|
Mkuu
wa Mkoa Tanga Mhe. Martin Shigela akipokea zawadi toka kwa meneja TMA kituo cha Handeni Ndg. Fabian Severine, alipotembelea banda la TMA katika
maonesho ya siku ya chakula duniani yaliyofanyika katika viwanja vya Handeni
Square, Tanga kuanzia Tarehe 09-14 Disemba, 2019.
|
|
Mkuu
wa Mkoa Tanga Mhe. Martin Shigela akipata elimu kutoka kwa meneja TMA kituo cha Handeni Ndg. Fabian Severine, juu ya namna taarifa za hali ya
hewa zinavyoweza kutumika katika kushauri wadau ili kukabiliana na changamoto
mbalimbali kwenye sekta zao, kupitia maonesho ya "ONE STOP JAWABU"
yaliyofanyika katika viwanja vya Handeni Square, Tanga kuanzia Tarehe 09-14
Disemba, 2019.
|
|
Matukio
mbalimbali katika picha wakati wataalamu wa hali ya hewa kutoka TMA wakiendelea
kutoa elimu kwa wadau, namna ya kutumia ushauri wa kitaalam kutoka TMA ili
kukabiliana na changamoto mbalimbali kwenye sekta zao, kupitia maonesho ya
"ONE STOP JAWABU" yaliyofanyika katika viwanja vya Handeni Square,
Tanga kuanzia Tarehe 09-14 Disemba, 2019.
|
|
Matukio
mbalimbali katika picha wakati wageni wakipokea zawadi mara walipotembelea
banda la TMA kupitia maonesho ya "ONE STOP JAWABU" yaliyofanyika katika
viwanja vya Handeni Square, Tanga kuanzia Tarehe 09-14 Disemba, 2019
|
|
Meneja TMA - Handeni Ndg. Fabian Severine,
akipata nafasi ya upendeleo toka kwa mshereheshaji ili kutoa elimu ya hali ya
hewa katika maonesho ya "ONE STOP JAWABU" yaliyofanyika katika viwanja vya
Handeni Square, Tanga kuanzia Tarehe 09-14 Disemba, 2019
|
Handeni,
14/12/2019;
Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Mhe. Martin
Shigela ameipongeza Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) kwa kuwa mfano katika
utunzaji wa mazingira. Pongezi hizo zilitolewa alipotembelea banda la TMA katika
maonesho ya "ONE STOP JAWABU" ambayo yalifanyika katika viwanja vya
Handeni Square, Tanga kuanzia Tarehe 09-14 Disemba, 2019.
"Nawapongeza kwa kuwa
mfano wa utunzaji wa mazingira kupitia utoaji zawadi za mifuko bora ambayo ni
rafiki wa mazingira". Alisema Mhe. Shigela.
Kupitia maonesho hayo, wadau
mbalimbali waliweza kutembelea banda la TMA na kupata ushauri wa kitaalam juu
ya matumizi sahihi ya taarifa za hali ya hewa katika kukabiliana na changamoto
mbalimbali kwenye sekta zao.
Aidha, kupitia maonesho hayo zaidi
ya wadau 160 waliweza kuelekezwa jinsi ya kupata taarifa za hali ya hewa
kupitia njia mbalimbali za mawasiliano ikiwemo tovuti pamoja na mitandao ya
kijamii ya TMA.
No comments:
Post a Comment