Tarehe
16/09/2019:‘Mkutano huu ni fursa kwa huduma za hali ya
hewa nchini kwa vile utajadili masuala mbalimbali yenye lengo la uboreshaji,
hivyo Tanzania itatumia fursa hiyo kuongeza ufanisi’, Mkurugenzi Mkuu wa TMA
Dkt. Kijazi, alizungumza hayo wakati wa mkutano wa mawaziri
wa SADC wa sekta ya tehama, habari, uchukuzi na hali ya hewa, ulioanza
nchini, katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Mwl. Julius Nyerere, Dar es
Salaam.
Aliongezea kwa kusema kuwa
Tanzania kupitia Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imekuwa ikifanya vizuri
katika ukanda wa nchi za SADC ikiwa ni pamoja na kusaidia nchi zingine
wanachama wa SADC katika kuboresha huduma za hali ya hewa kama vile kuanzisha
mifumo ya kiutendaji bado TMA inajikita katika kuongeza fursa za ajira na
kuweka mazingira wezeshi katika ukuaji wa uchumi wa nchi na jumuiya kupitia
huduma za hali ya hewa.
Aidha katika kuhakikisha TMA
inashiriki kikamilifu mkutano huo, TMA imeweka banda maalumu kwaajili ya kuelimisha
huduma inazozitoa na mifumo iliyopo sambamba na utabiri mahsusi kwa washiriki
wa mkutano.
Mkutano huo umeanza rasmi
leo tarehe 16 mpaka 20 Septemba 2019 ukijumuisha mawaziri na wataalamu
mbalimbali wa sekta husika kutoka nchi za SADC. Kauli mbiu ya mkutano huo ni
‘Mazingira Wezeshi kwa Ukuaji wa Uchumi Jumuishi na Endelevu, Kukuza Biashara
katik Jumuiya na Kuongeza Fursa ya Ajira’
HONGERENI SANA TMA KWA KAZI NZURI. MUNGU IBARIKI TMA, MUNGU IBARIKI TANZANIA.
ReplyDelete