|
Mkurugenzi mkuu wa TMA na Makamu wa Tatu wa Rais wa Shirika la
Hali ya Hewa Duniani Dkt. Agnes Kijazi (katikati mwenye suti nyeusi) akiongea wakati akifungua warsha ya wadau kujadili utabiri wa msimu wa mvua za vuli (Oktoba - Disemba 2019) unaotarajiwa kutolewa rasmi tarehe 03 Septemba 2019 katika ukumbi wa mikutano wa TMA, Ghorofa ya tatu, Ubungo Plaza, Dar es Salaam, Tanzania. |
|
Rais wa TMS Dkt. Burhani Nyenzi (kushoto) akizungumza kabla ya ufunguzi wa warsha
ya wadau kujadili utabiri wa msimu wa mvua za vuli (Oktoba -
Disemba 2019) unaotarajiwa kutolewa rasmi tarehe 03 Septemba 2019 katika ukumbi wa mikutano wa TMA, Ghorofa ya tatu, Ubungo Plaza, Dar es Salaam, Tanzania. |
|
Kaimu Mkurugenzi wa Huduma Saidizi Bi. Mariam Is-haaq akimkaribisha Mgeni rasmi kwa ajili ya ufunguzi wa warsha
ya wadau kujadili utabiri wa msimu wa mvua za vuli (Oktoba -
Desemba 2019) unaotarajiwa kutolewa rasmi tarehe 03 Septemba 2019 katika ukumbi wa mikutano wa TMA, Ghorofa ya tatu, Ubungo Plaza - Dar es Salaam, Tanzania. |
|
Bw. Wilberforce Kikwasi akichangia mada kwenye warsha
ya wadau kujadili utabiri wa msimu wa mvua za vuli (Oktoba -
Desemba 2019) unaotarajiwa kutolewa rasmi tarehe 03 Septemba 2019 katika ukumbi wa mikutano wa TMA, Ghorofa ya tatu, Ubungo Plaza - Dar es Salaam, Tanzania. |
|
Bw. Aloyce Swenya akiwasilisha mada kwenye warsha
ya wadau kujadili utabiri wa msimu wa mvua za vuli (Oktoba -
Desemba 2019) unaotarajiwa kutolewa rasmi tarehe 03 Septemba 2019 katika ukumbi wa mikutano wa TMA, Ghorofa ya tatu, Ubungo Plaza - Dar es Salaam, Tanzania. |
|
Bi. Sabiha Mukubwa akiwasilisha mada kwenye warsha
ya wadau kujadili utabiri wa msimu wa mvua za vuli (Oktoba -
Desemba 2019) unaotarajiwa kutolewa rasmi tarehe 03 Septemba 2019 katika ukumbi wa mikutano wa TMA, Ghorofa ya tatu, Ubungo Plaza - Dar es Salaam, Tanzania. |
|
Wadau mbalimbali wakichangia mada katika warsha
ya wadau kujadili utabiri wa msimu wa mvua za vuli (Oktoba -
Desemba 2019) unaotarajiwa kutolewa rasmi tarehe 03 Septemba 2019 katika ukumbi wa mikutano wa TMA, Ghorofa ya tatu, Ubungo Plaza - Dar es Salaam, Tanzania. |
|
Wadau kutoka sekta mbalimbali wakiwa katika picha ya pamoja na mgeni rasmi kwenye warsha
ya wadau kujadili utabiri wa msimu wa mvua za vuli (Oktoba -
Desemba 2019) unaotarajiwa kutolewa rasmi tarehe 03 Septemba 2019 katika ukumbi wa mikutano wa TMA, Ghorofa ya tatu, Ubungo Plaza - Dar es Salaam, Tanzania. |
Tarehe 29/08/2019: Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania
(TMA) kupitia programu ya Huduma za Hali ya Hewa ya kidunia (Global Framework
for Climate Services (GFCS)) iliyo chini ya Shirika la Hali ya Hewa Duniani
(WMO), imekutana na wadau wa sekta mbalimbali ili kujadili na kupata maoni yao
jinsi watakavyoutumia utabiri wa msimu wa mvua za vuli (Oktoba hadi Disemba,
2019) unaotarajiwa kutolewa rasmi tarehe 03 Septemba 2019.
Akiongea
wakati wa ufunguzi wa warsha hiyo, mgeni rasmi ambaye ni Mkurugenzi Mkuu wa TMA
na Makamu wa Tatu wa Rais wa WMO, Dkt. Agnes Kijazi aliwakumbusha washiriki
kutambua mabadiliko ya hali ya hewa ni changamoto kubwa katika sekta mbalimbali
hivi sasa, hivyo aliwataka washiriki kufanya juhudi za pamoja ili kuhakikisha
taarifa za hali ya hewa zinatumika ipasavyo na kuleta maendeleo endelevu hasa
kuchochea uchumi wa viwanda katika Taifa letu kwa kuzalisha malighafi
zitakazohitajika viwandani.
“Ni matumaini
yangu baada ya kikao hiki TMA kwa kushirikiana na ninyi wadau kutoka katika
sekta mbalimbali tutahakikisha watanzania wanapata taarifa za hali ya hewa kwa
wakati na wanazitumia ipasavyo katika sekta mbali mbali ili kuleta maendeleo
endelevu hasa kuchochea uchumi wa viwanda katika Taifa letu kwa kuzalisha
malighafi zitakazohitajika viwandani ikiwemo mali ghafi kutoka sekta ya kilimo”,
alifafanua Dkt. Kijazi
Aidha
Dkt.Kijazi alisisitiza wadau kupanga
mipango ya sekta zao kulingana na utabiri wa hali ya hewa utakaotolewa hapo
baadae wenye kujumuisha maoni yao, ikiwa ni moja ya utekelezaji wa maelekezo
kutoka Shirika la hali ya hewa Duniani la kutaka taasisi za hali ya hewa kuwahusisha
zaidi wadau ambao ndiyo watumiaji wa taarifa za hali ya hewa.
Washiriki
wa mkutano huo ulijumuisha sekta ya afya, nishati, maafa, wanahabari, kilimo, uchukuzi,
uvuvi, mifugo, NGO, na wataalamu wa lugha (BAKITA).
No comments:
Post a Comment