Dar es Salaam, 17 Disemba
2019:
Mamlaka
ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) inatoa taarifa ya mrejeo kuhusu uwepo wa vipindi
vya mvua kubwa katika maeneo mengi nchini. Mvua zinaendelea kusambaa katika
maeneo ya Pwani ya kaskazini pamoja na kanda kati.
Hivyo,
tahadhari ya kuendelea kwa vipindi vya mvua kubwa inatolewa katika baadhi ya
maeneo ya mikoa ya Pwani, Dar es salaam, Tanga, Morogoro, Dodoma, Singida
pamoja na visiwa vya Unguja na Pemba. Hali hiyo imetokana na kuimarika kwa
ukanda mvua na kusogea katika maeneo hayo kutokana na mwenendo wa mkondo baridi
katika eneo la kusini mwa Afrika. Hali hiyo ya vipindi vya mvua kubwa inatarajiwa kuendelea hadi alasiri ya leo tarehe 17 Disemba,
2019.
Aidha,
Angalizo lililotolewa la vipindi vya mvua kubwa zinazoendelea katika baadhi ya
maeneo ya Nyanda za juu kusini magharibi (Mikoa ya Rukwa, Songwe, Mbeya,
Iringa), Mikoa wa Ruvuma, Lindi, Mtwara pamoja na maeneo ya kusini mwa mkoa wa
Morogoro liendelee kuzingatiwa.
USHAURI: Wananchi
wanashauriwa kuendelea kufuatilia utabiri wa saa 24 pamoja na tahadhari kila
zinapotolewa na Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania na kuchukua hatua.
No comments:
Post a Comment