Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) ni miongoni mwa taasisi
za serikali zinazowakilisha Tanzania kikanda na kimataifa katika masuala ya
hali ya hewa. Aidha Tanzania kupitia TMA inashiriki katika kutekeleza itifaki
ya SADC ya Uchukuzi, Mawasiliano na Hali ya Hewa na mpango mkakati wake kama
ifuatavyo:
i.
Ushiriki katika Umoja wa Taasisi za Hali ya
Hewa za nchi za Kusini mwa Afrika “Meteorological Association of Southern
Africa (MASA)”
Tanzania kupitia TMA ni mwanachama wa MASA.
MASA ni Umoja wa Taasisi za Hali ya Hewa za nchi za Kusini mwa Afrika
ulioanzishwa mwaka 1999. Umoja huu ulianzishwa kwa lengo la kushirikiana na kuratibu
utekelezaji wa programu mbalimbali za hali ya hewa zinazotekelezwa katika
ukanda wa SADC. Katika kutimiza jukumu hilo, wanachama wa MASA hufanya mikutano
kila mwaka ili kujadili utekelezaji na kutoa mapendekezo kwa ngazi mbalimbali
za maamuzi za SADC. Katika Umoja huu,
Tanzania kupitia TMA imechaguliwa kuwa Mwenyekiti
wa Umoja wa Taasisi za Hali ya Hewa za nchi za SADC “SADC Meteorological
Association of Southern Africa (SADC-MASA)” kwa kipindi cha miaka miwili
kuanzia mwaka huu wa 2019, kabla ya hapo Tanzania ilikuwa ikishika nafasi ya Makamu Mwenyekiti wa MASA tangu mwaka 2016.
Sambamba na nafasi hiyo, wataalamu wa TMA
wamekuwa wakishiriki katika shughuli mbalimbali zenye lengo la kuimarisha
ushirikiano na utengamano uliopo kati ya wanachama wa SADC ambazo ni pamoja na
ukaguzi wa hesabu za fedha za MASA, kujengea uwezo kwa baadhi ya Taasisi za
Hali ya hewa za nchi wanachama wa SADC katika eneo la utoaji wa huduma bora za
hali ya hewa “ Quality Management System (QMS)” na mfumo wa utoaji wa tahadhari
kutokana na hali mbaya ya hewa “ Common Alerting Protocol (CAP)”.
ii.
Ushiriki katika Kamati ya Sekta ya Hali ya
Hewa kwa nchi wanachama wa SADC
“Sub-Sectoral Committee on Meteorology (SCOM)”
Tanzania kupitia Mamlaka ya Hali ya Hewa
Tanzania (TMA) imekabidhiwa Uenyekiti
wa Kamati ndogo ya Sekta ya Hali ya Hewa ya nchi wanachama wa Jumuiya ya
Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC) “Sub-Sectoral Committee on Meteorology
(SCOM) kwa kipindi cha mwaka mmoja. Kupitia mikutano inayofanyika kila mwaka ya
SCOM, Mamlaka hushirikiana na Taasisi zingine za
Hali ya Hewa za nchi wanachama wa SADC kujadili utekelezaji wa masuala
mbalimbali yanayohusu sekta ya hali ya hewa ambapo hutoa mapendekezo kwa ngazi za
juu za SADC hivyo kuchangia katika uboreshaji wa huduma za hali ya hewa katika
nchi wanachama wa SADC.
iii.
Kongamano la nchi za kusini mwa Afrika la
kuandaa utabiri wa msimu wa hali ya hewa“Southern Africa Regional Climate
Outlook Forum (SARCOF)”
Tanzania kupitia Mamlaka ya Hali ya Hewa
Tanzania (TMA) hushiriki kongamano la wataalamu ili kuandaa utabiri wa kikanda
wa msimu wa mvua kwa nchi wanachama wa SADC “Southern Africa Regional Climate Outlook Forum (SARCOF)”. Utabiri
huu wa hali ya hewa huandaliwa kwa
ushirikiano wa wataalamu wa taasisi za hali ya hewa na wadau wengine kutoka
nchi wanachama wa SADC.
iv.
Programu maalumu ya kuangalia hali mbaya ya
hewa “Severe Weather Forecasting Demonstration Project SWFDP - Southern Africa”
Tanzania kupitia Mamlaka ya Hali ya Hewa
Tanzania (TMA) inashiriki katika programu maalumu ya kufuatilia na kutoa
taarifa za hali mbaya ya hewa (vimbunga, mafuriko, joto kali n.k) kwa nchi wanachama
wa SADC hivyo kusaidia nchi kujipanga katika kukabiliana na athari zinazoweza
kujitokeza.
Faida zinazopatikana kwa Taifa kutokana na
ushiriki wa TMA katika SADC
i.
Kuboresha huduma za hali ya hewa kupitia mafunzo ya hali ya hewa
yanayotolewa kwa nchi wanachama wa SADC kupitia programu mbalimbali za hali ya
hewa.
ii.
Kupatikana kwa baadhi ya miundombinu ya hali ya hewa inayotolewa kupitia
programu na miradi ya hali ya hewa inayotekelezwa kwa nchi wanachama wa SADC.
iii.
Kupata utabiri wa misimu ya mvua kwa ukanda wa SADC unaoandaliwa kwa
ushirikiano wa wataalamu wa taasisi za hali ya hewa na wadau wengine kutoka nchi
wanachama.
iv.
Kupata taarifa za hali mbaya ya hewa kwa nchi wananchama ikiwemo Tanzania
v.
Kupata ujuzi unaotokana na ushirikiano na kubadilishana uzoefu baina ya
Taasisi za hali ya hewa za nchi wanachama wa SADC.
vi.
Kuimarisha ushiriki na ushawishi wa Tanzania katika masuala ya hali ya hewa
kikanda na kimataifa.
TMA IMEJIPANGAJE KUFIKIA AZMA YA MWENYEKITI YA UCHUMI WA VIWANDA KATIKA
SADC?
i.
Kutoa huduma bora za hali ya hewa zitakazosaidia upatikanaji wa malighafi
kwa ajili ya viwanda kama vile mazao.
ii.
Kutoa huduma bora za hali ya hewa zitakazosaidia kuongeza ufanisi na tija
katika ujenzi wa miundo mbinu ya viwanda na uendeshaji wa viwanda vyenyewe.
iii.
Tanzania kupitia TMA itaendelea kusaidia nchi zingine wanachama wa SADC
katika kuboresha huduma za hali ya hewa ikiwa ni pamoja na kuanzisha mifumo ya
kiutendaji.
No comments:
Post a Comment