MKURANGA,
PWANI 22/12/2019;
Mkurugenzi
wa Huduma za Utabiri wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), Dkt. Hamza Kabelwa
kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa TMA Dkt. Agnes Kijazi alifungua warsha ya wadau
kutoka sekta mbalimbali iliyohusu matumizi sahihi ya taarifa za hali ya hewa baina
ya muandaaji na mtumiaji wa taarifa za hali ya hewa, iliyofanyika katika ukumbi
wa Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga, Pwani kuanzia Tarehe 22-24 Disemba, 2019.
Katika
hotuba yake Dkt. Kabelwa alisisitiza wadau mara watakapomaliza warsha hiyo
kuchochea matumizi sahihi ya taarifa za hali ya hewa katika sekta zao ili kupunguza
au kuepusha athari zinazoweza kusababishwa na hali mbaya ya hewa.
“Mkiwa
kama kiunganishi kati ya TMA na wananchi
tunawaomba ninyi washiriki kuchochea matumizi sahihi ya taarifa za hali ya hewa
katika sekta zenu”, alisisitiza Dkt. Kabelwa.
Aidha,
washiriki walikumbushwa kutambua kuwa majanga ya asili hayawezi kuepukika, lakini
taarifa zikiwafikia walengwa kabla ya janga husika kutokea basi zitasaidia kujipanga
ili kukabiliana na madhara yanayoweza kujitokeza, hivyo Dkt. Kabelwa aliwataka
washiriki kushirikiana na TMA kuhakikisha taarifa za hali ya hewa zinawafikia
walengwa kwa wakati na kueleweka.
Warsha
hiyo iliandaliwa na TMA na kufadhiliwa na Shirika la Hali ya Hewa Duniani
(World Meteorological Organization – WMO), chini ya mwamvuli wa Programu ya kidunia
ya kuwaongezea ujuzi waandaaji na watumiaji wa taarifa za hali ya hewa barani
Afrika (Weather and Climate Information Services for Africa - WISER).
No comments:
Post a Comment