Dar es Salaam, 09 Disemba
2019:
Mamlaka
ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) inaendelea kutoa mrejeo wa taarifa iliyotolewa
tarehe 06 Disemba 2019 kuhusu uwepo wa mgandamizo mdogo wa hewa, ulioendelea
kuimarika kaskazini mwa kisiwa cha Madagascar na kufikia kiwango cha kuwa
kimbunga ‘Belna’.
Kimbunga
‘Belna’ kilichopo kusini magharibi mwa bahari ya Hindi (karibu na kisiwa cha Madagascar)
kimeendelea kuimarika hali iliyopelekea kuongezeka kwa vipindi vya mvua katika
maeneo machache hapa nchini. Hata hivyo, kimbunga ‘Belna’ kinatarajiwa kuingia
nchini Madagascar mnamo tarehe 10/12/2019, na hivyo kutokuwa na madhara katika
nchi yetu. Hii ni taarifa ya mwisho kuhusiana na kimbunga ‘Belna’.
Aidha,
msimu wa mvua unaendelea katika maeneo mengi nchini (yale yanayopata msimu
mmoja wa mvua pamoja na yale yanayopata misimu miwili ya mvua kwa mwaka), hivyo
vipindi vya mvua vinatarajiwa kuendelea katika maeneo mengi nchini. Hali
kadhalika, vipindi vya joto
vinatarajiwa kuendelea katika maeneo mengi nchini hususan katika nyakati zenye
upungufu wa mvua.
No comments:
Post a Comment