Matukio
mbalimbali kwa picha katika kikao cha TUGHE kilichofanyika tarehe 07Septemba
2019 katika ukumbi wa TMA, Ubungo Plaza - Dar es salaam
|
” Natambua umuhimu wa michezo kwa wafanyakazi kwani inaleta
umoja kazini (team work) pamoja na kuleta afya, hivyo kuifanya Mamlaka kuwa juu”
aliyasema hayo Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) na
Makamu wa Tatu wa Rais wa Shirika la Hali ya Hewa Duniani (WMO) Dkt. Agnes
Kijazi wakati akitoa nasaha zake katika kikao cha TUGHE kilichofanyikia tarehe
07 Septemba 2019 katika ukumbi wa TMA, Ubungo plaza - Dar es salaam.
Katika kikao hicho Dkt. Kijazi alipokea zawadi
mbalimbali toka kwa wanachama wa TUGHE kwa kushika nafasi ya umakamu wa tatu wa
Rais wa WMO kwa kipindi cha miaka minne kuanzia 2019 hadi 2022.
Aidha, Katibu wa TUGHE Kinondoni, Ndg. Litson Magawa
alimpongeza Dkt. Kijazi kwa kufanikisha TMA kuwa Mamlaka Kamili pamoja na
kushika nafasi ya umakamu wa tatu wa Rais wa WMO.
Naye Kaimu Katibu wa Uchukuzi Sports Club, Ndg. Joseph
Peter aliipongeza menejimenti ya TMA kwa kuwawezesha wachezaji wake kufika
kwenye mashindano kwa wakati na hatimaye kufanikisha kuchukua vikombe vya
ushindi mara kadhaa.
Awali, Kaimu Mwenyekiti wa TUGHE mkoa wa Dar es salaam,
Dkt. Peter Kibacha aliwasilisha mada iliyolenga kuokoa na kupunguza vifo kwa
wamama wajawazito ambaye baadae aliwakumbusha viongozi kufuatilia utekelezaji
wa mkataba wa hali bora kwa wafanyakazi.
Aidha washiriki wengine katika kikao hicho ni pamoja na
viongozi wa menejimenti ya TMA, viongozi wa Tughe ndani ya Mamlaka pamoja na
wanachama wengine wa Tughe.
Mbona huku mwishoni naona bado neno Agency bado lonaonekana?
ReplyDeletetaarifa njema
ReplyDelete