Thursday, October 8, 2026

CLIMATE INFORMATION MUST BE TRANSFORMED INTO DECISIONS AND ACTION.

 





Dar es Salaam, Tanzania, 06 Oktoba 2026.

 

The Tanzania Meteorological Authority (TMA) is hosting a three days Coordinated Regional Climate Downscaling Experiment (CORDEX)-Africa Workshop in Dar es Salaam. The CORDEX workshop provides an opportunity for improving climate resilience and preparedness as climate scientists, researchers, practioners and decision-makers work together to ensure that the climate information is relevant, accessible, usable and positioned to support real-world decision-making.

 

The workshop was officiated by Dr. Ladislaus Chang’a, the Director General of TMA, who is also the Vice-Chair of the Intergovernmental Panel on Climate Change (IPCC) and the Permanent Representative of Tanzania with the World Meteorological Organization (WMO). In his remarks, Dr Chang’a emphasized the importance of linking scientific research with the practical needs of meteorological information users.

“Climate information is most valuable when it meets the needs of decision-makers and helps governments plan, water managers prepare, health authorities forecast risks, farmers increase productivity, and disaster management institutions take timely action.” Said Dr. Chang’a.

 

Dr. Chang’a also pointed out the growing scientific evidence of climate change and the associated extreme weather and climate events which are increasing in magnitude and freaquecy. These extremes include the heavy rainfall, flooding, strong wind, tropical storm, drought and heatwaves. He also highlighed on the forecasted strong El Niño 2026/2027 conditions  and the need for climate scientists to continue to lead in providing scientific evidence for early warning and preparedness in various socio-economic sectors to reduce or avoid the expected impacts.

 

The three-day workshop is being attended by participants from many African countries,  including participants from Tanzania, South Africa, Kenya, Zimbabwe, Egypt, Senegal, Algeria, Cotedvoire, Burkinafaso, Nigeria, Togo, Ghana, Angola, Malawi, Mozambique,  and Cameroon. We also have participants from UK met office.

The workshop also provide opportunity for the experts to discuss ways and mechanism for strengthening the application of research findings into operational climate services at national as well as local government plans. Furthermore, participants are discussing ways to advance scientific collaboration and contribute to the preparation of the IPCC Seventh Climate Change Assessment Report (IPCC AR7). The IPCC Assessment Reports are essential as they provide credible scientific evidence and policy-relevant information that enables governments and stakeholders to formulate and implement policies, strategies and interventions for effective climate change adaptation and mitigation.



Thursday, September 17, 2026

TANZANIA YAZINDUA WISER ACTIONFIRST™ KUIMARISHA TAHADHARI ZA MAPEMA KWA SEKTA ZA KILIMO NA MIFUGO

















Morogoro, 16 Septemba 2026

Tanzania imezindua rasmi programu ya WISER ActionFirst™ inayolenga kuimarisha matumizi ya taarifa za hali ya hewa katika kuchukua hatua za mapema, hususan katika sekta za kilimo na mifugo, ili kupunguza athari za majanga yanayohusiana na hali ya hewa na tabianchi.


Uzinduzi huo umefanyika katika Ukumbi wa CATE Hotel, Morogoro, ukiambatana na Warsha ya Kitaifa ya Ushirikishwaji wa Wadau katika Kuandaa Taarifa Mahususi za Hali ya Hewa kwa Sekta za Kilimo na Mifugo, inayofanyika tarehe 16–18 Septemba 2026.


Akizindua rasmi programu hiyo na kufungua warsha, Mkurugenzi wa Idara ya Menejimenti ya Maafa, Ofisi ya Waziri Mkuu – Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu, Brigedia Jenerali Hosea Maloda Ndagala, alisema Tanzania inalenga kuimarisha mfumo wa tahadhari za mapema unaowezesha wananchi na taasisi kuchukua hatua kabla ya majanga kutokea.


Alisema kutoa utabiri pekee hakutoshi, bali kuna haja ya kueleza nini kifanyike. “Tunapaswa kutoka katika mfumo unaotuambia hali ya hewa inayotarajiwa kuwa vipi, kwenda kwenye mfumo unaotueleza hali hiyo inamaanisha nini, nini kifanyike, nani afanye, wapi na lini.”


Brigedia Jenerali Ndagala alisema kilimo na mifugo ni miongoni mwa sekta zilizo katika hatari kubwa kutokana na mafuriko, vipindi virefu vya ukavu, joto kali, upepo mkali, pamoja na wadudu na magonjwa yanayoathiriwa na hali hivyo, hatua za mapema zina umuhimu mkubwa katika kulinda uzalishaji, usalama wa chakula, maisha na mali, huku zikisaidia kupunguza gharama za kukabiliana na majanga baada ya kutokea.


Akizungumza katika hafla hiyo, Mkurugenzi wa Ofisi ya WMO Kanda ya Afrika, Dkt. Agnes Kijazi, alisema tukio hilo ni hatua muhimu katika safari ya Tanzania ya kuimarisha Utabiri Unaozingatia Hatua za kuchuka (Action-Based Forecasting – ABF).


Dkt. Kijazi alisisitiza, mchakato wa uandaaji shirikishi wa taarifa unalenga kuziba pengo kati ya taarifa za utabiri na hatua za mapema kwa kuimarisha ushirikiano kati ya huduma za hali ya hewa, huduma za kisekta, taasisi za menejimenti ya maafa, wadau wa maendeleo, wizara, vyombo vya habari na jamii zilizo katika hatari.


Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania, Dkt. Geofrid Chikojo (Mkurugenzi wa Udhibiti na Ubora-TMA), alisema WISER ActionFirst™ itasaidia kuongeza matumizi ya taarifa za hali ya hewa katika sekta za kilimo na mifugo.


Alisema TMA tayari inatoa Utabiri Unaozingatia Athari (Impact-Based Forecasting – IBF) kwa sekta mbalimbali, na mpango wa ActionFirst™ utasaidia kuendeleza msingi huo kwa kuhusisha watumiaji wa taarifa katika kuandaa taarifa zinazokidhi mahitaji yao.


“Ushirikishwaji wa wadau utasaidia kuboresha taarifa za tahadhari za mapema zinazolenga mahitaji ya sekta za kilimo na mifugo na kuongeza matumizi yake katika kufanya maamuzi”.Alisisitiza Dkt. Chikojo


Kwa upande wake, Mwakilishi wa WISER na UK Met Office, Bw. John Mungai, alifafanua kuwa ActionFirst™ inalenga kuhamisha mtazamo kutoka kwenye swali la “hali ya hewa itakuwaje?” kwenda kwenye maswali ya “hali hiyo ya hewa itafanya nini?” na “nini kinapaswa kufanyika?”


Programu hiyo inatekelezwa kwa ushirikiano wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) na Ofisi ya Waziri Mkuu – Idara ya Menejimenti ya Maafa, pamoja na Serikali ya Uingereza kupitia Ofisi ya Mambo ya Nje, Jumuiya ya Madola na Maendeleo (FCDO), Taasisi ya Hali ya Hewa ya Uingereza (UK Met Office) na Shirika la Hali ya Hewa Duniani (WMO).

Wednesday, September 16, 2026

DKT CHANG’A NA KATIBU MKUU WMO WAZUNGUMZIA HALI YA EL NINO YA 2026

 


Geneva: 15 Septemba, 2026

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), na Makamu wa Mwenyekiti wa Jopo la Kimataifa la Sayansi ya Mabadiliko ya Hali ya Hewa na Tabianchi (IPCC), Dkt. Ladislaus Chang’a alikutana na Katibu Mkuu wa Shirika la Hali ya Hewa Duniani (World Meteorological Organization - WMO) Prof. Celeste Saulo na kufanya mazungumzo kuhusu uboreshaji wa huduma za hali ya hewa, hali ya El Nino 2026 na umuhimu wa kuendelea kuimarisha utoaji wa taarifa za mapema na maandalizi ya kukabiliana na athari zake. 



Prof. Saulo alimpongeza Dkt. Chang’a na kufurahishwa na namna TMA wanavyoendelea kusimamia vyema utoaji wa huduma za hali ya hewa nchini Tanzania hususan katika kutoa elimu na kutahadharisha Umma na Wadau mbalimbali kuhusiana na hali ya El Nino na athari zake katika misimu ya mvua.  Aidha, Prof. Saulo ameahidi kuendelea kushirikiana na Tanzania katika kuboresha huduma za hali ya hewa kupitia programu mbalimbali za WMO ikiwa ni pamoja na eneo la matumizi ya akiliunde (AI) katika mnyororo mzima wa utoaji wa huduma za hali ya hewa. 


“Napongeza juhudi za Tanzania katika utoaji wa huduma za hali ya hewa na elimu hususan katika kipindi hiki tunachokabiliwa na Hali ya El Nino yenye nguvu. Tanzania imekuwa mfano wa kuigwa na nimetumia Tanzania kama mfano mzuri wa utoaji wa elimu kuhusu El Nino na maandalizi ya kukabiliana na hali hiyo katika hotuba yangu ya hivi karibuni kuhusiana na hali inavyoendelea” Alisema Prof. Celeste Saulo.


Katika Kikao hicho, Dkt.Chang’a alimshukuru Katibu Mkuu wa WMO kwa kuendelea kuiamini Tanzania na TMA na kuendelea kuisaidia TMA kupitia programu zake mbalimbali za uboreshaji wa huduma za hali ya hewa kikanda na kitaifa ambazo zinatekelezwa kwa ushirikiano na Wadau wa Maendeleo na Nchi Wanachama wa WMO ambapo utekelezaji wake unaendelea vizuri. 


“Naendelea kushukuru sana kwa usaidizi wa WMO kupitia programu zake mbalimbali ambazo zinachangia pakubwa katika kuboresha huduma na utoaji wa huduma za hali ya hewa nchini na nchi nyingine pia kuongeza nguvu katika uwekezaji mkubwa unaofanywa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika sekta ya hali ya hewa”.


Aidha, Dkt. Chang’a alimjulisha Katibu Mkuu wa WMO kuwa, kupitia programu za WMO, Tanzania imeweza kusaidia wataalamu wa hali ya hewa wa nchi nyingine kwa kutoa msaada wa kiufundi na miongoni mwa nchi hizo ni  Seychelles, Burundi, Sudan Kusini, na Namibia. Maeneo ambayo TMA imezisaidia nchi nyingine katika tasnia hii ya hali ya hewa ni pamoja na maeneo ya uboreshaji wa “Mfumo wa Usimamizi wa Ubora wa huduma na Umahiri wa Wataalamu (Quality Management System-QMS and Competency Assessment )”, “Utabiri wa Hali Mbaya ya Hewa (Severe Weather Forecasting)”, “Utabiri wa Hali ya Hewa kwa Kutumia Modeli za Kompyuta (Numerical Weather Prediction-NWP)”, “Mchakato wa kisheria katika sekta ya hali ya hewa (Legal Matters)” na Usambazaji wa Huduma za Hali ya Hewa kwa Umma (Public Weather Services-PWS). 

Vilevile Dkt. Chang’a alimshukuru Katibu Mkuu wa WMO kwa fursa ya kuleta mikutano mikubwa ya kitaalamu nchini ikiwa ni pamoja na mkutano wa nne (4) wa wataalamu wa matumizi ya huduma za hali ya hewa kwa sekta mbalimbali za kijamii na kiuchumi “The Fourth WMO Operational Climate Prediction (OCP-4)” uliofanyika Arusha mwishoni mwa mwezi Juni hadi mwanzo wa Julai 2026 kwa mara ya kwanza barani Afrika na kwa Tanzania na kwa ufanisi mkubwa. Tanzania , kupitia TMA itakuwa mwenyeji wa Mkutano wa nne wa wataalamu wabobezi wa sayansi ya mabadiliko ya hali ya hewa na tabianchi IPCC (IPCC WG1-LAM3) unaotarajiwa kufanyika Arusha mwanzoni mwa mwezi Novemba 2026.

Tuesday, August 18, 2026

MWELEKEO WA MVUA ZA MSIMU WA VULI (OKTOBA-DISEMBA),2026







 

TMA YATOA ANGALIZO DHIDI YA EL NINO, MSIMU WA VULI 2026


 Dar Es Salaam – 18 Agosti, 2026

Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imetoa rasmi utabiri wa msimu wa mvua za Vuli (Oktoba – Desemba) 2026, ikitoa angalizo la msimu huo kuathiriwa kwa kiwango kikubwa na hali ya El Niño yenye nguvu kubwa iliyotokana na joto la bahari kuwa Juu ya Wastani katika Bahari ya Pasifiki, hali itakayochagiza ongezeko la  Mvua za Vuli 2026 kuwa za Juu ya Wastani hadi Wastani katika maeneo mengi ya Ukanda wa Pwani ya Kaskazini, Nyanda za Juu Kaskazini Mashariki, Ukanda wa Ziwa Viktoria na kaskazini mwa Mkoa wa Kigoma.

 

Akizungumza juu ya utabiri huo, Mkurugenzi Mkuu wa TMA na Makamu Mwenyekiti wa Jopo la Kimataifa la Sayansi ya Mabadiliko ya Hali ya Hewa na Tabia Nchi (IPCC), Dkt. Ladislaus Chang'a alisema:-

"Msimu wa mvua za Vuli 2026 unatarajiwa kuathiriwa kwa kiwango kikubwa na hali ya El Niño yenye nguvu kubwa, hivyo mvua za Juu ya Wastani hadi Wastani zinatarajiwa katika maeneo mengi ya nchi Ukanda wa Pwani ya Kaskazini, Nyanda za Juu Kaskazini Mashariki, Ukanda wa Ziwa Viktoria na kaskazini mwa Mkoa wa Kigoma”. Aliongezea kusema kuwa Mvua hizo zinatarajiwa kuanza wiki ya nne ya mwezi Septemba hadi wiki ya kwanza ya mwezi Oktoba 2026 katika maeneo ya ukanda wa Ziwa Viktoria, na kusambaa taratibu katika maeneo mengine katika mwezi Oktoba 2026, aidha alifanunua kuwa kwa kawaida mvua za Vuli huisha mwezi Desemba japo katika msimu wa Vuli 2026 mvua za nje ya msimu zinatarajiwa kuendelea hadi mwezi Januari 2027, na ongezeko la mvua likitarajiwa hasa katika kipindi cha mwezi Novemba 2026.

 

Akielezea juu ya athari zinazotarajiwa, Dkt. Chang’a ametahadharisha kuwa "vipindi vya unyevu kwenye udongo wa kuzidi kiasi pamoja na mafuriko vinaweza kujitokeza na kuathiri ukuaji wa mazao na miundombinu ya kilimo," pia aliongezea kusema kuwa ongezeko la kina cha maji katika mabwawa na mito linaweza kuathiri miundombinu ya rasilimali za maji na nishati, huku magonjwa ya mlipuko yanaweza kujitokeza kutokana na uchafuzi wa maji. Magonjwa ya mazao yanayosababishwa na kuvu, bakteria na virusi yanaweza kuathiri uzalishaji wa viazi mviringo, alizeti, maharage, ufuta pamoja na matunda na mbogamboga, huku sekta za usafiri, ujenzi na utalii zikitarajiwa kukumbwa na changamoto za mmomonyoko wa barabara, uharibifu wa madaraja na kuhama kwa wanyamapori kutokana na mafuriko.

 

Katika hitimisho lake, Dkt. Chang’a amewashauri Wadau wa sekta mbalimbali za kiuchumi na kijamii kupanga na kutekeleza shughuli zao kwa kuzingatia taarifa mahususi za hali ya hewa zinazotolewa na TMA ikiwa ni pamoja na kuvuna maji ya mvua, kuimarisha miundombinu, kutoa tahadhari za mapema na kudhibiti mazalia ya mbu ili kupunguza magonjwa ya mlipuko.

 

Kwa taarifa zaidi tembelea: https://www.meteo.go.tz/uploads/documents/sw-1758375754-Mwelekeo%20wa%20Mvua%20za%20Vuli%202025.pdf

Monday, August 17, 2026

ATHARI ZA EL NIÑO KATIKA MVUA ZA VULI 2026: TMA YAWANOA WANAHABARI




Dar es Salaam, 17 Agosti 2026

Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imebainisha kuwa hali ya El Niño iliyoanza kujitokeza mwezi Aprili 2026 imeendelea kuimarika na inatarajiwa kuchagiza mwenendo wa mvua za msimu wa Vuli wan Oktoba hadi Disemba 2026 na kuleta vipindi vya hali mbaya ya hewa katika baadhi ya maeneo ya nchi.

 

Hayo yalisemwa na Mkurugenzi Mkuu wa TMA na Makamu Mwenyekiti wa Jopo la Kimataifa la Sayansi ya Mabadiliko ya Hali ya Hewa na Tabia Nchi (IPCC), Dkt. Ladislaus Chang'a, wakati wa warsha ya wanahabari iliyofanyika jijini Dar es Salaam. Warsha hiyo ni mwendelezo wa juhudi za TMA za kuhakikisha kuwa wanahabari wanapata uelewa wa utabiri wa hali ya hewa na tafsiri zake kabla haujatolewa rasmi ili kuifikia jamii kwa usahihi.

 

"Hali ya El Niño inatarajiwa kuendelea kuimarika na kufikia kiwango cha El Nino yenye nguvu kubwa kuelekea mwishoni mwa mawaka na hivyo kusababisha ongezeko la mvua katika ukanda wa Afrika Mashariki " alisema Dkt. Chang'a.

 

Dkt. Chang'a aliongeza kuwa, katika hatua za kuboresha Tuzo za Wanahabari Bora wa Habari za Hali ya Hewa kwa mwaka 2026, TMA na Taasisi ya Usimamizi wa Mazingira na Maendeleo ya Kiuchumi (EMEDO) wameungana ili  kuhakikisha kuwa tukio la utoaji wa tuzo hizo linakuwa kubwa na la kuvutia zaidi. Kwa sababu hiyo, aliwasisitiza wanahabari wote nchini kuwasilisha kazi zao za ushindani ili kuwania Tuzo hizo.

 

Aidha, kwa upande wao,  wanahabari, wameipongeza TMA kwa kuendelea kuboresha usahihi wa utabiri na  huduma za hali ya hewa kwa ujumla.

 

Utabiri rasmi wa Mvua za Vuli ulitolewa rasmi tarehe 18 Agosti 2026.

 

Kauli mbiu ya warsha hiyo ilikuwa: "Kupunguza Pengo la Uelewa wa Tahadhari za Hali ya Hewa kwa Pamoja."






Featured Post

DKT. KIJAZI: KIWANGO CHA USAHIHI WA UTABIRI WA MSIMU WA VULI 2019 KIWE CHA JUU ZAIDI.

Mkurugenzi mkuu wa TMA na Makamu wa Tatu wa Rais wa Shirika la Hali ya Hewa Duniani Dkt. Agnes Kijazi (katikati mwenye suti nyeusi) waka...