Mkurugenzi mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa
Tanzania(TMA) na Makamu wa tatu wa Rais wa Shirika la Hali ya Hewa Duniani
(WMO) Dkt. Agnes Kijazi, mbele ya waandishi wa habari akichambua mwenendo
wa mifumo ya hali ya hewa na mwelekeo wa mvua za Msimu wa Vuli Oktoba - Desemba
2019 |
Bi. Veronica
Mgalula akitoa tathmini ya mvua za msimu wa Masika 2019, kabla ya kutolewa
rasmi mwelekeo wa msimu wa mvua za vuli kwa kipindi cha mwezi Oktoba hadi
Desemba 2019.
|
Washiriki mbalimbali wakiwa kwenye mkutano wa
wanahabari wa kutoa mwelekeo wa mvua za Msimu wa Vuli Oktoba - Desemba 2019. |
Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imetoa rasmi utabiri wa msimu kuanzia mwezi Oktoba 2019 hadi Desemba, 2019 katika mkutano wa waandishi wa habari uliofanyika katika Ofisi za TMA.
Taarifa inatoa uchambuzi wa mwenendo wa mifumo ya hali ya hewa na mwelekeo wa msimu wa mvua katika kipindi cha mwezi Oktoba hadi Desemba, 2019. Pia ushauri na tahadhari kwa wadau wa sekta mbali mbali wanaohitaji taarifa za hali ya hewa katika utekelezaji wa majukumu yao kama vile Kilimo na Usalama wa Chakula, Mifugo na Wanyamapori, Maliasili na Utalii, Uchukuzi na Mawasiliano, Nishati na Maji, Mamlaka za Miji, Afya pamoja na Menejimenti za Maafa. Muhtasari wa mwelekeo wa mvua hizo na athari zake ni kama ifuatavyo: Kusoma zaidi ingia humu http://meteo.go.tz/news/226
No comments:
Post a Comment