Friday, September 20, 2019

BALOZI SEIF AFURAHISHWA NA HATUA YA TMA KUANZA KUTEKELEZA MKATABA WA KUSITISHA MATUMIZI YA ZEBAKI NCHINI.

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhe. Mhandisi Isack Kamwelwe akitoa ufafanuzi kwa Mh.Balozi Seif, Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar katika banda la TMA wakati wa mkutano wa mawaziri wa SADC wa sekta ya tehama, Habari, uchukuzi na hali ya hewa ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Mwl. Julius Nyerere, Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Huduma za Utabiri ambaye pia ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TMA, Dkt. Hamza Kabelwa akitoa maelezo kwa viongozi katika banda la TMA wakati mkutano wa mawaziri wa SADC wa sekta ya tehama, habari, uchukuzi na hali ya hewa ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Mwl. Julius Nyerere, Dar es Salaam

Washiriki kutoka TMA katika picha ya pamoja na Katibu Mkuu wa Uchukuzi Dkt. Leonard Chamuriho katika banda la TMA wakati mkutano wa mawaziri wa SADC wa sekta ya tehama, habari, uchukuzi na hali ya hewa ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Mwl. Julius Nyerere, Dar es Salaam


Mwakilishi wa Shirika la Hali ya Hewa Duniani (WMO) Kikanda, Bw. Mark Majodina akipata maelezo katika banda la TMA wakati mkutano wa mawaziri wa SADC wa sekta ya tehama, habari, uchukuzi na hali ya hewa ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Mwl. Julius Nyerere, 
Dar es Salaam


Mkuu wa Taasisi ya Hali ya Hewa ya Zimbabwe Bi. Rebecca Manzou akipata maelezo katika banda la TMA wakati mkutano wa mawaziri wa SADC wa sekta ya tehama, habari, uchukuzi na hali ya hewa ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Mwl. Julius Nyerere, Dar es Salaam

Bi. Rukia Mtingwa kutoka Zantel akipata elimu ya huduma za hali ya hewa katika banda la TMA wakati mkutano wa mawaziri wa SADC wa sekta ya tehama, habari, uchukuzi na hali ya hewa ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Mwl. Julius Nyerere, Dar es Salaam.



Tarehe 20/09/2019: “Nimefurahi kusikia Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imeanza kutelekeza mkataba wa MINAMATA wa kusitisha matumizi ya zebaki katika vifaa vya hali ya hewa”, alizungumza Mhe. Balozi Seif Ali Iddi, Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, mara baada ya kufunga mkutano wa mawaziri wa SADC wa sekta ya tehama, habari, uchukuzi na hali ya hewa na kutembelea banda la TMA kwenye ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Mwl. Julius Nyerere, Dar es Salaam.


Naye, Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhe. Mhandisi Isack Kamwelwe alimueleza Mhe. Balozi Seif kuwa serikali inaangalia namna sahihi ya kuweze kuteketeza vifaa hivyo kiusalama Zaidi, kwa vile zebaki ni moja ya vitu vinavyochangia katika uharibifu wa mazingira. 


Kwa upande wa Mkurugenzi wa Huduma za Utabiri ambaye pia ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TMA, Dkt. Hamza Kabelwa alisema kuwa, TMA imeshafanikisha zoezi hilo la kuacha matumizi ya vifaa vyenye zebaki vikiwemo vipima joto (thermometers), vipima mgandamizo wa hewa (barometers) n.k kwa asilimia kubwa kwa kuwezeshwa na serikali upatikanaji wa vifaa ambavyo havitumii zebaki.


Mkutano huo umefungwa rasmi leo tarehe 20 Septemba 2019. Kauli mbiu ya mkutano huo ilikuwa ‘Mazingira Wezeshi kwa Ukuaji wa Uchumi Jumuishi na Endelevu, Kukuza Biashara katik Jumuiya na Kuongeza Fursa ya Ajira’

No comments:

Post a Comment

Featured Post

DKT. KIJAZI: KIWANGO CHA USAHIHI WA UTABIRI WA MSIMU WA VULI 2019 KIWE CHA JUU ZAIDI.

Mkurugenzi mkuu wa TMA na Makamu wa Tatu wa Rais wa Shirika la Hali ya Hewa Duniani Dkt. Agnes Kijazi (katikati mwenye suti nyeusi) waka...