WANASAYANSI WA HALI YA HEWA NCHINI
(METEOROLOGISTS) WAKUTANA KUANDAA MWELEKEO WA HALI YA HEWA KWA KIPINDI
CHA MWEZI OKTOBA HADI DESEMBA 2018
Mamlaka
ya Hali ya Hewa Tanzania(TMA) ikiwa katika maandalizi ya kutoa
utabiri/mwelekeo wa msimu wa mvua za vuli imeandaa mkutano wa
wanasayansi wa hali ya hewa (meteorologists) kujadili rasimu ya mwelekeo
huo.
Akizungumza katika
ufunguzi wa mkutano huo, mgeni rasmi ambaye ni mkurugenzi mkuu wa TMA,
Dkt. Agnes Kijazi amewataka wataalam hao kuandaa kwa pamoja na kupitia
mfumo mzima wa uaandaaji ili kujiridhisha na utabiri utakao tolewa hapo
baadae sambamba na kutoa mapendekezo ya uboreshaji katika maandalizi
mengine ya misimu ijayo. Aidha Dk. Kijazi aliwapongeza wanasayansi hao
kwa kazi nzuri wanayoifanya ya kutoa utabiri wenye viwango vya juu vya
usahihi kwa zaidi ya asilimia 80 na kuwataka waendelea kufanya kazi kwa
bidii na ushirikiano ili kufikia juu ya asilimia 90.
Hii
ni mara ya kwanza kwa TMA kuwakutanisha wanasayansi kutoka vituo vyote
nchini ambapo awali kazi ya uandaaji utabiri ilikuwa ikifanywa na
wanasayansi wa makao makuu na uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwl.
Julius Nyerere (JNIA) pekee
TMA inatarajia kutoa mwelekeo wa msimu wa mvua za vuli kwa mikoa inayopata mvua mara mbili kwa mwaka tarehe 06 Septemba 2018.
IMETOLEWA NA MAMLAKA YA HALI YA HEWA TANZANIA
No comments:
Post a Comment