Wednesday, June 24, 2026

UNDP YAIKABIDHI TMA MAGARI MATANO KATIKA KUIMARISHA MIFUMO YA UANGALIZI WA HALI YA HEWA NA TAHADHARI ZA MAPEMA KUPITIA MRADI WA SOFF

 

Uploading: 522163 of 522163 bytes uploaded.









Dar es Salaam, 23 Juni 2026:


Shirika la Mpango wa Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP)  limekabidhi rasmi magari matano kwa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) kupitia Mradi wa Mfuko wa Umoja wa Mataifa wa kuimarisha Uangazi wa Hali ya Hewa (SOFF), hatua inayolenga kuimarisha uwezo wa Tanzania katika uendeshaji na matengenezo ya miundombinu muhimu ya uangalizi wa hali ya hewa nchini.

 

Makabidhiano hayo yalifanyika katika Ofisi za TMA, Ubungo Plaza , Dar es Salaam, tarehe 23 Juni 2026 yakiashiria hatua nyingine muhimu ya ushirikiano kati ya UNDP na TMA katika kuimarisha mifumo ya uangazi na kuboresha huduma za utabiri wa hali ya hewa pamoja na kuongeza ustahimilivu katika kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa nchini.

 

Magari hayo yatawezesha timu za kiufundi za TMA kufikia vituo vya uangazi wa hali ya hewa vilivyopo katika maeneo mbalimbali nchini kwa ajili ya ufungaji, matengenezo, ukaguzi na ufuatiliaji wa vifaa vya hali ya hewa. Hatua hii itasaidia kuhakikisha kunakuwa na ukusanyaji na usambazaji wa taarifa za hali ya hewa kwa kuzingatia viwango vya kimataifa.

 

Akizungumza katika hafla hiyo, Mwakilishi Mkazi wa UNDP Tanzania, Shigeki Komatsubara alisema kuwa uwekezaji huo unaenda mbali zaidi ya kukabidhi magari.

Kwa mtazamo wa kwanza, makabidhiano ya leo yanaweza kuonekana kama kukabidhi magari. Hata hivyo, kwa hakika ni uwekezaji unaowezesha ukusanyaji wa taarifa bora za hali ya hewa ambazo ni msingi wa utabiri sahihi wa hali ya hewa, mifumo ya tahadhari za mapema na kupunguza madhara ya majanga,” alisema.

 

Makabidhiano hayo ni sehemu ya utekelezaji wa Mradi wa SOFF, ambao ni miongoni mwa uwekezaji mkubwa zaidi unaoendelea nchini Tanzania katika sekta ya miundombinu ya hali ya hewa. Mradi huo una thamani ya takribani Dola za Marekani milioni 13.5, ikijumuisha Dola milioni 9 kutoka Mfuko wa SOFF Multi-Partner Trust Fund na Dola milioni 4.5 kama mchango wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

 

Kupitia uwekezaji katika vituo vya uangazi wa hali ya hewa ardhini na angani, mafunzo ya kitaalamu, mradi huo unalenga kuimarisha mchango wa Tanzania katika Mtandao wa Kimataifa wa Uangazi wa Hali ya Hewa (‘Global Basic Observing Network’ - GBON) na kuongeza uwezo wa nchi katika kutoa utabiri sahihi wa hali ya hewa pamoja na huduma madhubuti za tahadhari za mapema.

 

Mkurugenzi Mkuu wa TMA, Dkt. Ladislaus B. Chang’a, amepongeza ushirikiano unaoendelea kati ya TMA na UNDP pamoja na msaada unaotolewa kupitia Mradi wa SOFF, akisisitiza umuhimu wa kuimarisha uwezo wa kiutendaji wa taasisi katika kusimamia mtandao wa kisasa wa uangazi wa hali ya hewa nchini.

 

Wakati ambapo matukio ya hali mbaya ya hewa na athari za mabadiliko ya hali ya hewa yanaongezeka kwa kasi, umuhimu wa mifumo imara ya uangazi wa hali ya hewa na huduma za tahadhari za mapema hauwezi kupuuzwa.

 

Kuhusu UNDP

Shirika la Mpango wa Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) linafanya kazi katika takribani nchi na maeneo 170 duniani, likisaidia kuondoa umaskini, kupunguza ukosefu wa usawa na kujenga ustahimilivu ili nchi ziweze kufikia maendeleo endelevu. Nchini Tanzania, UNDP inashirikiana na Serikali pamoja na wadau mbalimbali katika maeneo ya utawala bora, ukuaji shirikishi wa uchumi, mabadiliko ya tabianchi, mazingira na maendeleo endelevu.

 

Kuhusu TMA

Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) ni taasis ya Serikali iliyoanzishwa kwa sheria ya Mamlaka ya Hali ya Hewa Na.2 ya mwaka 2019 ikiwa na jukumu la kuratibu, kudhibiti na kutoa huduma za hali ya hewa katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Saturday, June 13, 2026

WATAALAMU KUTOKA UGANDA NA KENYA WATEMBELEA TMA KUJIFUNZA KUHUSU MIFUMO YA UTOAJI WA TAHADHARI ZA HALI MBAYA YA HEWA NA URATIBU WA MAAFA















Dodoma, Tanzania, 9 Juni 2026.

Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imepokea wataalamu wa hali ya hewa na uratibu wa maafa kutoka Uganda na Kenya, na pia kutoka Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Kupunguza Hatari za Maafa (UNDRR) kwa lengo la kujifunza na kubadilishana uzoefu kuhusu  mifumo ya tahadhari za mapema.


 Ziara hiyo ililenga kupata uzoefu kutoka Tanzania, ambayo ni miongoni mwa nchi kinara katika utekelezaji wa mifumo ya tahadhari za mapema ili kusaidia juhudi za kuanzisha na kuimarisha mifumo kama hiyo nchini Kenya na Uganda.


Aidha ziara hiyo iliongozwa na Dr. Agnes Kijazi, Mkurugenzi wa Shirika la Hali ya Hewa Duniani Kanda ya Afrika pamoja na Dkt. Martin Brown Munene, Mtaalamu wa Tahadhari za Mapema kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa ya Kupunguza Hatari za Maafa (UNDRR).

Akizungumza wakati wa ziara hiyo, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania na Makamu Mwenyekiti wa Jopo la Kimataifa la Sayansi ya Mabadiliko ya Hali ya Hewa na Tabianchi (IPCC), Dkt. Ladislaus Chang'a, alisisitiza umuhimu wa ushirikiano katika kujenga jamii zitakazoweza kukabiliana na hatari zinazohusiana na matukio ya hali mbaya ya hewa.

"Mifumo ya tahadhari za mapema ni muhimu sana  kwa ajili ya kulinda maisha na mali kutokana na changamoto za mabadiliko ya hali ya hewa, hususan matukio ya hali mbaya ya hewa, yanayoendelea kuongezeka kwa idadi na ukubwa wake.   Kupitia ziara hii wenzetu watajifunza na kupata uzoefu wa namna bora ya kujenga, kutumia na kuratibu mifumo ya tahadhari. Lengo kubwa ni kuimarisha ushirikiano ili kuhakikisha hakuna anayeachwa nyuma katika kanda yetu na Afrika kwa ujumla," alisema Dkt. Chang'a


Dkt. Agnes Kijazi, Mkurugenzi wa Shirika la Hali ya Hewa Duniani Kanda ya Afrika alipongeza juhudi zinazofanywa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika kuimarisha mifumo ya tahadhari za mapema na uratibu wa maafa. Nawapongeza sana Tanzania kwa ushirikiano mzuri na hatua kubwa ya kuimarisha huduma za hali ya hewa na uratibu wa maafa.


"Ziara ya kubadilishana uzoefu inatoa fursa muhimu kwa nchi za Afrika kujifunza kutokana na uzoefu wa kila mmoja katika kuimarisha mifumo ya tahadhari ya mapema na usimamizi wa hatari za majanga ya hali ya hewa. Nawapongeza kwa uratibu madhubuti katika kuhakikisha tahadhari za mapema zinafika kwa jamii zilizo hatarini na kuchukua hatua za haraka," alisema Dkt. Kijazi.


Akiwakilisha Shirika la Umoja wa Mataifa la Kupunguza Hatari za Maafa (UNDRR), Dkt. Martin Brown Munene,  alishukuru kwa kupata fursa ya kuja kujifunza Tanzania na alisisitiza umuhimu wa kuendelea kuimarisha ushirikiano kwa nchi zote za Afrika Mashariki.

Thursday, June 11, 2026

TMA HOSTS DANISH METEOROLOGICAL INSTITUTE MISSION TO STRENGTHEN TECHNICAL CAPACITY FOR SUSTAINABLE GBON COMPLIANCE













Dodoma, 8 June 2026

The Tanzania Meteorological Authority (TMA)  welcomed a technical mission from the Danish Meteorological Institute (DMI) under the Systematic Observations Financing Facility (SOFF) Project aimed at strengthening Tanzania's technical and institutional capacity to sustain compliance with the Global Basic Observing Network (GBON).


Opening the mission in Dodoma, TMA Director General and Vice Chair of the Intergovernmental Panel on Climate Change (IPCC), Dr. Ladislaus Chang'a, said the visit marks an important step in enhancing TMA's operational effectiveness and ensuring long-term sustainability of investments made through the SOFF Project.

"Building human resource capacity is equally important as investing in infrastructure. Our goal is to ensure that TMA maintains GBON compliance over the long term while improving the quality and reliability of meteorological services delivered to the nation and the global community," said Dr. Chang'a.


The week-long mission will assess TMA's technical capabilities in key areas including meteorological data exchange, calibration facilities, equipment maintenance, instrument fabrication, and the operation of surface and upper-air observation networks.


Dr. Chang'a commended the continued partnership between TMA, Danish Meteorological Institute (DMI) and the United Nations Development Programme (UNDP), noting that the collaboration is already contributing to the enhancement of TMA services and its role at the regional and International levels. “I trust that the strong partnership that has been built between TMA, DMI and UNDP will continue to strengthen  and deliver highly desirable and long lasting results  and Impacts in the advancement of meteorological services in the Tanzania and across Africa. “ Said Dr Chang’a


Dr. Sebastian Hornum, Project Manager at DMI, emphasized the importance of the mission and its expected outcome. "This mission provides an opportunity to work closely with TMA experts to identify practical solutions that will enhance technical capacity and support sustainable compliance with international observing standards."


Meanwhile, Dr. Abbas Kitogo, Co-Chair of the SOFF Project Technical Coordination Committee and UNDP Representative, reaffirmed UNDP's commitment to supporting the successful implementation of the project.

"The progress achieved so far reflects the admirable cooperation between TMA, DMI and UNDP. UNDP remains fully committed to supporting the successful implementation of the SOFF Project in Tanzania”

."

The mission will include visits to designated GBON observation stations in Dodoma and Dar es Salaam to assess operational capacities and identify areas for further improvement.

TMA YAPOKEA UJUMBE WA KITAALAMU KUTOKA TAASISI YA HALI YA HEWA YA DENMARK KWA AJILI YA KUIMARISHA MTANDAO WA VITUO VYA HALI YA HEWA VIWANGO VYA GBON












Dodoma, 8 Juni 2026

Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imepokea ujumbe wa wataalamu kutoka Taasisi ya Hali ya Hewa ya Denmark (DMI) chini ya Mradi wa Mfuko wa Umoja wa Mataifa wa kuimarisha Uangazi wa Hali ya Hewa (SOFF), wenye lengo la kuimarisha Mtandao wa Vituo vya Hali ya Hewa nchini ili kufikia viwango vya Mtandao wa Kimataifa wa Uangazi wa Hali ya Hewa (GBON). Mtandao huu ulioanzishwa na Shirika la Hali ya hHewa Duniani (WMO) ukiwa na malengo ya kuimarisha ukusanyaji wa data za hali ya hewa duniani, Kuhakikisha data za uangazi zinapatikana kwa wakati na kwa ubora unaotakiwa, Kuboresha utabiri wa hali ya hewa na tahadhari za mapema, Kusaidia nchi hasa zinazoendelea, kutimiza mahitaji ya uangazi wa hali ya hewa yanayowekwa na WMO.


Akizungumza wakati wa ufunguzi wa ziara hiyo jijini Dodoma, Mkurugenzi Mkuu wa TMA na Makamu mwenyekiti  wa Jopo la Kimataifa la Mabadiliko ya Hali ya Hewa na Tabianchi (IPCC), Dkt. Ladislaus Chang'a, alisema kuwa ujumbe huo wa kitaalamu unaonesha dhamira ya pamoja ya kuendelea kuimarisha uwezo wa TMA katika uangazi wa hali ya hewa na kuhakikisha uwekezaji unaofanywa kupitia mradi wa SOFF unaleta matokeo  chanya na endelevu yanayoiwezesha Tanzania kuendelea kutimiza viwango vya GBON.


"Lengo letu ni kuhakikisha TMA inaendelea kutimiza viwango vya GBON kwa muda mrefu huku ikiboresha ubora na usahihi wa huduma za hali ya hewa zinazotolewa kwa jamii taifa, kiatika kanda na kimataifa," alisema Dkt. Chang'a.


Ziara hiyo ya kitaalamu ita tathmini uwezo wa TMA katika maeneo mbalimbali ikiwemo mfumo wa ubadilishanaji wa taaarifa za hali ya hewa kimataifa, matengenezo na ukarabati wa vifaa, mchakato wa kujenga uwezo kwa wataalamu wa TMA, huduma za uhakiki wa vifaa pamoja na uendeshaji wa vituo vya uangazi wa hali ya hewa vya ardhini na anga la juu.


Nae Meneja wa Mradi kutoka DMI, Dkt. Sebastian Hornum,  alisema, "Ziara hii inatoa fursa muhimu ya kufanya kazi kwa karibu na wataalamu wa TMA ili kubaini mbinu mbalimbali zitakazosaidia kuimarisha uwezo wa kiufundi na kufikia viwango vya kimataifa vya uangazi wa hali ya hewa.”


Kwa upande wake, Mwenyekiti Mwenza wa Kamati ya Uratibu wa Mradi wa SOFF (PTCC) kutoka UNDP, Dkt. Abbas Kitogo, alisema:

“Mafanikio yaliyopatikana hadi sasa yanaakisi ushirikiano mzuri uliopo kati ya TMA, DMI na UNDP. Tutaendelea kutoa ushirikiano unaohitajika kuhakikisha Mradi wa SOFF unatekelezwa kikamilifu kwa faida endelevu za kiuchumi na kijamii nchini.”


Ziara hiyo itahusisha kutembelea vituo vya uangazi wa hali ya hewa vilivyopo Dodoma na Dar es Salaam ambavyo vimejumuishwa katika mtandao wa GBON ili kutathmini hali ya uendeshaji na kubaini maeneo yanayohitaji kuimarishwa zaidi.

Tuesday, June 2, 2026

NAIBU WAZIRI AHIMIZA USHIRIKIANO KUSAMBAZA TAARIFA ZA HALI YA HEWA KWA WANANCHI WA VIJIJINI

Dodoma, Juni 1, 2026.





Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mhe. Reuben Nhamanilo Kwagilwa, ameitaka Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) kuendelea kuimarisha ushirikiano na wadau mbalimbali ili kuhakikisha taarifa za hali ya hewa zinawafikia wananchi wote, hususan wanaoishi katika maeneo ya vijijini na maeneo ya mbali yanayokabiliwa na changamoto za upatikanaji wa huduma za mawasiliano.


Mhe. Kwagilwa ameyasema hayo alipotembelea banda la TMA wakati wa Ufunguzi wa Maonesho ya Siku ya Mazingira Duniani 2026 yanayofanyika kuanzia tarehe 1 hadi 5 Juni 2026 katika Viwanja vya Jakaya Kikwete Convention Centre (JKCC), jijini Dodoma, chini ya kauli mbiu isemayo "Dira 2050: Tuwajibike Kukijanisha Tanzania"


Akizungumza na wataalamu wa TMA, Mhe. Kwagilwa ameipongeza mamlaka hiyo kwa kazi kubwa inayoendelea kufanya katika utoaji wa huduma za hali ya hewa na kusisitiza umuhimu wa kuhakikisha taarifa hizo zinawafikia wananchi wanaozitegemea katika shughuli zao za kila siku, hususan sekta ya kilimo.

“Nawapongeza kwa kazi nzuri mnayoifanya na tunaona matokeo yake. Hata hivyo, kuna umuhimu wa kuhakikisha taarifa hizi zinawafikia wananchi waliopo kwenye maeneo ya mbali ambao wanategemea utabiri wa hali ya hewa katika shughuli zao za kimsimu, hasa kilimo,” amesema Mhe. Kwagilwa.


Aidha, amesisitiza umuhimu wa kuimarisha ushirikiano kati ya TMA na Vituo vya Kijamii vya Uhimilivu dhidi ya Mabadiliko ya Tabianchi (CCCRC) ili vituo hivyo viwe daraja muhimu la kufikisha taarifa za hali ya hewa kwa wananchi ngazi ya jamii na kuwawezesha kupata taarifa sahihi zinazohusu maeneo yao pamoja na mwongozo wa hatua stahiki za kuchukua katika misimu mbalimbali.


Ushiriki wa TMA katika maonesho hayo ni sehemu ya juhudi za Mamlaka kuendelea kusogeza huduma za hali ya hewa kwa wananchi, kuongeza uelewa wa matumizi ya taarifa za hali ya hewa katika sekta mbalimbali za maendeleo na kuimarisha ushirikiano na wadau

TMA inawakaribisha wananchi, wadau wa mazingira, watafiti, wanafunzi na washiriki wote wa maonesho hayo kutembelea banda la TMA ili kujifunza zaidi kuhusu huduma za hali ya hewa na mifumo ya utoaji wa utabiri wa hali ya hewa.

Featured Post

DKT. KIJAZI: KIWANGO CHA USAHIHI WA UTABIRI WA MSIMU WA VULI 2019 KIWE CHA JUU ZAIDI.

Mkurugenzi mkuu wa TMA na Makamu wa Tatu wa Rais wa Shirika la Hali ya Hewa Duniani Dkt. Agnes Kijazi (katikati mwenye suti nyeusi) waka...