Sunday, September 22, 2019

MATUKIO MBALIMBALI KATIKA PICHA WAKATI TMA IKIJUMUIKA NA WADAU WENGINE TOKA SEKTA YA UTALII KATIKA MAONESHO YA UTALII, KARIBU KUSINI YANAYOFANYIKA KIHESA, KILOLO-IRINGA.


Mkuu wa wilaya ya Kilolo, Iringa Mhe. Asia J. Abdallah akipata elimu kutoka kwa mtaalamu wa hali ya hewa ya namna taarifa za hali ya hewa zinavyoweza kusaidia kukuza sekta ya utalii hapa nchini kupitia maonesho ya utalii ya karibu kusini yanayoendelea  katika viwanja vya Kihesa, Kilolo, Iringa, Tarehe 20 mpaka 22 Septemba 2019.

Mkuu wa wilaya ya Sumbawanga Mhe. Dkt. Halfan Haule akisaini kwenye kitabu cha wageni kabla ya kupatiwa elimu ya hali ya hewa toka kwa mtaalamu wa hali ya hewa ya namna taarifa za hali ya hewa zinavyoweza kusaidia kukuza sekta ya utalii hapa nchini kupitia maonesho ya utalii ya karibu kusini yanayoendelea  katika viwanja vya Kihesa, Kilolo, Iringa, Tarehe 20 mpaka 22 Septemba 2019.

Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mjini, Mhe. Richard Atufigwege Kasesela  akisaini kwenye kitabu cha wageni kabla ya kupatiwa elimu ya hali ya hewa toka kwa mtaalamu wa hali ya hewa ya namna taarifa za hali ya hewa zinavyoweza kusaidia kukuza sekta ya utalii hapa nchini kupitia maonesho ya utalii ya karibu kusini yanayoendelea  katika viwanja vya Kihesa, Kilolo, Iringa, Tarehe 20 mpaka 22 Septemba 2019.


Meneja wa Tanzania Civil Aviation Authority (TCAA) kituo cha Iringa, Bi. Rosalia Makwaya akisaini kwenye kitabu cha wageni kabla ya kupatiwa elimu ya hali ya hewa toka kwa mtaalam wa hali ya hewa ya namna taarifa za hali ya hewa zinavyoweza kusaidia kukuza sekta ya utalii hapa nchini kupitia maonesho ya utalii ya karibu kusini yanayoendelea  katika viwanja vya Kihesa, Kilolo, Iringa, Tarehe 20 mpaka 22 Septemba 2019.
 

Wawekezaji toka katika sekta ya utalii wakiendelea kutembelea banda la TMA na kupewa elimu kutoka kwa mtaalamu wa hali ya hewa ya namna taarifa za hali ya hewa zinavyoweza kusaidia kukuza sekta ya utalii hapa nchini kupitia maonesho ya utalii ya karibu kusini yanayoendelea katika viwanja vya Kihesa, Kilolo, Iringa, Tarehe 20 mpaka 22 Septemba 2019.




Wataalamu wa hali ya hewa kutoka TMA wakiendelea kutoa elimu ya namna taarifa za hali ya hewa zinavyoweza kusaidia katika kukuza sekta ya utalii hapa nchini kupitia maonesho ya utalii ya karibu kusini yanayoendelea katika viwanja vya Kihesa, Kilolo, Iringa, Tarehe 20 mpaka 22 Septemba 2019.

Miss Utalii - Ruaha, Bi. Linda Samson pamoja na Miss Utalii - Kanda ya Kusini, Bi. Sara Michael Nkuki wakipata elimu kutoka kwa Meneja wa Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Bw. Issa Hamad, juu ya namna taarifa za hali ya hewa zinavyoweza kusaidia kukuza sekta ya utalii hapa nchini kupitia maonesho ya utalii ya karibu kusini yaliyofanyika  katika viwanja vya Kihesa, Kilolo, Iringa, Tarehe 20 mpaka 22 Septemba 2019.



Bi.  Itiweni S. Luhwago (Mhadhili wa Chuo Kikuu cha Iringa) akijibu swali aliloulizwa na mtaalamu wa hali ya hewa kabla ya kupokea  zawadi toka kwa Meneja wa Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Bw. Issa Hamad katika maonesho ya utalii ya karibu kusini yanayoendelea  katika viwanja vya Kihesa, Kilolo, Iringa, Tarehe 20 mpaka 22 Septemba 2019.

 Miss Utalii - Ruaha, Bi. Linda Samson(mwenye mfuko wa rangi ya bluu) pamoja na Miss Utalii - Kanda ya Kusini, Bi. Sara Michael Nkuki  (mwenye mfuko wa rangi nyeupe) kwenye picha ya pamoja na washiriki baada ya kupokea zawadi walipotembelea banda la TMA katika maonesho ya utalii ya karibu kusini yaliyofanyika katika viwanja vya Kihesa, Kilolo, Iringa, Tarehe 20 mpaka 22 Septemba 2019

Wageni wakipokea zawadi mbalimbali mara walipotembelea banda la TMA katika maonesho ya utalii ya karibu kusini yanayoendelea  katika viwanja vya Kihesa, Kilolo, Iringa, Tarehe 20 mpaka 22 Septemba 2019.


Meneja wa Kanda Nyanda za Juu Kusini Bw. Issa Hamad akiendelea kutoa elimu ya hali ya hewa kupitia vyombo vya habari kwenye maonesho ya utalii ya karibu kusini yanayoendelea katika viwanja vya Kihesa, Kilolo, Iringa, Tarehe 20 mpaka 22 Septemba 2019.

No comments:

Post a Comment

Featured Post

DKT. KIJAZI: KIWANGO CHA USAHIHI WA UTABIRI WA MSIMU WA VULI 2019 KIWE CHA JUU ZAIDI.

Mkurugenzi mkuu wa TMA na Makamu wa Tatu wa Rais wa Shirika la Hali ya Hewa Duniani Dkt. Agnes Kijazi (katikati mwenye suti nyeusi) waka...