMA, Dkt. Pascal Waniha akizungumza katika kikao kazi cha kujenga uelewa na mkakati wa utelezaji wa sheria ya Mamlaka ya Hali ya Hewa kilichofanyika Kibaha, Tarehe 27-28 Desemba 2019. |
Meneja Rasilimali Watu Bi. Mariam Is-Haaq akizungumza katika kikao kazi cha kujenga uelewa na mkakati wa utelezaji wa sheria ya Mamlaka ya Hali ya Hewa kilichofanyika Kibaha, Tarehe 27-28 Desemba 2019. |
|
Kibaha,
28 Desemba 2019;
Menejimenti
ya Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imefanya kikao kazi kwa siku mbili
ili kupitia kwa pamoja na kupata uelewa wa namna bora ya utekelezaji wa sheria
Na. 2 ya mwaka 2019 ya Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania.
Akizungumza
wakati wa kufunga kikao kazi hicho, Mkurugenzi Mkuu wa TMA na mwenyekiti wa
kikao aliwataka wakurugenzi na mameneja kujenga utamaduni wa utendaji kazi wenye
lengo la uboreshaji huduma ilikufikia malengo ya Mamlaka katika utekelezaji wa
sheria iliyopo. Aidha, aliwapongeza na kuwashukuru washiriki wa kikao kazi
hicho kwa jinsi walivyojitoa kuifanya kazi hiyo kwa umakini mkubwa kwa zaidi ya
saa kumi na mbili za kazi kila siku pasipo mtu yoyote kuondoka.
‘Nataka
baada ya kikao hiki viongozi wote muwe mstari wa mbele katika kuhakikisha
watumishi mnaowasimamia wana fahamu sheria, taratibu na kanuni kwenye utekelezaji
wa majukumu yao kwa maslahi ya Mamlaka na Taifa kwa ujumla’. Alizungumza Dkt.
Kijazi.
Awali,
akifungua kikao kazi hicho Dkt. Kijazi aliwapongeza wafanyakazi wote wa TMA kwa
utendaji mzuri wa kazi uliopelekea kufanikiwa kukishikilia cheti cha ubora cha
ISO 9001:2015 baada ya ukaguzi uliofanyika kati ya tarehe 16 na 20 Disemba,
2019 ambapo TMA ilikaguliwa na Mkaguzi wanje kutoka Canada.
Kikao
kazi hicho kiliwakutanisha Mkurugenzi Mkuu, wakurugenzi, Mkurugenzi Ofisi ya
Zanzibar, Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Hali ya Hewa- Kigoma, mameneja kutoka
makao makuu, mameneja wa Kanda na wanasheria wa TMA.
Awali,
wajumbe walipitia vifungu vyote vya sheria na kujadili kwa kina ili kuhakikisha
viongozi wote wa Mamlaka wanakuwa na uelewa wa pamoja wa sheria hiyo ili
kurahisisha utekelezaji wake katika maeneo yao ya kazi na hivyo kuchangia
katika ustawi wa maendeleo ya nchi kupitia sayansi ya hali ya hewa.
Aidha,
wajumbe hao waliainisha maeneo ya uboreshaji katika kanuni hususan kwenye
udhibiti wa huduma za hali ya hewa katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ukusanyaji
mapato, utoaji huduma za hali ya hewa kwa usahihi na kwa wakati pamoja na kutoa
elimu kwa umma na wadau kuhusu sheria ya Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania.
‘Tunapaswa
kutoa elimu kwa umma hasa wale wadau ambao wanamiliki vituo vya hali ya hewa watambue
kwamba ni kosa kisheria kuwa na vituo ambavyo havijasajiliwa na pia kutumia
vifaa ambavyo havijahakikiwa (calibration) na TMA’ . Alisema Dkt. Kijazi.
Naye
Mkurugenzi wa Ofisi ya Zanzibar-TMA, Ndugu. Mohamed Ngwali akitoa salamu za
shukrani kwa niaba ya washiriki wote, alimshukuru Mkurugenzi Mkuu wa TMA kwa
kufanikisha kikao kazi ambacho kimeongeza uelewa mpana wa matumizi ya sheria
mpya ya TMA na kuahidi kudumisha umoja katika utendaji kazi kwa watumishi wote.
No comments:
Post a Comment