Wataalamu wa hali ya hewa kutoka TMA wakiendelea utoa elimu wa wageni kwenye maonesho ya wiki ya viwanda ya SADC, Ukumbi wa Julius Nyerere, Dar es Salaam |
Wataalamu wa hali ya hewa kutoka TMA wakiendelea kutoa elimu kupitia vyombo vya habari kwenye maonesho ya wiki ya viwanda ya SADC, Ukumbi wa Julius Nyerere, Dar es Salaam |
Tarehe 8/08/2019; Naibu waziri wa Wizara ya Viwanda na Biashara Mhe. Mhandisi Stella M. Manyanya (MB) ameipongeza
Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) kwa kazi nzuri inayoifanya kwa kutoa
taarifa sahihi za hali ya hewa kwa wananchi.
Alizungumza hayo
wakati alipotembelea banda la TMA katika Maonesho ya Wiki ya Viwanda ya SADC,
viwanja vya ukumbi wa Julius Nyerere, Dar es Salaam.
‘Nawapongeza sana
TMA kwa kazi nzuri mnayoifanya kwa sasa ya umakini ambao umehakikisha kiwango
cha usahihi kimekuwa juu hivyo kutoa tabiri za kweli’
Aliongezea kwa
kusema kutokana na usahihi huo, wizara ya viwanda imeweza kunufaika katika
maendeleo ya ukuaji wa viwanda hususani upatikanaji wa malighafi za kilimo n.k
Kwa upande mwingine
alitoa pongezi zake za dhati kwa Mkurugenzi Mkuu wa TMA Dkt. Agnes Kijazi kwa
kuchaguliwa kuwa Makamu wa Tatu wa Rais wa Shirika la Hali ya Hewa Duniani na
hivyo kuiletea sifa nchi na kuwakilisha vyema wanawake wa Tanzania kimataifa
Alimalizia kwa kuwataka wafanyakazi wa
TMA kuendelea kuchapa kazi kwa vile mchango wao unaonekana katika maendeleoya
nchi
No comments:
Post a Comment