Tarehe
29/08/2019: ‘Kupitia kikao hiki natarajia kiwango cha usahihi wa
utabiri wa msimu huu wa VULI kitakuwa juu zaidi ya misimu yote’, alisema Dkt.
Kijazi, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA)
na Makamu wa tatu wa Rais wa Shirika la Hali ya Hewa Duniani (WMO) .
Alisema hayo wakati wa
kikao kazi kilichowakutanisha wanasayansi wa hali ya hewa (meteorologists) ili
kujadili rasimu ya utabiri/mwelekeo wa msimu wa mvua za vuli Oktoba hadi
Desemba 2019 .
Aidha, Dkt. Agnes Kijazi
alisisitiza kwa kuwajulisha washiriki hao kuwa TMA inategemea kuzinduliwa rasmi
kutoka ‘Agency’ kwenda ‘Authority’ tarehe 05 Septemba mwaka huu, hivyo ni vyema
wakatambua kwamba wanapaswa kufanyakazi kwa bidii ili kukidhi mategemeo ya
wadau. Alisema, kazi kubwa waliyonayo kwasasa ni kuhakikisha mwelekeo wa msimu
wa mvua za vuli 2019 unakuwa wenye manufaa na tija kwa watumiaji kwa kwa na
usahihi na usambazaji wa viwango vya juu zaidi.
TMA imewakutanisha
wanasayansi kutoka vituo vyake mbalimbali nchini ikiwa ni mwendelezo wa utamaduni
wake wa utendaji kazi wa pamoja. Mwelekeo wa msimu wa mvua za vuli 2019
utatolewa rasmi tarehe 03 Septemba 2019.
No comments:
Post a Comment