Tuesday, January 28, 2020

TMA YAISHUKURU TAASISI YA EUMETSAT KWA USHIRIKIANO WA KUWAKUTANISHA WATAALAMU KUTOKA SEKTA MBALIMBALI PAMOJA NA WIZARA KUPITIA MKUTANO WA WADAU WA MAANDALIZI KUELEKEA MKUTANO MKUBWA WA KUMI NA NNE (14) WA WADAU WA HUDUMA ZA SETILAITI BARANI AFRIKA, “14th EUMETSAT User Forum in Africa”

Mkurugenzi wa Huduma za Utabiri wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania(TMA), Dkt. Hamza Kabelwa akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa TMA Dkt. Agnes Kijazi katika ufunguzi wa mkutano wa wadau wa kitaifa wa maandalizi ya mkutano mkubwa wa wadau wa huduma za setilaiti barani Afrika (14th Eumetsat User Forum in Africa) unaotarajiwa kufanyika Jijini Dar es salaam mwezi Septemba 2020. 






Wadau kutoka sekta mbalimbali wakichangia mada katika mkutano wa wadau wa kitaifa wa maandalizi ya mkutano mkubwa wa wadau wa huduma za setilaiti barani Afrika (14th Eumetsat User Forum in Africa) unaotarajiwa kufanyika Jijini Dar es salaam mwezi Septemba 2020.





Washiriki wakifuatilia kwa umakini mada mbalimbali zilizokuwa zikiwasilishwa  katika mkutano wa wadau wa kitaifa wa maandalizi ya mkutano mkubwa wa wadau wa huduma za setilaiti barani Afrika (14th Eumetsat User Forum in Africa) unaotarajiwa kufanyika Jijini Dar es salaam mwezi Septemba 2020.
Washiriki wa mkutano katika picha ya pamoja na mgeni rasmi Dkt. Hamza Kabelwa ambaye pia ni Mkurugenzi wa huduma za Utabiri wa TMA aliyemwakilisha Mkurugenzi Mkuu wa TMA Dkt. Agnes Kijazi katika mkutano wa wadau wa kitaifa wa maandalizi ya mkutano mkubwa wa wadau wa huduma za setilaiti barani Afrika (14th Eumetsat User Forum in Africa) unaotarajiwa kufanyika Jijini Dar es salaam mwezi Septemba 2020.



Dar es salaam, 24 Januari 2020.

Dr. Hamza Kabelwa ambaye ni Mkurugenzi wa huduma za utabiri wa hali ya hewa wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa TMA ambaye pia ni Makamu wa Tatu wa Rais wa Shirika la Hali ya Hewa Duniani (WMO), Dkt. Agnes Kijazi amefungua mkutano wa wadau wa kitaifa wa maandalizi ya mkutano mkubwa wa wadau wa huduma za setilaiti barani Afrika unaotarajiwa kufanyika Jijini Dar es Salaam mwezi Septemba 2020 (14th EUMETSAT User Forum in Africa).

Katika hotuba ya ufunguzi aliyoiwasilisha kwa niaba ya Dkt. Kijazi aliwashukuru waandaaji wa mkutano huo ambao ni taasisi ya utafiti ya Ulaya (European Organization for the Exploration of Meteorological Satellite- EUMETSAT) kwa kuwezesha mkutano huo wa wadau wa maandalizi na juhudi wanazofanya katika kujenga daraja kati ya watoa huduma (EUMETSAT na TMA) pamoja na watumiaji wa huduma za Setilaiti zinazohusiana na hali ya hewa kwa nchi wanachama wa Shirika la Hali ya Hewa Barani Afrika.

“Napenda kuishukuru taasisi ya EUMETSAT ilivyoshirikiana na TMA, kuwakutanisha wataalamu kutoka sekta mbalimbali pamoja na Wizara kuja kwenye mkutano huu wa wadau wa maandalizi ya mkutano wa 14 wa EUMETSAT kwa wadau wa Bara la Afrika “(National Preparatory Workshop for the 14th EUMETSAT User Forum in Africa)”, pia nawashukuru EUMETSAT kwa mchango wenu mkubwa katika kutoa huduma za uangazi ambazo zinatumika katika utabiri wa hali ya hewa wa kila siku na ufuatiliaji wa hali ya mazingira; ikizingatiwa pia kuwa mimi ni Mwenyekiti wa Kamati ya WMO ya kuongeza uwezo wa Nchi Wanachama wa WMO katika kuboresha huduma za hali ya hewa “Capacity building”, alisema Dkt. Kabelwa kwa niaba ya Dkt. Kijazi.

Dkt. Kabelwa aliwakumbusha wadau kuwa Bara la Afrika linakabiliana na changamoto za kutokuwa na taarifa za kutosha za uangazi wa hali ya hewa na mazingira ambazo ni muhimu sana katika kufanya maamuzi, hivyo akawahimiza wadau wa mkutano kushiriki kwa wingi katika mkutano wa wadau wa Septemba 2020 ikiwa ni pamoja na kuwa mstari wa mbele katika maandalizi yake ili ufanyike kwa ufanisi na kwa heshima ya Tanzania. 

Aidha, wadau wa mkutano huu wa maandalizi waliwasilisha mada zilizoonesha uzoefu wao katika matumizi ya huduma zitolewazo na EUMETSAT hususan namna wanavyoshiriki katika miradi ya kikanda ya ufuatiliaji wa hali ya hewa na mazingira ambayo inalenga kuboresha huduma za hali ya hewa na mazingira katika nyanja kuu nne (4) ambazo ni ufuatiliaji wa matukio ya ukame, matukio ya mafuriko, matukio ya moto na kilimo. Taarifa hizi ni za muhimu sana katika maendeleo ya kijamii na uchumi wa nchi yetu.

Tuesday, January 21, 2020

WAJUMBE BARAZA LA WAWAKILISHI ZANZIBAR WAZITAKA TAASISI KUCHANGIA HUDUMA ZA HALI YA HEWA.

Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya TMA Dkt. Makame Omar Makame pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa TMA, Dkt. Agnes Kijazi wakiwapokea wajumbe wa Kamati ya Ardhi na Mawasiliano ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar walipotembelea ofisi za TMA, Dar es Salaam, Tarehe 21/01/2020
Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya TMA Dkt. Makame Omar Makame akiwakaribisha wajumbe wa Kamati ya Ardhi na Mawasiliano ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar walipotembelea ofisi za TMA, Dar es Salaam, Tarehe 21/01/2020
Mkurugenzi Mkuu wa TMA, Dkt. Agnes Kijazi akiwakaribisha wajumbe wa Kamati ya Ardhi na Mawasiliano ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar walipotembelea ofisi za TMA, Dar es Salaam, Tarehe 21/01/2020
Mwenyekiti wa Kamati ya Ardhi na Mawasiliano ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mhe. Hamza Hassan Juma akizungumza na menejiment ya TMA walipotembelea ofisi za TMA, Dar es Salaam, Tarehe 21/01/2020
Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Ardhi na Mawasiliano ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mhe. Suleimani Sarahani Said akizungumza na menejiment ya TMA walipotembelea ofisi za TMA, Dar es Salaam, Tarehe 21/01/2020
Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya TMA Dkt. Makame Omar Makame pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa TMA, Dkt. Agnes Kijazi wakifafanua jambo kwa wajumbe wa Kamati ya Ardhi na Mawasiliano ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar walipotembelea ofisi za TMA, Dar es Salaam, Tarehe 21/01/2020
Mkurugenzi Ofisi ya Zanzibar-TMA, Mohamed Ngwali akifafanua jambo kwa wajumbe wa Kamati ya Ardhi na Mawasiliano ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar walipotembelea ofisi za TMA, Dar es Salaam, Tarehe 21/01/2020
Meneja Mipango-TMA, Kidimwa S. Kidimwa akiwasilisha taarifa ya TMA kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu kwa wajumbe wa Kamati ya Ardhi na Mawasiliano ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar walipotembelea ofisi za TMA, Dar es Salaam, Tarehe 21/01/2020
Mjumbe wa Kamati ya Ardhi na Mawasiliano ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mhe. Ussi Yahya Haji akifuatilia jambo wakati walipotembelea ofisi za TMA, Dar es Salaam, Tarehe 21/01/2020


Dar es Salaam, Tarehe 21/01/2020:

 “Iko haja ya kuangalia ukusanyaji wa mapato ili kusaidia katika uwekezaji mkubwa wa huduma za hali ya hewa nchini, sisi tutalifuatilia hili ila na nyie muweza kujipanga vizuri”. Alizungumza Mhe. Hamza Hassan Juma, Mwenyekiti Kamati ya Ardhi na Mawasiliano ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar wakati wa ziara katika ofisi za Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), ambaye aliambatana na wajumbe wengine wa kamati hiyo.

Mhe. Hamza Hassan Juma alizitaka taasisi zinazotumia huduma za hali ya hewa kibiashara kuchangia huduma hizo za hali ya hewa kwa vile huduma hizo zimekuwa zikitumiwa katika kufanikisha shughuli za taasisi hizo kila siku, huku akitolea mfano wa huduma za bandarini na viwanja vya ndege ambazo ufanisi wake unategemea kwa kiasi kikubwa huduma za hali ya hewa.

Kwa upande mwingine, Mhe. Hamza Hassan Juma alifurahishwa na kazi nzuri inayofanywa na TMA katika kutoa tahadhari za hali mbaya ya hewa na hivyo kusaidia wananchi kukabiliana na athari zinazoweza kujitokeza, sambamba na hayo alifurahishwa pia na kuimairishwa kwa muungano kwa vile Bodi ya TMA hivi sasa ina makamu mwenyekiti anayetokea Zanzibar.

‘Bila Mamlaka ya Hali ya Hewa maisha ya watanzania yangekuwa ya kubahatisha, huko nyuma watu walikuwa hawafuatilii utabiri wa hali ya hewa ila kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa (climate change) kumekuwa na haja ya kujua hali ya hewa itakavyokuwa kwa siku za mbele ili kupanga vyema shughuli za maendeleo’. Alisema Mhe, Hamza Hassan Juma

 Naye makamu mwenyekiti wa Bodi ya TMA, Dkt. Makame Omar Makame alitoa shukrani za dhati kwa wajumbe waliofika na kuahidi kufanyia kazi mawazo yaliyotolewa ikiwemo njia za usambazaji taarifa za hali ya hewa kupitia vyombo vya habari (chaneli) za dini na awali aliwaeleza wajumbe kuhusu mabadiliko ya TMA kisheria.

Wakati wa ukaribisho na utambulisho Mkurugenzi Mkuu wa TMA, Dkt. Agnes Kijazi, aliwakaribisha wajumbe na kuwashukuru kwa kutembelea TMA kwa mara nyingine tokea mwaka 2017, vile vile aliwasilisha taarifa ya Mamlaka ambayo iliweza kuonesha huduma mbalimbali za TMA na utekelezaji wa maagizo yaliyotolewa na kamati hiyo mwaka 2017 ikiwa ni pamoja na kufanikisha ukarabati wa jengo la ofisi ya TMA, Chukwani, Zanzibar.

Wajumbe wa Kamati hiyo walifurahishwa na utendaji wa TMA na kwa umoja wao waliipongeza Mamlaka kwa kazi nzuri wanayofanya katika kuokoa Maisha ya watu na mali zao. Aidha walitaka TMA kuendelea  kutoa elimu (awareness) ili wananchi hasa wavuvi wazitumie taarifa za hali ya hewa.
 ‘kila inapotokea hali mbaya ya hewa kwa maeneo ya bahari watu wa visiwani hususani Pemba huwa wanaathirika kwasababu ya ufuatiliaji usioridhisha wa taarifa zinazotolewa na TMA, kuna haja ya kutoa elimu kwa jamii hadi kufikia ‘level’ ya familia’ alisema Mhe. Sulemani Sarahani Said makamu mwenyekiti wa kamati hiyo.

katika kuhitimisha ziara yao wajumbe wa kamati walitembelea maeneo mbalimbali na kujionea namna kazi kubwa ya kuandaa utabiri inavyofanyika kwa saa 24, uokozi wa data za hali ya hewa kutoka katika makaratasi (taarifa za muda mrefu kuanzia 1800) na kuziweka katika mfumo wa kidigitali, usambazaji wa taarifa za hali ya hewa kupitia studio ya TMA. Huduma hizo za hali ya hewa zilizoboreshwa ni kichocheo kikubwa katika ukuaji wa uchumi wa nchi yetu. 

IMETOLEWA NA
KITENGO CHA UHUSIANO
MAMLAKA YA HALI YA HEWA TANZANIA

Sunday, January 19, 2020

DKT. BURUHANI NYENZI AMBAE NI RAIS WA TANZANIA METEOROLOGICAL SOCIETY (TMS) NA MAKAMU WA RAIS WA JUKWAA LA KIMATAIFA LA VYAMA VYA WATAALAM WA HALI YA HEWA DUNIANI (IFMS) ANAYESHUGHULIKIA UTAWALA, AYATANGAZA MAFANIKIO YA TMS KATIKA MKUTANO WA SITA WA JUKWAA HILO.



Rais wa Chama cha wataalam wa sayansi ya hali ya hewa Tanzania (TMS) na makamu wa Rais wa IFMS anayeshughulikia masuala ya utawala, Dkt. Buruhani Nyenzi akiwasilisha mada kuhusu shughuli zilizofanywa na TMS kwa mwaka 2019.
Washiriki wa mkutano wa 6 wa IFMS wakiwa katika picha ya pamoja na makamu wa tatu wa Rais wa WMO Dkt. Agnes Kijazi na Katibu mkuu wa WMO Prof. Petteri Taalas wakati wa ufunguzi wa mkutano huo.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) na Makamu wa Tatu wa Rais wa Shirika la Hali ya Hewa Duniani (WMO) akifuatilia mawasilisho mbalimbali yaliyowasilishwa katika  ufunguzi wa mkutano wa sita wa IFMS.
Washiriki wa mkutano wa IFMS wakifuatilia mada iliyowasilishwa na katibu Mkuu wa Shirika la Hali ya Hewa Duniani. Katika meza ya mbele, kulia ni Rais wa IFMS, Dkt. Harinder Ahluwalia na kushoto ni Rais wa TMS na makamu wa Rais wa IFMS, Dkt. Buruhani Nyenzi.

Rais wa Chama cha Wataalamu wa Sayansi ya Hali ya Hewa Tanzania “Tanzania Meteorological Meteorological Society (TMS)”, Dkt. Buruhani Nyenzi amesema kwamba, licha ya changamoto zilizokuwepo katika mwaka 2019, chama hicho kimeweza kupiga hatua katika kutekeleza majukumu yake.  Dkt Nyenzi alisema hayo tarehe 16 Januari 2016 wakati akiwasilisha mada inayohusu shughuli zilizofanywa na TMS kwa mwaka 2019 katika Mkutano wa 6 wa Jukwaa la Kimataifa la Vyama vya Wataalamu wa Hali ya Hewa Duniani “International Forum of Meteorolocal Societies (IFMS) uliofanyika kuanzia tarehe 14 hadi 16 Januari, 2020 Boston nchini Marekani.

Baadhi ya mafanikio yaliyopatikana kwa mwaka 2019 ni pamoja na kuanza kwa mchakato wa kuandaa mpango mkakati wa TMS; kuongezeka kwa idadi ya wanachama; na kushiriki katika kutoa elimu kwa wadau wa huduma za hali ya hewa, jambo ambalo limechangia kuboresha zaidi matumizi ya utabiri wa hali ya hewa utolewao na TMA. Alisema Dkt. Nyenzi. Rais huyo wa TMS ambaye pia ni Makamu wa Rais wa IFMS anayeshughulikia masuala ya utawala alisema ushirikiano uliopo kati ya TMA na TMS unafaa kuigwa na vyama vingine hasa katika nchi za Afrika ambapo vyama vingi vinashindwa kutekeleza majukumu yao kutokana na ushirikiano hafifu na Taasis za hali ya hewa katika nchi hizo. Pamoja na mafanikio hayo changamoto kubwa inayoikabili TMS ni ufinyu wa bajeti, ambapo chanzo kikuu cha mapato ni michango ya wanachama pekee ambayo hata hivyo haitolewi kwa wakati. Aliongeza Dkt. Nyenzi.

Awali akifungua mkutano huo Rais wa IFMS Dkt. Harinder Ahluwalia aliwasisitiza viongozi wa vyama vya wataalamu wa hali ya hewa  na wadau wengine wa sekta binafsi kuunganisha nguvu ili kusaidia kukuza sekta ya hali ya hewa. Alifafanua ushirikiano uliopo kati ya IFMS na WMO na akamshukuru Dkt. Agnes Kijazi ambaye ni makamu wa tatu wa Rais wa WMO kwa kuhudhuria ufunguzi wa mkutano huo. Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Shirika la Hali ya Hewa Duniani (WMO), Prof. Petteri Taalas alisema sekta binafsi, vikiwemo vyama vya wataalamu wa hali ya hewa vinatarajiwa kutoa mchango chanya katika utekelezaji wa mpango mkakati wa WMO, ambao unaenda sambamba na mabadiliko ya kimuundo katika Shirika hilo. Alisema mabadiliko hayo yamelenga kupunguza changamoto za sekta ya hali ya hewa  ili kukidhi mahitaji ya wadau, ambayo yameendelea kuongezeka, hususan katika kipindi hiki ambacho dunia inakabiliwa na changamoto za mabadiliko ya hali ya hewa na tabianchi.

Mkutano wa IFMS umefanyika kwa mujibu wa kalenda ya shughuli zake za mwaka 2019, kwa lengo la kujadili utekelezaji wa shughuli za vyama vya wataalamu wa sayansi ya hali ya hewa vya Nchi wanachama wa WMO. Mkutano huo umefanyika sambamba na mkutano mkuu wa 100 wa Chama cha Wataalamu wa Hali ya Hewa  cha Marekani “100th Annual Meeting of American Meteorological Societies (AMS100).

Featured Post

DKT. KIJAZI: KIWANGO CHA USAHIHI WA UTABIRI WA MSIMU WA VULI 2019 KIWE CHA JUU ZAIDI.

Mkurugenzi mkuu wa TMA na Makamu wa Tatu wa Rais wa Shirika la Hali ya Hewa Duniani Dkt. Agnes Kijazi (katikati mwenye suti nyeusi) waka...