Wednesday, July 1, 2020

BODI YA TMA YAKAGUA UTEKELEZAJI WA MRADI WA RADA YA HALI YA HEWA MTWARA.

Wajumbe wa Bodi ya TMA katika picha ya pamoja katika ziara ya ukaguzi wa utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa Rada ya hali ya hewa - Mtwara.
Mkurugenzi Mkuu wa TMA na Makamu wa Tatu wa Rais wa Shirika la Hali ya Hewa Duniani (WMO) Dkt. Agnes Kijazi, akiwapokea wajumbe wa Bodi ya TMA mara walipowasili katika ofisi za TMA, Kanda ya Kusini ili kupata taarifa ya utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa Rada ya hali ya hewa - Mtwara
Mkurugenzi Mkuu wa TMA na Makamu wa Tatu wa Rais wa Shirika la Hali ya Hewa Duniani Dkt. Agnes Kijazi, akikaribisha wajumbe wa Bodi ya TMA kabla ya kupata taarifa ya utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa Rada ya hali ya hewa unaoendelea Mtwara.
Meneja wa Kanda ya Kusini TMA, ndugu Amasi Daudi akitoa taarifa ya Kanda ya Kusini.

Msanifu Majengo - TMA, Alfa Buzenzeli akielezea hatua mbalimbali zilizopitiwa katika utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa Rada ya hali ya hewa - Mtwara.
Muhandisi, Mugundu Rambika akielezea jinsi mtambo wa Rada utakavyofanya kazi na manufaa yake katika kuboresha utabiri wa hali ya hewa kwa wajumbe wa Bodi ya TMA walipofanya ziara ya ukaguzi wa utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa Rada ya hali ya hewa - Mtwara.

Mwenyekiti wa Bodi ya TMA, Dkt. Buruhani Nyenzi akipokea taarifa ya utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa Rada ya hali ya hewa - Mtwara kutoka kwa Meneja wa Kanda ya Kusini TMA, ndugu Amasi Daudi.
Wajumbe wa Bodi ya TMA, wakikagua baadhi ya vifaa vya Rada za hali ya hewa vilivyokwisha kuwasili hapa nchini katika utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa Rada ya hali ya hewa unaoendelea Mtwara.
Wajumbe wa Bodi ya TMA, wakipewa elimu ya namna vifaa vya hali ya hewa vinavyopima taarifa za hali ya hewa, walipofanya ziara ya kukagua utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa Rada ya hali ya hewa unaoendelea Mtwara.
Mwenyekiti wa Bodi ya TMA, Dkt. Buruhani Nyenzi akisisitiza jambo wakati bodi hiyo ilipotembelea kituo cha hali ya hewa TMA - Mtwara katika ziara iliyoifanya ya kukagua utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa Rada ya hali ya hewa unaoendelea Mtwara.
Wajumbe wa Bodi ya TMA, wakipewa elimu ya namna vifaa vya hali ya hewa vinavyopima taarifa za hali ya hewa, walipofanya ziara ya kukagua utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa Rada ya hali ya hewa unaoendelea Mtwara.
Wajumbe wa Bodi ya TMA wakipata maelezo ya namna kifaa cha kupima mnunurisho wa jua kinavyofanya kazi, walipofanya ziara ya kukagua utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa Rada ya hali ya hewa unaoendelea Mtwara.
Wajumbe wa Bodi ya TMA wakipata maelezo ya namna kifaa cha kupima mvukisho wa maji angani kinavyofanya kazi, walipofanya ziara ya kukagua utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa Rada ya hali ya hewa unaoendelea Mtwara.
Wajumbe wa Bodi ya TMA katika picha ya pamoja walipotembelea ofisi ya TMA, Kanda ya Kusini, walipofanya ziara ya kukagua utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa Rada ya hali ya hewa unaoendelea Mtwara.
Kibao kilichopo Barabara Kuu - Mtwara, kinachoelekeza barabara ya mchepuko kuelekea kwenye Rada ya hali ya hewa.
Wajumbe wa Bodi ya TMA, wakipewa maendeleo ya mradi na Msanifu Majengo kutoka Wakala wa Majengo Tanzania, Ndugu Godfrey Semi, walipofanya ziara ya kukagua utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa Rada ya hali ya hewa unaoendelea Mtwara
Meneja wa mipango na ufuatiliaji-TMA, ndugu. Shabani Kidimwa akifafanua jambo wakati wajumbe wa bodi ya TMA walipofika katika eneo la ujenzi wa mradi wa Rada ya hali ya hewa unaoendelea Mtwara
Wajumbe wa Bodi ya TMA wakikagua bango lililosimikwa kuutambulisha mradi wa ujenzi wa Rada ya hali ya hewa unaoendelea Mtwara.
Baadhi ya mafundi wakiendelea na ujenzi wa uzio wa ukuta unaozunguka majengo na eneo itakaposimikwa Rada ya hali ya hewa - Mtwara.
Wajumbe wa Bodi ya TMA katika picha ya pamoja wakiwa na baadhi ya wafanyakazi wa TMA na wakandarasi wa mradi wa Rada ya hali ya hewa unaoendelea Mtwara.

Mtwara,Tarehe 28/06/2020:
Bodi ya Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imefanya ziara ya ukaguzi wa utekelezaji wa mradi wa Rada ya hali ya hewa unaogharimu kiasi cha zaidi ya Tsh. Bilioni 6, rada hiyo inayotarajiwa kufungwa katika kilima cha Mbae, Mtwara, ambapo utekelezaji wake umefikia zaidi ya asilimia 80 na kuleta maendeleo mbalimbali ikiwemo miundombinu ya barabara, maji na umeme kwa kaya zaidi ya 750 za Mtaa wa Mbae ‘A’.

Akizungumza baada ya kukagua majengo ya eneo hilo, Mwenyekiti wa Bodi hiyo Dkt. Buruhani Nyenzi kutoka Dar es Salaam alimtaka mkandarasi ahakikishe anamaliza sehemu iliyobaki kulingana  na makubaliano ya mkataba pamoja na kuwa imetokea changamoto ya COVID 19 iliyopelekea wataalamu wanaotakiwa kuja kuifunga rada hiyo kutoka Marekani kushindwa kufanya hivyo.

Aidha, aliishukuru Serikali kwa kutoa fedha nyingi kwa ajili ya Rada hiyo kwa vile itakuwa msaada mkubwa kwa wananchi wa mikoa ya Kusini, huku akiomba uongozi wa mkoa wa Mtwara kuhakikisha eneo la Rada linakuwa salama wakati wote.

“Ningeomba sana uongozi wa mkoa wajaribu kuangalia barabara isiharibike, hili ni tatizo ambalo nimeliona sehemu nyingine, barabara kama hii imetengenezwa baada ya muda unakuta imeharibika kwa sababu ya kukosa usimamizi wa kutosha kutoka katika uongozi wa eneo husika”. Alizungumza Dkt. Nyenzi

                                                                                                                         
Kwa upande mwingine, Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya TMA, Prof. Makame Omar Makame kutoka Zanzibar alielezea shukrani zake kwa serikali kwa vile umuhimu wa rada hiyo ni kwa manufaa ya nchi nzima kwa vile taarifa zitazopatikana zitasaidia maendeleo ya nchi katika sekta mbalimbali kama vile usafiri wa baharini, nchi kavu, uvivu, kilimo n.k

“Rada hii ni muhimu kwa mwambao wa bahari ikiwemo visiwa vya Unguja na Pemba lakini pia katika mwambao wa Dar es Salaam mpaka kufikia Mtwara, hivyo kumalizika kwake kutatoa fursa ya kupata taarifa zenye usahihi wa utabiri wa hali ya hewa kwa shughuli mbalimbali”. Aliongezea Prof. Makame.

Naye Mkurugenzi Mkuu wa TMA na makamu wa tatu wa rais wa Shirika la Hali ya Hewa Duniani, Dkt. Agnes Kijazi aliishukuru Bodi hiyo kwa kutembelea eneo la Rada na pia aliishukuru Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli kwa kuendelea kuboresha huduma za hali ya hewa nchini. Alieleza kuwa, ufungwaji wa rada hiyo utasaidia wananchi wa mikoa ya kusini kupata taarifa sahihi kwa vile ina uwezo wa kuona maeneo madogomadogo zaidi na kuweza kutambua aina ya mvua,  eneo mvua inaponyesha, kuona matone ya mvua, vimbunga na hivyo kusaidia kuboresha utabiri kwa ujumla.  

“Serikali imekwisha kulipia rada mbili ambazo zitafungwa Mbeya na Kigoma, hapo utaona katika mtandao wa rada ukijumuisha Dar es Salaam, Mwanza na hii ya Mtwara utakuwa umefikia rada tano lakini matarajio yetu ni kuwa na rada saba nchini, tayari Mamlaka imekwisha kutengewa bajeti katika mwaka wa fedha 2020/21 ya kufunga rada mbili za Dodoma na Kilimanjaro, hivyo kufikia mwaka ujao wa fedha, Mamlaka itakuwa imekamilisha idadi ya rada saba zinazohitajika nchini”.  Aliongeza Dkt. Kijazi.

Aliendelea kwa kuelezea vifaa vyote vya rada vimekwishafika na kwamba wanasubiriwa wataalamu kutoka Marekani ambao wamekwama kutokana na janga la COVID 19, vile vile alieleza kuwa eneo hilo la ujenzi limejumuisha jengo la mtambo, jengo la wataalamu, jengo la mlinzi, ukuta na mnara utakaoshika antenna ya rada. Kwa upande wa namna TMA ilivyojipanga, Dkt. Kijazi alisema tayari waatalam wa ndani wamepatiwa mafunzo ikiwa na kufanikiwa kufika mpaka kiwandani, hivyo kazi iliyobakia ni kuleta matokea chanya kwa maendeleo ya nchi.

Ziara ya Bodi hiyo ilifanikiwa pia kwa kutembelea ofisi ya TMA Kanda-Mtwara na kujionea shughuli za Ofisi hiyo pamoja na kupata taarifa fupi ya Kanda kutoka kwa Meneja wa Kanda hiyo Ndugu. Amas Daudi. 

Featured Post

DKT. KIJAZI: KIWANGO CHA USAHIHI WA UTABIRI WA MSIMU WA VULI 2019 KIWE CHA JUU ZAIDI.

Mkurugenzi mkuu wa TMA na Makamu wa Tatu wa Rais wa Shirika la Hali ya Hewa Duniani Dkt. Agnes Kijazi (katikati mwenye suti nyeusi) waka...