Wednesday, October 27, 2021

SEKTA MBALIMBALI ZASHAURIWA KUJIPANGA KUKABILIANA NA UPUNGUFU WA MVUA ZA MSIMU WA NOVEMBA 2021 HADI APRILI 2022 UNAOTARAJIWA KUJITOKEZA






Dar Es Salaam, Tarehe 27/10/2021.

Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania imetoa rasmi utabiri wa mvua za msimu kwa maeneo yanayopata mvua za msimu mara moja kwa mwaka, ikijumuisha mikoa iliyopo magharibi mwa nchi ( Kigoma, Tabora na Katavi), yyanda za juu kusini magharibi (Rukwa, Mbeya, Songwe, Njombe, Iringa), katikati mwa nchi (Dodoma na Singida), pwani ya kusini (Lindi na Mtwara), mkoa wa Ruvuma pamoja na maeneo yaliyoko kusini mwa mkoa wa Morogoro katika kipindi cha miezi ya Novemba, 2021 hadi Aprili, 2022.

Akiwasilisha utabiri huo kwa waandishi wa habari, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) ambaye pia ni Makamu wa Tatu wa Rais wa Shirika la Hali ya Hewa Duniani (WMO) Dkt. Agnes Kijazi alisema kuwa, utabiri huo wa mvua za msimu unatarajiwa kuwa wa wastani hadi chini ya wastani hivyo kuwataka wadau kutoka sekta mbalimbali kuzitumia taarifa hizi za hali ya hewa kwa kujipanga ili kukabiliana na matarajio hayo.

“Natoa ushauri kwa wadau wa sekta mbalimbali wanaotumia taarifa za hali ya hewa katika utekelezaji wa majukumu yao kama vile kilimo na usalama wa chakula, mifugo na uvuvi, maliasili, wanyamapori na utalii, nishati na maji, usafirishaji (nchi kavu, kwenye maji na angani), mamlaka za miji, afya, sekta binafsi pamoja na menejimenti za maafa kujipanga na kutumia njia ambazo zitaweza kukabiliana na upungufu wa mvua unaotarajiwa kujitokeza katika kipindi cha mwezi  Novemba, 2021 hadi Aprili, 2022” Alisema Dkt. Kijazi

Dkt. Kijazi aliongezea kusema, mvua hizo zinatarajiwa kuanza kwa maeneo mengi katika wiki ya tatu ya mwezi Novemba, 2021 na kuisha katikati ya wiki ya pili na ya tatu ya mwezi Aprili, 2022. Hata hivyo, ongezeko kidogo la mvua linatarajiwa mwezi Machi, 2022 katika nusu ya pili ya msimu huo. 

Aidha, Dkt. Kijazi alisisitiza kuwa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania itaendelea kufuatilia mwenendo wa mifumo ya hali ya hewa na kutoa mirejesho ya mwelekeo wa mvua nchini kadri inavyohitajika na kuwashauri wadau kuendelea kuwasiliana na Mamlaka ili kupata taarifa mahsusi za utabiri wa msimu ili kukidhi mahitaji maalum katika sekta zao.

Kwa maelezo kamili kuhusu utabiri huu tembelea: https://www.meteo.go.tz/




Tuesday, October 26, 2021

TMA YATOA TUZO KWA WANAHABARI BORA WA TAARIFA ZA HALI YA HEWA 2021.



Dar es Salaam, Tarehe 26/10/2021

Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imetoa tuzo kwa wanahabari bora wa taarifa za hali ya hewa 2021, tuzo hizo zimetolewa kwa wanahabari waliofanya vizuri katika kutoa taarifa za hali ya hewa kwa jamii kwa kipindi cha mwaka mmoja kuanzia Septemba 2020 hadi Julai 2021 katika ukumbi wa mikutano wa Baraza la Wakunga na Wauguzi Tanzania – Kibaha. 

Tuzo hizo zilitolewa rasmi na Mwenyekiti wa Bodi ya TMA, Dkt. Buruhani S. Nyenzi katika warsha ya wanahabari inayohusu mwelekeo wa mvua za msimu kwa kipindi cha mwezi Novemba 2021 hadi Aprili 2022, ambaye aliwapongeza washindi wa tuzo hizo na kuwapa hamasa wengine kuendelea kufanya kazi hizo kwa weledi ili ziweze kutambuliwa na Mamlaka na kuwa sehemu ya mchakato wa Tuzo hizo katika wakati ujao.

“Napenda kutumia nafasi hii kuwapongeza sana na kuwapa hamasa wengine kuendelea kufanya kazi bora zaidi na kuwasilisha taarifa za kazi zenu ili ziweze kutambuliwa na Mamlaka na kuwa sehemu ya mchakato wa tuzo hizo katika wakati ujao”. Alizungumza Dkt. Nyenzi.

Awali wakati wa ufunguzi wa warsha hiyo, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) ambaye pia ni Makamu wa Tatu wa Rais wa Shirika la Hali ya Hewa Duniani (WMO), Dkt. Agnes Kijazi alieleza kuwa kwa kipindi kirefu sasa TMA imeendelea kuandaa warsha kwa wanahabari kila inapokaribia kutoa utabiri wa msimu wa mvua, na aliahidi kuendeleza utaratibu huo ili kuhakikisha taarifa za hali ya hewa zinawafikia walengwa kwa usahihi na kwa wakati.

Utabiri wa msimu wa mvua za Vuli 2021 unatarajiwa kutolewa rasmi Tarehe 27/10/2021, katika ukumbi wa mikutano wa TMA, Ghorofa ya tatu, Ubungo Plaza, Dar es Salaam.

Monday, October 25, 2021

TMA YATOA MAFUNZO KWA WATUMISHI WA KADA YA HUDUMA SAIDIZI

Mgeni rasmi ambaye pia ni Mkurugenzi wa Tehama na Huduma za Ufundi TMA, Dkt. Pascal Waniha  akizungumza  na watumishi wakati akifungua mafunzo ya kujenga uelewa wa huduma za hali ya hewa kilimo kwa watumishi wa kada ya huduma saidizi ili kuongeza usambazaji na matumizi ya taarifa za hali ya hewa katika kupunguza athari za mabadiliko ya hali ya hewa katika shughuli za kilimo. Mafunzo hayo yalifanyika katika Ukumbi wa Baraza la Wakunga na Manesi, Kibaha, Pwani, tarehe 22-23 Oktoba, 2021.






Watumishi katika TMA wakichangia mada wakati wa mafunzo ya kujenga uelewa wa huduma za hali ya hewa kilimo kwa watumishi wa kada ya huduma saidizi ili kuongeza usambazaji na matumizi ya taarifa za hali ya hewa katika kupunguza athari za mabadiliko ya hali ya hewa katika shughuli za kilimo. Mafunzo hayo yalifanyika katika Ukumbi wa Baraza la Wakunga na Manesi, Kibaha, Pwani, tarehe 22-23 Oktoba, 2021.











Mkurugenzi wa Utafiti na Matumizi ya Hali ya Hewa, Dkt. Ladislaus Chang'a akitoa mafunzo kwa watumishi wa TMA wakati wa Warsha ya kujenga uelewa wa huduma za hali ya hewa kilimo kwa watumishi wa kada ya huduma saidizi ili kuongeza usambazaji na matumizi ya taarifa za hali ya hewa katika kupunguza athari za mabadiliko ya hali ya hewa katika shughuli za kilimo. Mafunzo hayo yalifanyika katika Ukumbi wa Baraza la Wakunga na Manesi, Kibaha, Pwani, tarehe 22-23 Oktoba, 2021.






Mgeni rasmi ambaye pia ni Mkurugenzi wa Tehama na Huduma za Ufundi TMA, Dkt. Pascal Waniha (katikati) katika picha ya pamoja na watumishi wakati wa mafunzo ya kujenga uelewa wa huduma za hali ya hewa kilimo kwa watumishi wa kada ya huduma saidizi ili kuongeza usambazaji na matumizi ya taarifa za hali ya hewa katika kupunguza athari za mabadiliko ya hali ya hewa katika shughuli za kilimo. Mafunzo hayo yalifanyika katika Ukumbi wa Baraza la Wakunga na Manesi, Kibaha, Pwani, tarehe 22-23 Oktoba, 2021.



Pwani; Tarehe 22 – 23 Oktoba, 2021;


Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imetoa mafunzo ya kujenga uelewa wa huduma za hali ya hewa kilimo kwa watumishi wa kada ya huduma saidizi ili kuongeza usambazaji na matumizi ya taarifa za hali ya hewa katika kupunguza athari za mabadiliko ya hali ya hewa katika shughuli za kilimo. Mafunzo hayo yalifanyika katika Ukumbi wa Baraza la Wakunga na Manesi, Kibaha, Pwani, tarehe 22-23 Oktoba, 2021.

 

Akizungumza wakati akifungua Warsha ya Watumishi wa Kada ya Huduma Saidizi mgeni rasmi, ambaye ni Mkurugenzi wa Tehama na Huduma za Ufundi TMA Dkt. Pascal Waniha alisema mafunzo haya ni sehemu ya mkakati wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) wa kuboresha upatikanaji, uelewa na matumizi ya taarifa za hali ya hewa ili kusaidia katika kufanya maamuzi sahihi katika shughuli mbalimbali za kilimo. 

 

“Katika kufanikisha adhima hii, Mamlaka imeona ni vyema kutoa mafunzo kwa watumishi wa kada ya huduma saidizi kwani kutokana na shughuli zenu za kila siku licha ya kukutana na wadau mbalimbali wakiwemo wakulima, shughuli zenu za nje ya kazi kama vile bustani na kilimo zimekuwa zikiathiriwa kutokana na hali ya hewa hivyo kupitia warsha hii mtaweza kuelewa huduma mbalimbali zitolewazo na TMA na mtakuwa na jukumu la kusaidia kuzitafsiri, kuzitumia na kuzisambaza taarifa hizi kwa wadau ili waweze kukabiliana na changamoto zinazotokana na athari ya mabadiliko ya hali ya hewa”. Alizungumza Dkt. Waniha.

 

Awali, wakati akimkaribisha mgeni rasmi, Dkt. Ladislaus Chang’a, Mkurugenzi wa Utafiti na Matumizi ya Hali ya Hewa TMA alimshukuru Mkurugenzi Mkuu wa TMA kwa warsha hii kwani imekuwa sehemu ya historia na kuwahimiza watumishi kujifunza zaidi na zaidi.

 

“Kila siku ni fursa, kama tumepewa fursa ya kuwa sehemu ya historia basi sisi wenyewe tunatakiwa tuwe historia kwa namna tunavyoishi na kwa namna tunavyofanya kazi”. Alisema Dkt. Chang’a.

 

Kwa upande wa watumishi, waliishukuru TMA kwa kuandaa na kuwawezesha kushiriki katika warsha hii ya kujenga uelewa wa huduma za hali ya hewa kilimo ambayo haijawahi kutokea na kuomba mafunzo haya kuwa endelevu.


Friday, October 22, 2021

TMA WAJIPANGA KUTOA UTABIRI KATIKA NGAZI YA WILAYA

Mgeni rasmi ambaye pia ni Mwenyekiti wa Bodi ya TMA Dkt. Buruhani Nyenzi akizungumza wakati akifungua mkutano wa wadau wa Utabiri wa Mvua za Msimu (Novemba, 2021 hadi Aprili, 2022) wenye kauli mbiu “Matumizi sahihi ya utabiri wa maeneo madogomadogo kwa ukuaji wa uchumi wa viwanda”, katika Ukumbi wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT). Utabiri huo unatarajiwa kutolewa rasmi Tarehe 27 Oktoba 2021 katika ukumbi wa mikutano wa TMA, Ghorofa ya tatu, Ubungo Plaza - Dar es Salaam, Tanzania.

Mkurugenzi Mkuu wa TMA na Makamu wa Tatu wa Rais wa Shirika la Hali ya Hewa Duniani Dkt. Agnes Kijazi  akiongea kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi kwa ajili ya ufunguzi wa mkutano wa wadau wa Utabiri wa Mvua za Msimu (Novemba, 2021 hadi Aprili, 2022) wenye kauli mbiu “Matumizi sahihi ya utabiri wa maeneo madogomadogo kwa ukuaji wa uchumi wa viwanda”, katika Ukumbi wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT). Utabiri huo unatarajiwa kutolewa rasmi Tarehe 27 Oktoba 2021 katika ukumbi wa mikutano wa TMA, Ghorofa ya tatu, Ubungo Plaza - Dar es Salaam, Tanzania.

Mkurugenzi wa Huduma za Utabiri wa TMA, Dkt. Hamza Kabelwa  akiongea kabla ya kumkaribisha Mkurugenzi mkuu wa TMA na Makamu wa Tatu wa Rais wa Shirika la Hali ya Hewa Duniani Dkt. Agnes Kijazi katika mkutano wa wadau wa Utabiri wa Mvua za Msimu (Novemba, 2021 hadi Aprili, 2022) wenye kauli mbiu “Matumizi sahihi ya utabiri wa maeneo madogomadogo kwa ukuaji wa uchumi wa viwanda”, katika Ukumbi wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT). Utabiri huo unatarajiwa kutolewa rasmi Tarehe 27 Oktoba 2021 katika ukumbi wa mikutano wa TMA, Ghorofa ya tatu, Ubungo Plaza - Dar es Salaam, Tanzania.

Mtaalam wa Hali ya hewa kutoka TMA, Bw. Ramadhani Omary akiwasilisha mada katika mkutano wa wadau wa Utabiri wa Mvua za Msimu (Novemba, 2021 hadi Aprili, 2022) wenye kauli mbiu “Matumizi sahihi ya utabiri wa maeneo madogomadogo kwa ukuaji wa uchumi wa viwanda”, katika Ukumbi wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT). Utabiri huo unatarajiwa kutolewa rasmi Tarehe 27 Oktoba 2021 katika ukumbi wa mikutano wa TMA, Ghorofa ya tatu, Ubungo Plaza - Dar es Salaam, Tanzania.










Wadau kutoka sekta ya mbalimbali wakichangia mada katika mkutano wa wadau wa Utabiri wa Mvua za Msimu (Novemba, 2021 hadi Aprili, 2022) wenye kauli mbiu ya “Matumizi sahihi ya utabiri wa maeneo madogomadogo kwa ukuaji wa uchumi wa viwanda”, katika Ukumbi wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT). Utabiri huo unatarajiwa kutolewa rasmi Tarehe 27 Oktoba 2021 katika ukumbi wa mikutano wa TMA, Ghorofa ya tatu, Ubungo Plaza - Dar es Salaam, Tanzania.











Wataalam bingwa wa hali ya hewa pamoja na wadau kutoka sekta mbalimbali wakichangia mada katika mkutano wa wadau wa Utabiri wa Mvua za Msimu (Novemba, 2021 hadi Aprili, 2022) wenye kauli mbiu “Matumizi sahihi ya utabiri wa maeneo madogomadogo kwa ukuaji wa uchumi wa viwanda”, katika Ukumbi wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT). Utabiri huo unatarajiwa kutolewa rasmi Tarehe 27 Oktoba 2021 katika ukumbi wa mikutano wa TMA, Ghorofa ya tatu, Ubungo Plaza - Dar es Salaam, Tanzania.










Wataalam bingwa wa hali ya hewa pamoja na wadau kutoka sekta mbalimbali wakiwa katika makundi wakijadili athari na ushauri kwa msimu wa mvua 2021 katika mkutano wa wadau wa Utabiri wa Mvua za Msimu (Novemba, 2021 hadi Aprili, 2022) wenye kauli mbiu “Matumizi sahihi ya utabiri wa maeneo madogomadogo kwa ukuaji wa uchumi wa viwanda”, katika Ukumbi wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT). Utabiri huo unatarajiwa kutolewa rasmi Tarehe 27 Oktoba 2021 katika ukumbi wa mikutano wa TMA, Ghorofa ya tatu, Ubungo Plaza - Dar es Salaam, Tanzania.








Matukio kwa picha wakati wadau wakisikiliza mada mbalimbali zilizowasilishwa katika mkutano wa wadau wa Utabiri wa Mvua za Msimu (Novemba, 2021 hadi Aprili, 2022) wenye kauli mbiu “Matumizi sahihi ya utabiri wa maeneo madogomadogo kwa ukuaji wa uchumi wa viwanda”, katika Ukumbi wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT). Utabiri huo unatarajiwa kutolewa rasmi Tarehe 27 Oktoba 2021 katika ukumbi wa mikutano wa TMA, Ghorofa ya tatu, Ubungo Plaza - Dar es Salaam, Tanzania.

Wadau kutoka sekta mbalimbali wakiwa katika picha ya pamoja na mgeni rasmi katika mkutano wa wadau wa Utabiri wa Mvua za Msimu (Novemba, 2021 hadi Aprili, 2022) wenye kauli mbiu “Matumizi sahihi ya utabiri wa maeneo madogomadogo kwa ukuaji wa uchumi wa viwanda”, katika Ukumbi wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT). Utabiri huo unatarajiwa kutolewa rasmi Tarehe 27 Oktoba 2021 katika ukumbi wa mikutano wa TMA, Ghorofa ya tatu, Ubungo Plaza - Dar es Salaam, Tanzania.
 

Dar es Salaam, Tarehe 21/10/2021

“Utabiri huu wa Msimu utaambatana na utabiri katika ngazi ya Wilaya zilizomo kwenye maeneo yanayopata msimu mmoja wa mvua. Hivyo, nawapongeza sana TMA kwa hatua hii kubwa ya kuongeza wigo wa utoaji utabiri hususani kwa watumiaji wa taarifa za hali ya hewa wa sekta mbalimbali ambao wamekuwa na uhitaji wa taarifa za utabiri wa maeneo madogo madogo kwenye maeneo yao kwa kutumia fursa mbali mbali zilizopo”. Dkt. Buruhani Nyenzi, Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) aliyasema hayo wakati akifungua mkutano wa wadau wa Utabiri wa Mvua za Msimu (Novemba, 2021 hadi Aprili, 2022) wenye kauli mbiu ya “Matumizi sahihi ya utabiri wa maeneo madogomadogo kwa ukuaji wa uchumi wa viwanda”, katika Ukumbi wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT).

Aidha, ili taarifa hizi za utabiri zilizoandaliwa kwa kila wilaya, ziwe na tija iliyokusudiwa  tunahitaji  kuipatia Mamlaka ushirikiano katika kuhakikisha kwamba taarifa hizi zinawafikia watumiaji wa mwisho kwenye sekta mbalimbali ili kuweza kuchangia katika ukuaji wa uchumi. Pia alisema wanapojiandaa kupokea taarifa ya Utabiri wa Msimu wa Mvua za Novemba 2021 hadi April, 2022 ni muhimu sana kila mmoja kufuatilia kwa karibu, kuelewa, kupanga na kukabiliana na hali ya hewa inayotarajiwa katika sekta yake. Aliongezea Dkt. Nyenzi

Kwa upande wake Dkt. Agnes Kijazi, Mkurugenzi Mkuu Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania na Makamu wa Tatu wa Rais wa Shirika la Hali ya Hewa Duniani (WMO) amesema kuwa ni vyema kila wilaya na kila sekta ikatumia taarifa za hali ya hewa katika kufanya maamuzi sahihi na kuweka mipango ili kuboresha huduma zao kwa lengo la kuongeza tija na pia kupunguza athari za hali mbaya ya hewa inapojitokeza.

Aidha, wadau wameipongeza Mamlaka kwa jitihada za kuhakikisha kuwa taarifa hizi za hali ya hewa zinawafikia walengwa wakuu na pia wameitaka Mamlaka kuongeza wigo wa kuifikia jamii ili ipate taarifa kwa wakati na pale inapotokea mabadiliko ya utabiri wa hali ya hewa.

Featured Post

DKT. KIJAZI: KIWANGO CHA USAHIHI WA UTABIRI WA MSIMU WA VULI 2019 KIWE CHA JUU ZAIDI.

Mkurugenzi mkuu wa TMA na Makamu wa Tatu wa Rais wa Shirika la Hali ya Hewa Duniani Dkt. Agnes Kijazi (katikati mwenye suti nyeusi) waka...