Tarehe 29/08/2019 Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) kwa kushirikiana na Chama cha Wataalam wa Hali ya Hewa Tanzania (TMS) kupitia programu ya “Weather and Climate Information Services” (WISER), imejipanga katika kuongeza nguvu ya utoaji hudumza za hali ya hewa ili kufikia wananchi wengi zaidi.
Hayo
yalizungumzwa na mkurugenzi mkuu wa TMA na Makamu wa Tatu wa Rais wa Shirika la
Hali ya Hewa Duniani Dkt. Agnes Kijazi wakati akifungua rasmi uzinduzi
wa programu ya Huduma za Hali ya Hewa kwa Afrika (Weather Information and
Services for Africa (WISER) Kitaifa “WISER National Project” katika ukumbi wa Ubungo Plaza, Dar es Salaam, Tanzania.
‘Programu
hiyo itaiwezesha Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania kusambaza taarifa za hali ya
hewa pamoja na kuelimisha wadau mbalimbali juu ya matumizi sahihi ya taarifa za
hali ya hewa hususan katika sekta za Kilimo, Usafiri majini, Udhibiti wa
majanga, Maji na Nishati hivyo itaongeza nguvu katika kuwafikia wananchi wengi’,alizungumza
Dkt. Kijazi.
Aidha,
aliendelea kueleza kuwa madhumuni makubwa ya program ya WISER
Kitaifa ni kuhakikisha kunakuwa na matumizi sahihi ya tarifa za hali ya hewa
katika sekta mbali mbali za maendeleo kwa lengo la kukabiliana na athari
zitokanazo na mabadiliko ya hali ya hewa na tabianchi.
Kwa upande wa
mratibu
wa programu ya WISER kwa Nchi za Afrika Mashariki, Ndugu. John Mungai alieleza kuwa lengo la warsha ya
uzinduzi huo ni kuwakutanisha wadau na kuwa na uelewa wa pamoja wa programu hii
pia kutoa taarifa ya kuanza kwa utekelezaji wake kwa wadau wanaohusika katika program
hii.
Awali
Rais wa TMS Dkt. Burhani Nyenzi aliwajulisha washiriki kuwa tayari utekelezaji
wa awali umeanza kufanyika kwa kuwajengea
uwezo wadau wa sekta husika pamoja na wanahabari katika mikoa ya Dodoma, Simiyu,
Tanga na Manyara.
Programu
hii inafadhiliwa na Serikali ya Uingereza kupitia Shirika lake la Kimataifa la
maendeleo (DFID) na ulijumuisha wadau mbalimbali wakiwemo wizara na taasisi za
serikali, taasisi zisizo za kiserikali (NGO), mashuleni, watendaji wa vijiji na
wanahabari.
No comments:
Post a Comment