Thursday, December 24, 2020

SALAMU ZA KRISMAS NA MWAKA MPYA 2021


 Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania tunakutakia Krismas njema na HerĂ­ ya mwaka mpya 2021

Tuesday, December 22, 2020

SERIKALI YAKABIDHIWA RADA YA TATU YA HALI YA HEWA ILIYOPO MTWARA.

Mgeni rasmi ambaye pia ni mwakilishi wa Katibu Mkuu, Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi (Sekta ya Uchukuzi) Mhandisi Aron Kisaka, akizungumza wakati wa makabidhiano ya rada ya tatu ya hali ya hewa iliyopo Mtwara iliyofanyika Makao Makuu ya Mamlaka ya hewa Tanzania, Ubungo Plaza.


Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa na Makamu wa tatu wa Rais wa Shirika la Hali ya Hewa Duniani (WMO) Dkt. Agnes Kijazi (wa pili kulia) akiwa na Mhandisi Aron Kisaka (wa kwanza kushoto), Mwakilishi wa Katibu Mkuu, Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi (Sekta ya Uchukuzi) wakiwa mbele ya gari iliyokabidhiwa na wawakilishi kutoka kampuni ya Enterprise Electronics Corporation (EEC) Makao Makuu ya Mamlaka ya hewa Tanzania, Ubungo Plaza.

 






Picha mbali mbali wakati na baada ya kuweka sahihi kwenye mikataba wakati wa makabidhiano ya rada kutoka kampuni ya Enterprise Electronics Corporation (EEC) katika ofisi za Mamlaka ya hewa Tanzania, Ubungo Plaza.



 

Dar es Salaam; Tarehe 18 Disemba, 2020;

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imekabidhiwa rasmi rada ya tatu ya hali ya hewa ambayo imefungwa katika Kilima cha Mbae, Mtwara. Makabidhiano hayo yamefanyika baini ya Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) na mzabuni Enterprise Electronics Corporation (EEC) kutoka Marekani. Makabidhiano hayo yalifanyika  kwenye kituo kikuu cha utabiri cha TMA, Tarehe: 18 Disemba 2020 na yalishuhudiwa na mwakilishi wa mwenyekiti wa bodi ya TMA.

“Serikali imekamilisha upatikanaji wa rada ya tatu ya hali ya hewa, Rada ya kisasa ni moja ya mitambo michache iliyofungwa Duniani hivyo tunauhakika wa kupata taarifa za hali ya hewa za uhakika na kwa wakati” alisema hayo Mhandisi Aron Kisaka, Mwakilishi wa Katibu Mkuu, Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi (Sekta ya Uchukuzi)  wakati wa makabidhiano hayo.

Aidha aliongeza kwa kuishukuru Enterprise Electronics Corporation (EEC) kwa ushirikiano waliouonesha hata kufanikisha ufungwaji wa rada hiyo ya kisasa hapa nchini na akawataka kuendelea kutoa ushirikiano katika kipindi chote ambacho rada hiyo itakuwa kwenye warranty. Aidha alieleza kuwa uzinduzi rasmi wa Rada ya Mtwara utafanyika hivi karibuni baada ya kumalizika kipindi cha majaribio.

 Kwa upande wa Mkurugenzi Mkuu wa TMA na Makamu wa Tatu wa Rais wa Shirika la Hali ya Hewa Duniani (WMO), Dkt. Agnes Kijazi aliishukuru serikali kwa jitihada zake za kuboresha huduma za hali ya hewa nchini kwa kuendelea kukamilisha ahadi ya kufungwa Rada saba nchi nzima, hii ikiwa rada ya tatu kufungwa na tayari rada zingine mbili zitakazofungwa Mbeya na Kigoma ziko katika hatua za mwisho za matengenezo. 

Naye mwakilishi wa Enterprise Electronics Corporation (EEC) kutoka Marekani Bw. Edwin Kasanga aliihakikishia Serikali kuwa wataendelea kutoa ushirikiano wa dhati ili kuhakikisha miradi inayoendelea inakamilika kwa wakati kulingana na makubaliano ya mikataba. Aidha, akisoma ujumbe Bw. Chris Goode ambaye ni Rais wa EEC, Mhandisi James Youngblood alieleza kuwa pamoja na janga kubwa la virusi vya COVID19 kampuni yake ilipambana kufanikisha makubaliano ya mkataba kwani ilitambua umuhimu wa rada hiyo katika uboreshaji wa huduma za hali ya hewa Tanzania.

Rada ya Mtwara ni rada ya tatu kufungwa nchini, ikiwa ni moja kati ya rada saba zinazotarajiwa kukamilisha mtandao wa rada hapa nchini.

Featured Post

DKT. KIJAZI: KIWANGO CHA USAHIHI WA UTABIRI WA MSIMU WA VULI 2019 KIWE CHA JUU ZAIDI.

Mkurugenzi mkuu wa TMA na Makamu wa Tatu wa Rais wa Shirika la Hali ya Hewa Duniani Dkt. Agnes Kijazi (katikati mwenye suti nyeusi) waka...