Elimu ya sayansi ya hali ya hewa ikiendelea kutolewa - Simiyu |
Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imeshiriki
katika maonesho ya 27 ya Nanenane yaliyofanyika katika viwanja vya Mwakangale
mkoani Mbeya, viwanja vya Nanenane Mkoani Morogoro na kitaifa kwa mara ya pili yanafanyika
katika viwanja vya nyakabindi mkoani Simiyu, yaliyoenda sambamba na kauli mbiu
isemayo “ Kilimo, mifugo na uvuvi kwa ukuaji wa uchumi wa Nchi.
Katika ufunguzi wa maonesho hayo tarehe 01 Agosti 2019,
Mhe. Samia aliwataka watafiti wote nchini kutoa matokeo ya utafiti kwa walengwa
kwa kuwapatia elimu ya kutosha ili waweze kunufaika na tafiti hizo.
“Nitoe rai kwa watafiti wote nchini kutoa matokeo ya
tafiti zenu kwa walengwa na kuwapa elimu ya kutosha ili waweze kunufaika
ipasavyo” aliongea mama Samia.
Katika kufanikisha rai hiyo ya Makamu wa Rais wa
Jumhuri ya Muungano wa Tanzania, TMA imeanza kwa kutoa elimu kwa wadau
mbalimbali juu ya umuhimu wa kutumia taarifa za hali ya hewa katika kufanya
shughuli zao zenye kuleta tija hususani wakulima na wavuvi ambapo zoezi la
utoaji wa elimu hiyo linatarajiwa kuendelea mpaka siku ya kilele cha
maadhimisho hayo tarehe 08 Agosti 2019.
IMETOLEWA NA OFISI YA UHUSIANO
MAMLAKA YA HALI YA HEWA TANZANIA
No comments:
Post a Comment