Friday, May 17, 2024

UWEPO WA KIMBUNGA “IALY” KATIKA BAHARI YA HINDI KASKAZINI MWA MADAGASCAR


Dar es Salaam, 17 Mei 2024:

Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) inatoa taarifa ya uwepo wa kimbunga “IALY” katika Bahari ya Hindi kaskazini mwa kisiwa cha Madagascar.

Mifumo ya hali ya hewa inaonesha kuwa kimbunga hicho kitaendelea kusalia katika Bahari ya Hindi katika eneo kati ya Madagascar na visiwa vya Shelisheli kwa siku nne zijazo kabla ya kuanza kupungua nguvu.

Aidha, kutokana na umbali kutoka nchini, kimbunga hicho hakitarajiwi kuwa na athari za moja kwa moja katika kusababisha ongezeko la mvua nchini. Hata hivyo vipindi vya upepo mkali na mawimbi makubwa vinaweza kujitokeza katika Bahari ya Hindi.

USHAURI: Watumiaji wa bahari na wananchi kwa ujumla wanashauriwa kuendelea kufuatilia na kuzingatia taarifa za utabiri kutoka Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania pamoja na kupata ushauri na miongozo ya wataalam wa kisekta.

Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) inaendelea kufuatilia mwenendo wa kimbunga hicho na athari zake kwa mifumo ya hali ya hewa hapa nchini na itaendelea kutoa taarifa kila inapobidi.

Imetolewa na:
Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania.

Tuesday, May 14, 2024

SEVERE WEATHER FORECASTING PROGRAMME TO OPEN UP NEW COLLABORATION IN AFRICA.

 


















Dar es Salaam, Tanzania, 14 May 2024.

Chairperson of Tanzania Meteorological Authority (TMA) Board, Hon. Judge Mshibe Ali Bakari urged for more collaboration among National Meteorological and Hydrological Services (NMHSs) of Eastern Africa countries to promote innovation and collaboration in addressing challenges facing effectiveness in early warning services specifically forecasting of severe weather events. “I really encourage NMHSs to consider collaborating among yourselves to harness available capacities in our respective countries in ensuring that we achieve the goal of attaining effective early warning services in line with the ‘United Nations Early Warning for All initiative”. Said Hon. Mshibe during the opening ceremony of the Meeting of the Regional Sub-programme Management Team (RSMT) of Severe Weather Forecasting Programme for Eastern Africa (SWFP-EA), on 14 -17 May 2024, Four Points, Dar es Salaam.

He also commented on the role of local capacities and collaboration as the key to complement the global guidance products in enhancing the capacity of Regional Specialized Meteorological Centres and National Meteorological Hydrological Services in provision of improved products and quality services.   

The Acting Director of TMA -Zanzibar Office , Mr. Masoud Faki who represented the Acting Director General of TMA  said, among the benefits that TMA acquired through the implementation of Severe Weather Forecasting Programme are Weather Forecast Guidance products from the Contributing Global and Regional Meteorological Centers which have demonstrated to be highly useful in preparation of National level weather forecasts through the cascading approach involving downscaling to the national domain.

“TMA has been given the role by WMO to oversee activities of the “Regional Specialized Meteorological Centre – Dar es Salaam (RSMC-Dar es Salaam)” with the responsibilities of preparing and issuing severe weather forecast guidance products for the Lake Victoria basin for use by the National Meteorological and Hydrological Services (NMHSs) of Eastern African countries around Lake Victoria basin”, Explained Mr. Masoud.

On the other hand, Representatives of WMO Secretariat Dr. Ata Hussain expressed his sincere appreciation to the United Republic of Tanzania for hosting important gathering which seeks to improve early warning services, specifically forecasting of severe weather events in Eastern African countries with the aim of reducing fatalities associated with weather hazards. This meeting is therefore of vital importance to the work of National Meteorological and Hydrological Services (NHMSs) in enhancing Early Warning Services delivery, particularly Severe Weather Forecasting to support Disaster Risk Reduction in the Eastern Africa Sub-region in line with the “United Nations’ Early Warning for All” initiative.

Participants were from Tanzania, Burundi, Djibouti, Ethiopia, Kenya, Rwanda, Somalia, Sudan, Uganda, Djibouti, Somalia, South Sudan and other experts from Contributing World Meteorological Centres -WMCs and Regional Specialized Meteorological Centres -RSMCs.


NCHI ZA KANDA YA AFRIKA MASHARIKI ZASISITIZWA USHIRIKIANO KUKABILIANA NA HALI MBAYA YA HEWA

 



















Dar es Salaam, Tanzania: 14 Mei, 2024.

Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), Mhe. Jaji Mshibe Ali Bakari ametoa rai kwa wataalamu kutoka nchi za Kanda ya Afrika Mashariki kuboresha ushirikiano ili kuweza kukabiliana na changamoto zinazojitokeza hususani kipindi cha matukio ya hali mbaya ya hewa. Mhe. Mshibe alisema hayo wakati akifungua rasmi Mkutano wa Kamati ya Usimamizi wa Programu ya Shirika la Hali ya Hewa Duniani (WMO) ya Utabiri wa Hali Mbaya ya Hewa kwa nchi Wanachama Kanda ya Afrika Mashariki, unaofanyika Dar es Salaam, 14-17 Mei, 2024.

Aidha, alisisitiza kuwa, mkutano huo umewaleta pamoja wataalamu kutoka nchi za Tanzania, Burundi, Djibouti, Ethiopia, Kenya, Rwanda, Somalia, Sudan, Uganda, Djibouti, Somalia, Eritrea, Sudan Kusini pamoja na Wataalamu wengine kutoka vituo mbalimbali vya Kikanda vya WMO, hivyo kupitia ushirikiano huo huduma za hali ya hewa kwa nchi wanachama wa WMO Kanda ya Afrika Mashariki zinatarajiwa kuboresha huduma zake za hali ya hewa ili kupunguza athari zitokanazo na matukio ya hali mbaya ya hewa.

Akimwakilisha Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TMA, Kaimu Mkurugenzi wa TMA ofisi ya Zanzibar, Bw. Masoud Faki alisema kupitia programu hiyo ya Utabiri wa Hali Mbaya ya Hewa, TMA imeweza kunufaika na masuala mbalimali yakiwemo ya mafunzo kwa wataalamu na miongozo ya pamoja ya utendaji kazi ambayo imesaidia katika maandalizi ya utabiri katika ngazi ya nchi.

Bw. Masoud aliendelea kueleza kuwa mwaka 2019 Tanzania kupitia TMA ilichaguliwa na WMO kuendesha Kituo cha Kanda cha kutoa mwongozo wa utabiri wa hali mbaya ya hewa kwa nchi zilizopo katika Ukanda wa Ziwa Victoria ambazo ni Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda na Burundi.

Katika hatua nyingine, mwakilishi kutoka sekretarieti ya WMO aliishukuru Serikali ya Tanzania kukubali kuandaa na kuwa mwenyeji wa mkutano huo muhimu wenye lengo la kuboresha huduma za taarifa za hali mbaya ya hewa kwa nchi wanachama wa Kanda ya Mashariki, lengo ambalo linaenda sambamba na jitihada za Umoja wa Kimataifa.

Featured Post

DKT. KIJAZI: KIWANGO CHA USAHIHI WA UTABIRI WA MSIMU WA VULI 2019 KIWE CHA JUU ZAIDI.

Mkurugenzi mkuu wa TMA na Makamu wa Tatu wa Rais wa Shirika la Hali ya Hewa Duniani Dkt. Agnes Kijazi (katikati mwenye suti nyeusi) waka...