Tuesday, December 31, 2019
Monday, December 30, 2019
MENEJIMENT YA TMA YAJIPANGA UTEKELEZAJI WA SHERIA YA MAMLAKA YA HALI YA HEWA TANZANIA
Mkurugenzi wa Ofisi ya Zanzibar-TMA, Ndugu, Mohamed Ngwali akizungumza katika kikao kazi cha kujenga uelewa na mkakati wa utelezaji wa sheria ya Mamlaka ya Hali ya Hewa kilichofanyika Kibaha, Tarehe 27-28 Desemba 2019. |
Mkurugenzi wa Huduma za Utabiri-TMA, Dkt. Hamza Kabelwa akizungumza katika kikao kazi cha kujenga uelewa na mkakati wa utelezaji wa sheria ya Mamlaka ya Hali ya Hewa kilichofanyika Kibaha, Tarehe 27-28 Desemba 2019. |
Mkurugenzi wa Utafiti na Matumizi-TMA, Dkt. Ladislaus Chang'a akizungumza katika kikao kazi cha kujenga uelewa na mkakati wa utelezaji wa sheria ya Mamlaka ya Hali ya Hewa kilichofanyika Kibaha, Tarehe 27-28 Desemba 2019. |
Mkurugenzi wa TEHAMA na Huduma za Ufundi-TMA, Dkt. Pascal Waniha akizungumza katika kikao kazi cha kujenga uelewa na mkakati wa utelezaji wa sheria ya Mamlaka ya Hali ya Hewa kilichofanyika Kibaha, Tarehe 27-28 Desemba 2019. |
Meneja Rasilimali Watu Bi. Mariam Is-Haaq akizungumza katika kikao kazi cha kujenga uelewa na mkakati wa utelezaji wa sheria ya Mamlaka ya Hali ya Hewa kilichofanyika Kibaha, Tarehe 27-28 Desemba 2019. |
|
Kibaha,
28 Desemba 2019;
Menejimenti
ya Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imefanya kikao kazi kwa siku mbili
ili kupitia kwa pamoja na kupata uelewa wa namna bora ya utekelezaji wa sheria
Na. 2 ya mwaka 2019 ya Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania.
Akizungumza
wakati wa kufunga kikao kazi hicho, Mkurugenzi Mkuu wa TMA na mwenyekiti wa
kikao aliwataka wakurugenzi na mameneja kujenga utamaduni wa utendaji kazi wenye
lengo la uboreshaji huduma ilikufikia malengo ya Mamlaka katika utekelezaji wa
sheria iliyopo. Aidha, aliwapongeza na kuwashukuru washiriki wa kikao kazi
hicho kwa jinsi walivyojitoa kuifanya kazi hiyo kwa umakini mkubwa kwa zaidi ya
saa kumi na mbili za kazi kila siku pasipo mtu yoyote kuondoka.
‘Nataka
baada ya kikao hiki viongozi wote muwe mstari wa mbele katika kuhakikisha
watumishi mnaowasimamia wana fahamu sheria, taratibu na kanuni kwenye utekelezaji
wa majukumu yao kwa maslahi ya Mamlaka na Taifa kwa ujumla’. Alizungumza Dkt.
Kijazi.
Awali,
akifungua kikao kazi hicho Dkt. Kijazi aliwapongeza wafanyakazi wote wa TMA kwa
utendaji mzuri wa kazi uliopelekea kufanikiwa kukishikilia cheti cha ubora cha
ISO 9001:2015 baada ya ukaguzi uliofanyika kati ya tarehe 16 na 20 Disemba,
2019 ambapo TMA ilikaguliwa na Mkaguzi wanje kutoka Canada.
Kikao
kazi hicho kiliwakutanisha Mkurugenzi Mkuu, wakurugenzi, Mkurugenzi Ofisi ya
Zanzibar, Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Hali ya Hewa- Kigoma, mameneja kutoka
makao makuu, mameneja wa Kanda na wanasheria wa TMA.
Awali,
wajumbe walipitia vifungu vyote vya sheria na kujadili kwa kina ili kuhakikisha
viongozi wote wa Mamlaka wanakuwa na uelewa wa pamoja wa sheria hiyo ili
kurahisisha utekelezaji wake katika maeneo yao ya kazi na hivyo kuchangia
katika ustawi wa maendeleo ya nchi kupitia sayansi ya hali ya hewa.
Aidha,
wajumbe hao waliainisha maeneo ya uboreshaji katika kanuni hususan kwenye
udhibiti wa huduma za hali ya hewa katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ukusanyaji
mapato, utoaji huduma za hali ya hewa kwa usahihi na kwa wakati pamoja na kutoa
elimu kwa umma na wadau kuhusu sheria ya Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania.
‘Tunapaswa
kutoa elimu kwa umma hasa wale wadau ambao wanamiliki vituo vya hali ya hewa watambue
kwamba ni kosa kisheria kuwa na vituo ambavyo havijasajiliwa na pia kutumia
vifaa ambavyo havijahakikiwa (calibration) na TMA’ . Alisema Dkt. Kijazi.
Naye
Mkurugenzi wa Ofisi ya Zanzibar-TMA, Ndugu. Mohamed Ngwali akitoa salamu za
shukrani kwa niaba ya washiriki wote, alimshukuru Mkurugenzi Mkuu wa TMA kwa
kufanikisha kikao kazi ambacho kimeongeza uelewa mpana wa matumizi ya sheria
mpya ya TMA na kuahidi kudumisha umoja katika utendaji kazi kwa watumishi wote.
Tuesday, December 24, 2019
TMA YASISITIZA WADAU KUCHOCHEA MATUMIZI SAHIHI YA TAARIFA ZA HALI YA HEWA KATIKA SEKTA ZAO.
Wadau wakiwa kwenye picha ya pamoja na mgeni rasmi, Dkt. Hamza Kabelwa (katikati mwenye miwani) katika warsha ya wadau kutoka sekta mbalimbali inayohusu matumizi sahihi ya taarifa za hali ya hewa baina ya muandaaji na mtumiaji, iliyofanyika katika ukumbi wa Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga, Pwani kuanzia Tarehe 22-24 Disemba, 2019. |
Mkurugenzi wa Huduma za Utabiri wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania(TMA), Dkt. Hamza Kabelwa (Kushoto) akizungumza wakati akifungua warsha ya wadau kutoka sekta mbalimbali inayohusu matumizi sahihi ya taarifa za hali ya hewa baina ya muandaaji na mtumiaji, iliyofanyika katika ukumbi wa Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga, Pwani kuanzia Tarehe 22-24 Disemba, 2019. |
Wataalam wa hali ya hewa kutoka TMA wakiwasilisha mada katika warsha ya wadau inayohusu matumizi sahihi ya taarifa za hali ya hewa baina ya muandaaji na mtumiaji, iliyofanyika katika ukumbi wa Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga, Pwani kuanzia Tarehe 22-24 Disemba, 2019. |
Wadau mbalimbali wakichangia mada katika warsha ya wadau kutoka sekta mbalimbali inayohusu matumizi sahihi ya taarifa za hali ya hewa baina ya muandaaji na mtumiaji, iliyofanyika katika ukumbi wa Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga, Pwani kuanzia Tarehe 22-24 Disemba, 2019. |
MKURANGA,
PWANI 22/12/2019;
Mkurugenzi
wa Huduma za Utabiri wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), Dkt. Hamza Kabelwa
kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa TMA Dkt. Agnes Kijazi alifungua warsha ya wadau
kutoka sekta mbalimbali iliyohusu matumizi sahihi ya taarifa za hali ya hewa baina
ya muandaaji na mtumiaji wa taarifa za hali ya hewa, iliyofanyika katika ukumbi
wa Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga, Pwani kuanzia Tarehe 22-24 Disemba, 2019.
Katika
hotuba yake Dkt. Kabelwa alisisitiza wadau mara watakapomaliza warsha hiyo
kuchochea matumizi sahihi ya taarifa za hali ya hewa katika sekta zao ili kupunguza
au kuepusha athari zinazoweza kusababishwa na hali mbaya ya hewa.
“Mkiwa
kama kiunganishi kati ya TMA na wananchi
tunawaomba ninyi washiriki kuchochea matumizi sahihi ya taarifa za hali ya hewa
katika sekta zenu”, alisisitiza Dkt. Kabelwa.
Aidha,
washiriki walikumbushwa kutambua kuwa majanga ya asili hayawezi kuepukika, lakini
taarifa zikiwafikia walengwa kabla ya janga husika kutokea basi zitasaidia kujipanga
ili kukabiliana na madhara yanayoweza kujitokeza, hivyo Dkt. Kabelwa aliwataka
washiriki kushirikiana na TMA kuhakikisha taarifa za hali ya hewa zinawafikia
walengwa kwa wakati na kueleweka.
Warsha
hiyo iliandaliwa na TMA na kufadhiliwa na Shirika la Hali ya Hewa Duniani
(World Meteorological Organization – WMO), chini ya mwamvuli wa Programu ya kidunia
ya kuwaongezea ujuzi waandaaji na watumiaji wa taarifa za hali ya hewa barani
Afrika (Weather and Climate Information Services for Africa - WISER).
Thursday, December 19, 2019
TMA YAWEKA MSISITIZO WA KUKABILIANA NA CHANGAMOTO ZA MABADILIKO YA HALI YA HEWA BAHARINI.
Dkt. Agnes Kijazi, akitoa mada kuhusu umuhimu wa
kuzijengea uwezo mamlaka za hali ya hewa katika nchi wanachama wa shirika la
hali ya hewa duniani.
|
Dkt. Agnes Kijazi,
akishiriki katika jopo la majadiliano kuhusiana na matukio ya hali mbaya ya hewa yanayojitokeza ikiwemo
vimbunga katika bahari.
|
Dkt. Agnes Kijazi,
akitoa mada kuhusiana na mahusiano ya masuala ya Jinsia na changamoto ya
mabadiliko ya hali ya hewa.
|
Kutokea kulia ni Dkt. Agnes Kijazi akifuatiwa na
Mwenyekiti wa IPCC Profesa.
Hoesung Leena pamoja na Dkt.
Ladislaus Chang’a katika picha ya pamoja wakati wa majadiliano kuhusiana na maandalizi ya ripoti ya sita ya
tathmini ya mabadiliko ya hali ya hewa inayotarajiwa kukamilishwa mwaka 2022.
|
Dkt. Ladislaus Chang’a (kulia) akishiriki
katika majadiliano kuhusiana na maandalizi ya Ripoti ya sita ya tathmini ya
mabadiliko ya hali ya hewa inayotarajiwa kukamilishwa mwaka 2022.
|
Katibu
Mkuu wa Shirika la Hali ya Hewa Duniani Prof. Petteri Taalas (wa pili kutoka kulia) wakijadiliana na Mkurugenzi
Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania ambaye pia ni Makamu wa tatu wa Rais wa Shirika la Hali ya Hewa Duniani, Dkt. Agnes
Kijazi, wakiwa pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Uganda pamoja na
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa
Malawi (wa kwanza kutoka kushoto) mara baada ya kusainiwa kwa makubaliano ya
kuimarisha huduma za hali ya hewa katika nchi zinazoendelea baina ya shirika la
hali ya hewa duniani na taasisi za kibenki na mashirika mengine ya kimataifa yakiwemo,
UNDP, AfDB, WFP.
|
Madrid, Hispania Tarehe 13/12/2019;
Mamlaka
ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), imeshiriki Mkutano wa 25 wa Kimataifa wa
Mabadiliko ya Hali ya Hewa (2019 United Nations Framework Convention on Climate
Change-UNFCCC-COP25) uliofanyika tarehe 02-13 Disemba 2019 nchini Hispania.
Pamoja na kutoa mchango na ushauri katika sayansi ya hali
ya hewa kwa ujumbe wa Tanzania ulioshiriki katika Mkutano huo, TMA ilishiriki
pia katika mikutano iliyofanyika sambamba na Mkutano huo wa UNFCCC-COP25, Mkurugenzi
Mkuu wa TMA na Makamu wa Tatu wa Rais wa Shirika la Hali ya Hewa Duniani (WMO),
Dkt. Agnes Kijazi, alishiriki kutoa
mada na baadae katika jopo la majadiliano kuhusiana na umuhimu wa kujenga uwezo
na kuimarisha huduma za hali ya hewa, hususan katika nchi zinazoendelea
sambamba na kuweka msisitizo wa kuhakikisha dunia inaongeza jitihada za kukabiliana na changamoto za
mabadiliko ya hali ya hewa katika maeneo ya bahari na yaliyo kandokando ya
bahari.
“Kumekuwa
na ongezeko la kina cha bahari, ongezeko kubwa la vimbunga kwa upande wa
Afrika, mfano kimbunga IDAI kilishosababisha vifo vya mamia ya watu na kuharibu
mazao na makazi ya watu katika nchi za Msumbiji, Zimbabwe na Malawi, hii inaonesha
kuwa changamoto za mabadiliko ya hali ya hewa ni halisia, ni vyema tukachukua
hatua stahiki sasa”. Alisema Dkt. Kijazi.
Kwa upande mwingine, Dkt Kijazi
alishiriki kutoa mada kuhusiana
na masula ya jinsia na changamoto ya mabadiliko ya hali ya hewa. Dkt. Kijazi,
alisisitiza kuwa kuna tofauti kubwa ya namnna ambavyo mabadiliko ya hali ya
hewa yanawaathiri wanawake, watoto, wazee na wanaume. Wanawake, watoto na wazee
wanaathirika zaidi na mabadiliko ya hali ya hewa hasa katika nchi zinazoendelea
kutokana na nafasi na shughuli zao katika jamii. Dkt. Kijazi aliitaka jumuiya
ya kimataifa kufuata mfano wa Tanzania katika kutoa nafasi kwa wanawake katika
nafasi za maamuzi, ambapo Makamu wa Rais wa Tanzania ni mwanamke, Naibu Spika
ni mwanamke na akasema vilevile na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa
ni mwanamke ambaye ni yeye mwenyewe.
Katika hatua nyingine, Mkurugenzi wa Utafiti na Matumizi kutoka TMA alielezea
umuhimu wa kuimarisha uangazi na uboreshaji wa huduma za hali ya Hewa katika
bara la Afrika na nchi zinazoendelea pamoja na kushiriki katika jopo la
majadiliano kuhusiana na maandalizi ya ripoti ya sita ya tathmini ya mabadiliko
ya hali ya hewa duniani, ambapo tayari kuna ripoti maalamu tatu zimetolewa na
maandalizi yanaendelea kukamilisha ripoti kuu nne na zinatarajiwa kukamilika
mwaka 2022.
Aidha, TMA ilishiriki pia hafla
ya WMO ya kusaini ushirikiano na
washirika wa maendeleo katika uboreshaji wa huduma za hali ya hewa
(Alliance for Hydromet). Hafla hiyo ilimshirikisha Katibu Mkuu wa WMO, Prof.
Petteri Taalas, viongozi mbalimbali wa WMO na viongozi wa Taasisi za Hali ya
Hewa-Afrika ikiwemo Malawi, Uganda na Tanzania.
Subscribe to:
Posts (Atom)
Featured Post
DKT. KIJAZI: KIWANGO CHA USAHIHI WA UTABIRI WA MSIMU WA VULI 2019 KIWE CHA JUU ZAIDI.
Mkurugenzi mkuu wa TMA na Makamu wa Tatu wa Rais wa Shirika la Hali ya Hewa Duniani Dkt. Agnes Kijazi (katikati mwenye suti nyeusi) waka...
-
10 Septemba 2024, Arusha: Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imetoa elimu kwa wadau mbalilmbali wa Ununuzi kuhusu matumizi sahihi ya h...
-
06 Septemba 2024, Dar es Salaam: Wahandisi nchini wamekumbushwa umuhimu wa huduma za hali ya hewa sambamba na kuchangia gharama za upatik...
-
DODOMA; Tarehe 19 Agosti, 2024; Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), imekutana na wadau kutoka sekta mbalimbali nchini ili kujipanga na...