Mamlaka ya Hali ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) inashiriki maonesho ya 4 ya wiki ya viwanda SADC yanayoendelea katika viwanja vya ukumbi wa mwl. Nyerere, Dar es Salaam kuanzia tarehe 05 mpaka 09 Agosti 2019.
Katika maonesho hayo wananchi mbalimbali wameweza kupata elimu ya sayansi ya hali ya hewa katika kuchochea ukuaji wa sekta ya viwanda kwenye nchi za kusini mwa Afrika, ambapo wataalamu walipata fursa ya kuelezea umuhimu wa matumizi ya taarifa za hali ya hewa kwenye sekta zinachochea moja kwa moja ukuaji wa uchumi wa viwanda ikiwa na pamoja na upatikanaji wa malighafi,mitambo n.k.
Akizungumza na wananchi waliotembelea banda hilo, meneja wa huduma za hali ya hewa kwa usafiri wa anga na majini Bw. John Mayunga aliwaeleza wananchi jinsi usafiri wa anga na usafiri wa majini unavyoathirika na hali mbaya ya hewa hivyo kusisitiza kufuatilia na kufanya maamuzi stahiki taarifa hizo katika shughuli za usafirishaji.
Kwa upande wake Bw. Wilberforce Kikwasi mtabiri mwandamizi aliendelea kuwaasa wananchi kutumia fursa ya utabiri unaotolewa na TMA katika viwanja hivyo katika kufungasha bidhaa zao huku akitolea mfano wa mafuta ya mgando yaliyoyeyu kakutokana na joto la linaloendelea katika jiji la Dar es Salaam hususan muda wa mchana.
Katika maonesho hayo TMA imewaka ‘screen’ maalumu inayoonesha utabiri wa hali ya hewa kwa siku za 5 za maonesho hayo, hivyo kuweka fursa kwa washiriki na wananchi kwa ujumla kupata taarifa hizo sambamba na elimu.
No comments:
Post a Comment