Saturday, April 24, 2021

MWENENDO WA KIMBUNGA “JOBO” KATIKA PWANI YA TANZANIA

 


Dar es Salaam, 24 Aprili 2021 mchana:

Taarifa hii inahuisha taarifa ya kimbunga Jobo” iliyotolewa na Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania leo asubuhi tarehe 24/04/2021. Mwenendo wa kimbunga “Jobo” kilichopo bahari ya Hindi unaonyesha kuwa kitovu cha kimbunga hicho kipo umbali wa kilomita 76 mashariki mwa kisiwa cha Mafia.

Kimbunga “Jobo” kwa sasa kinasafiri kwa kasi ya kilometa 20 kwa saa baharini ambayo ni kasi kubwa kwa mwenendo wa vimbunga. Kutokana na kasi hiyo kubwa, kisiwa cha Mafia na maeneo jirani yanatarajiwa kuanza kupata mvua kubwa mapema zaidi leo jioni tarehe 24/04/2021.

Kwa upande mwingine, kuanzia usiku wa kuamkia Jumapili tarehe 25/04/2021, maeneo ya kusini mwa mikoa ya Pwani na Dar Es Salaam yanatarajiwa kupata mvua kubwa wakati maeneo mengine ya Lindi, Mtwara na kisiwa cha Unguja pia yanatarajiwa kupata vipindi vya mvua kubwa siku ya kesho Jumapili tarehe 25/04/2021 kwa baadhi ya maeneo. Aidha, pamoja na upepo wa kimbunga kupungua kwa kiasi kikubwa, vipindi vya upepo mkali vinaweza kujitokeza hususan wakati wa mvua kubwa.

USHAURI: Wananchi wanashauriwa kuendelea kufuatilia na kuzingatia taarifa za utabiri kutoka Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania pamoja na kupata ushauri na miongozo ya wataalam katika sekta husika ili kupunguza athari zinazoweza kujitokeza. Izingatiwe kuwa vipindi vya mvua kubwa vinaweza kusababisha mafuriko.

MWENENDO WA KIMBUNGA JOBO KATIKA PWANI YA TANZANIA

 


Dar es Salaam, 24 Aprili 2021 asubuhi:

Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) inaendelea kutoa taarifa ya mwenendo wa kimbunga “Jobo” kilichopo bahari ya Hindi. Kimbunga “Jobo” kipo umbali wa kilomita 200 mashariki mwa kisiwa cha Mafia. Kimbunga hicho kimepungua nguvu kwa haraka baada ya kuingia katika mazingira yenye mzunguko wa upepo kinzani. Hivyo, “Jobo” kwa sasa ni kimbunga hafifu kinachosafiri kwa kasi ya kilometa 18 kwa saa baharini.

Hata hivyo, kimbunga hafifu “Jobo” kinatarajiwa kusababisha vipindi vya mvua kubwa katika maeneo machache hususan ya ukanda wa Pwani kadri kinavyosogea nchi kavu kwa siku ya leo tarehe 24 na kesho 25 mwezi Aprili, 2021. Izingatiwe kuwa uwepo wa kimbunga hafifu baharini, unatarajiwa kusababisha mawimbi makubwa.

Maeneo yanayotarajiwa kupata athari za moja kwa moja ni pamoja na mikoa ya Mtwara, Lindi, Pwani (ikiwemo kisiwa cha Mafia), Dar es Salaam pamoja na kisiwa cha Unguja.

USHAURI: Wananchi wanashauriwa kuendelea kufuatilia na kuzingatia taarifa za utabiri kutoka Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania pamoja na kupata ushauri na miongozo ya wataalam katika sekta husika ili kupunguza athari zinazoweza kujitokeza.


Friday, April 23, 2021

MWENENDO WA KIMBUNGA JOBO KATIKA PWANI YA TANZANIA


 Dar es Salaam, 23 Aprili 2021:

Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) inaendelea kutoa taarifa ya mwenendo wa kimbunga “Jobo” kilichopo bahari ya Hindi. Kimbunga Jobo kimeendelea kusogea kuelekea maeneo ya pwani ya nchi yetu ambapo usiku wa kuamkia tarehe 24/4/2021 (Jumamosi) kimbunga hiki kinatarajiwa kuwa umbali wa takriban kilomita 235 mashariki mwa kisiwa cha Mafia. Jumamosi mchana kimbunga Jobo kinatarajiwa kuwa umbali wa takribani kilomita 125 mashariki mwa Mafia. Aidha, usiku wa kuamkia Jumapili tarehe 25 Aprili 2021, kimbunga Jobo kinatarajiwa kuendelea kupungua nguvu na kuwa mgandamizo mdogo wa hewa kikiwa katika mwambao wa pwani ya Tanzania.

 

Vipindi vya upepo mkali unaofikia kilometa 50 hadi 60 kwa saa, mawimbi makubwa baharini pamoja na ongezeko la mvua kwa maeneo ya ukanda wa pwani vinatarajiwa kujitokeza. Maeneo yanayotarajiwa kupata athari za moja kwa moja kutokana na kimbunga Jobo ni pamoja na mikoa ya Pwani (ikiwemo kisiwa cha Mafia), Lindi, Dar es Salaam pamoja na kisiwa cha Unguja. Aidha, maeneo mengine yanayotarajiwa kuathirika ni mikoa ya Mtwara, Tanga pamoja na kisiwa cha Pemba. Hata hivyo, izingatiwe kuwa uwepo wa kimbunga Jobo unatarajiwa kuendelea kutawala na kuathiri mifumo ya hali ya hewa hapa nchini na kusababisha ongezeko/ vipindi vya mvua kwa maeneo mengine yaliyo mbali na ukanda wa pwani (ikiwemo ukanda wa Ziwa Victoria). 


USHAURI: Wananchi wanashauriwa kuendelea kufuatilia na kuzingatia taarifa za utabiri kutoka Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania pamoja na kupata ushauri na miongozo ya wataalam katika sekta husika ili kupunguza athari zinazoweza kujitokeza.

Thursday, April 22, 2021

TROPICAL CYCLONE “JOBO” IN THE INDIAN OCEAN-NORTH OF MADAGASCAR


Dar es Salaam, 22nd April, 2021:


This statement issues the update of a tropical cyclone named “Jobo” which is currently 

located at the north of Madagascar in the Indian ocean. 

Tropical cyclone Jobo continued to intensify and moved towards our country where 

by during the night of 23th April 2021, the tropical cyclone is expected to be at a 

distance of 410 Kilometres from the coast of Lindi region. However, strength of the 

cyclone Jobo is expected to be reduced as it moved towards the coastal belt of 

Tanzania.


Moreover, the presence of tropical cyclone Jobo may impact weather systems by 

influencing periods of strong winds and enhanced rains along the coastal belts.


ADVISORY: Tanzania Meteorological Agency (TMA) advises all users to make weather 

follow-ups and good use of warnings and weather updates issued by the Tanzania 

Meteorological Agency and to continue seeking and utilizing experts’ advice on their relevant sectors to reduce the associated impacts.


Tanzania Meteorological Authority is continuing to monitor the progress of tropical 

cyclone Jobo and its associated impacts on weather systems and issue updates 

whenever necessary. 

MWENENDO WA KIMBUNGA JOBO KATIKA BAHARI YA HINDI KASKAZINI MWA MADAGASCAR

 


Dar es Salaam, 22 Aprili 2021: 

Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) inaendelea kutoa taarifa ya mwenendo wa kimbunga “Jobo” kilichopo bahari ya Hindi kaskazini mwa kisiwa cha Madagascar.

Kimbunga Jobo kimeendelea kuimarika na kusogea kuelekea maeneo ya nchi yetu ambapo leo usiku wa kuamkia tarehe 23/4/2021 kimbunga hiki kinatarajiwa kuwa umbali wa takriban kilomita 410 kutoka pwani ya mkoa wa Lindi. Hata hivyo, kimbunga Jobo kinatarajiwa kupungua nguvu yake kadri kinavyosogea katika pwani ya Tanzania. 

Aidha, izingatiwe kuwa uwepo wa kimbunga Jobo unatarajiwa kutawala na kuathiri mifumo ya hali ya hewa ikiwa ni pamoja na kusababisha vipindi vya ongezeko la mvua na upepo mkali katika maeneo ya ukanda wa Pwani. 

USHAURI: Wananchi wanashauriwa kuendelea kufuatilia na kuzingatia taarifa za utabiri kutoka Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania pamoja na kupata ushauri na miongozo ya wataalam katika sekta husika ili kupunguza athari zinazoweza kujitokeza.


Wednesday, April 21, 2021

KIMBUNGA JOBO KATIKA BAHARI YA HINDI KASKAZINI MWA MADAGASCAR



Dar es Salaam, 21 Aprili 2021:

Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) inatoa taarifa kuhusu kimbunga Jobo
kaskazini mwa kisiwa cha Madagascar.
Kumejitokeza mgandamizo mdogo wa hewa ambao umefikia kiwango cha kimbunga 
hafifu kwa jina Jobo. Kimbunga hicho kipo kaskazini mwa Kisiwa cha Madagascar
katika Bahari ya Hindi umbali wa Kilometa 930 na kilometa 1030 kutoka pwani ya Lindi 
na Mtwara. Aidha, uwepo wa kimbunga hicho unatarajiwa kusababisha ongezeko la 
upepo na mawimbi katika bahari ya Hindi hususan katika Pwani ya mwambao wa mikoa ya Mtwara na Lindi. 

Mamlaka inaendelea kufuatiliia mwenendo na mwelekeo wa kimbunga Jobo kwa 
kuzingatia mifumo mingine ya hali ya hewa iliyo jirani zaidi na kimbunga hicho ambayo 
inaweza kubadili nguvu na mwelekeo wa kimbunga Jobo katika wakati ujao.
Wananchi waendelee kuzingatia tahadhari ya upepo na mawimbi iliyotolewa na 
Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania katika maeneo husika. Mamlaka ya Hali ya Hewa 
itaendelea kutoa taarifa kila inapobidi. 

Saturday, April 3, 2021

TMA YASAINI MKATABA WA RADA MBILI ZA DODOMA NA KILIMANJARO










 Dar es Salaam; Tarehe 01 Aprili, 2021.

Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), imesaini mkataba wa ununuzi  wa Rada mbili za hali ya hewa zitakazofungwa eneo la Nala mkoani Dodoma na Maretoni, Arumeru mpakani mwa mkoa wa Kilimanjaro na Arusha. 

Akizungumza katika hafla fupi ya kusaini mkataba huo, Mwenyekiti wa Bodi ya TMA, Dkt. Buruhani Nyenzi alisema kuwa ununuzi wa Rada hizo mbili za mwisho unakamilisha mtandao wa Rada saba nchini. 

“Ununuzi wa Rada hizi mbili kwa ajili ya Dodoma na Kilimanjaro unagharimu kiasi cha  dola za kimarekani 4,990,447.00, utengenezaji na ufungaji wake utachukua miezi kumi na nne hadi kukamilika kwake”. Alisema Dkt. Nyenzi. Awali Mwenyekiti huyo wa Bodi, aliwataka washiriki wa hafla hiyo fupi kusimama na kuwa na dakika moja ya utulivu ili kumkumbuka Rais wetu Mpendwa Hayati Dkt. John Joseph Pombe Magufuli ambaye katika kipindi cha uongozi wake huduma za hali ya hewa nchini zimeboreshwa kawa kasi kubwa.

“Rada hizi zinauwezo wa kuona zaidi ya kilometa za mkato 450 huku zikizunguka na kuona matone madogo sana ya mvua katika hali ya uhalisia ndani ya kilometa 250. Aidha, mitambo hii pia inasaidia katika kukusanya data za hali ya hewa zinazoonesha uhalisi wa anga letu la Tanzania”. Aliongeza kusema Dkt. Nyenzi. 

Kwa upande wa Mkurugenzi Mkuu wa TMA na Makamu wa Tatu wa Rais wa Shirika la Hali ya Hewa Duniani (WMO), Dkt. Agnes Kijazi aliishukuru Serikali ya Awamu ya Tano chini ya uongozi wa Hayati Dkt. John Joseph Pombe Magufuli kwa kuiwezesha TMA kutengewa fedha za miradi ya maendeleo ambazo zimefanikisha upatikanaji wa Rada 5.

“Katika kipindi kifupi cha miaka mitano ya uongozi wa Jemadari wetu Hayati Dkt. John Joseph Pombe Magufuli, TMA imeweza kutimiza lengo la kuwa na Rada saba (7) za hali ya hewa nchini, haya ni mafanikio makubwa  sana kwa Mamlaka kuweza kupatikana kwa Rada hizo kwa kipindi kifupi”. Alizungumza Dkt. Kijazi.

Aidha, Dkt. Kijazi aliahidi kuendelea kutoa ushirikiano kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango ili kuhakikisha huduma za hali ya hewa zinatolewa kwa viwango vya kimataifa na hivyo kuweza kusaidia kukuza uchumi wa nchi yetu. “Mabadiliko ya hali ya hewa (Climate change) yamekuwa na athari kubwa duniani kote, ambapo hapa nchini tumeshuhudia kubadilika kwa mifumo ya hali ya hewa yenye athari katika utabiri wa msimu na matukio ya majanga yanayosababishwa na hali mabaya ya hewa, ambapo kuwepo kwa vifaa vya kisasa ukiwepo mtandao wa rada kutaiwezesha TMA kutoa huduma bora kwa maendeleo ya Taifa letu”. Alisistiza Dkt. Kijazi.

Naye, mwakilishi kutoka Kampuni ya Enterprise Electronics Corporation (EEC) kutoka Marekani, Bw. Edwin Kisanga alisema mkataba huo unajumuisha pia mafunzo ya wataalamu kutoka TMA yatakayofanyika hapa nchini na kiwandani kule Marekani.

Mkataba huo umesainiwa baina ya TMA na EEC, ukishuhudiwa na Mwenyekiti wa Bodi ya TMA, Dkt Buruhani Nyenzi, Mjumbe wa Bodi  ya TMA kutoka Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi, Mhandisi Aron Kisaka, Mwanasheria kutoka TMA Adv. Emanuel Ntenga, Mwanasheria kutoka EEC Adv. Seni Malimi, menejimenti ya TMA  na baadhi ya wageni waalikwa.

Kwa sasa Mamlaka imeshafunga Rada tatu katika sehemu za Dar es Salaam, Mwanza na Mtwara, na ipo katika hatua za mwisho za matengenezo ya Rada za Mbeya na Kigoma. TMA inaendelea kusisitizaa wananchi wanaoishi karibu na mitambo ya Rada za hali ya hewa,  kuilinda na kuitunza mitambo hiyo kwa manufaa ya Taifa letu.

Featured Post

DKT. KIJAZI: KIWANGO CHA USAHIHI WA UTABIRI WA MSIMU WA VULI 2019 KIWE CHA JUU ZAIDI.

Mkurugenzi mkuu wa TMA na Makamu wa Tatu wa Rais wa Shirika la Hali ya Hewa Duniani Dkt. Agnes Kijazi (katikati mwenye suti nyeusi) waka...