Tuesday, August 4, 2026

WATAALAM WA TANROADS WASISITIZWA KUZINGATIA MATUMIZI YA TAARIFA ZA HALI YA HEWA KATIKA KUPANGA NA KUTEKELEZA SHUGHULI ZA UJENZI

 





Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imesisitiza umuhimu wa kuzingatia  matumizi ya taarifa za hali ya hewa katika utekelezaji wa miradi ya ujenzi wa miundombinu ikiwemo barabara na madaraja . 


Akizungumza na viongozi na watumishi mbalimbali wa  Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS)- DODOMA, katika kikao kilichofanyika leo kati ya TMA na Menejimenti na Wataalamu wa TANROAD -Dodoma, Mkurugenzi Mkuu wa TMA na Makamu Mwenyekiti wa Jopo la Kimataifa ya Sayansi ya Mabadiliko ya Hali ya Hewa na Tabianchi, Dkt.Ladislaus Chang’a, alisema “Dunia inakabiliwa na changamoto ya kasi kubwa ya ongezeko la joto, idadi na ukubwa wa matukio ya hali mbaya ya hewa ikiwemo mvua kubwa, mafuriko, upepo mkali na ukame. Matukio haya ya hali mbaya ya hewa yanaendelea kuhatarisha maisha ya watu na mali zao, ikiwemo uharibifu wa miundombinu mbalimbali ikiwemo ya barabara na madaraja". 


Aidha, aliongeza kwa kusema kuwa mwaka huu 2026, dunia inakabiliwa na changamoto ya El Nino, ambayo inatarajiwa kuendelea kuimarika kuelekea mwishoni mwa mwaka. Mamlaka ya Hali ya Hewa inaendelea kufuatilia kwa karibu na itatoa taarifa ya kina kuhusu mwelekeo na athari za El-Nino 2026 tarehe 18/08/2026 wakati wa kutoa utabiri wa mvua za VULI. 


Dkt. Chang’a alisisitiza umuhimu wa kuzingatia sheria ya Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania Na. 2 ya Mwaka 2019 katika matumizi ya taarifa na huduma za hali ya hewa katika sekta zote za kiuchumi na kijamii ili kuokoa maisha ya watu na mali zao, na pia kuongeza ufanisi na tija katika shughuli zote za kimaendeleo.


Hatua na mikutano hii ni mwendelezo wa mkakati wa kuhamasisha matumizi ya taarifa na  huduma za hali ya hewa katika mipango na maendeleo ya Taifa, hususan kipindi hiki ambapo Dunia kwa ujumla inakabiliwa na changamoto za mabadiliko ya hali ya hewa.

MAONESHO YA NANENANE YAWA CHANZO CHA ELIMU YA HALI YA HEWA KWA WADAU.

3 Agosti 2026, Dodoma.








Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) inashiriki  katika maonesho ya NaneNane  2026 yanayofanyika  kuanzia tarehe 1 hadi 8 Agosti 2026,katika viwanja vya John Malecela, Nzunguni jijini Dodoma.


Maonesho hayo yanatoa fursa kwa wadau mbalimbali kupata elimu ya hali ya hewa, shughuli mbalimbali zinazotekelezwa na TMA,ikiwemo shughuli ya uthibiti na uratibu wa huduma za hali ya hewa nchini.


TMA inashiriki katika maonesho ya Kikanda Mbeya na Morogoro. 


Kaulimbiu ya mwaka huu ni ‘‘Tambua soko, Ongeza tija, Tekeleza Diira 2050

Featured Post

DKT. KIJAZI: KIWANGO CHA USAHIHI WA UTABIRI WA MSIMU WA VULI 2019 KIWE CHA JUU ZAIDI.

Mkurugenzi mkuu wa TMA na Makamu wa Tatu wa Rais wa Shirika la Hali ya Hewa Duniani Dkt. Agnes Kijazi (katikati mwenye suti nyeusi) waka...