Shirika la Hali ya Hewa Duniani (World Meteorological
Organization (WMO)) ni taasisi mahsusi la Umoja wa Mataifa inayoshughulikia
masuala ya ushirikiano wa kimataifa yanayohusiana na ufuatiliaji wa mifumo ya
hali ya hewa na namna mifumo hii inavyoathiri mazingira yetu. Shirika hufanya kazi
zake kupitia taasisi za hali ya hewa za nchi wanachama (National Meteorolgical
and Hydrological Services - NMHSs) ambapo Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA)
ni mwakilishi rasmi wa shirika hili hapa nchini.
Katibu
Mkuu wa WMO amefanya ziara katika ofisi za TMA ili kujionea shughuli za hali ya
hewa na namna ambavyo WMO inaweza kusaidia katika maeneo mbalimbali yahusuyo
hali ya hewa ikiwa pamoja na mafunzo na vifaa vya hali ya hewa. Aidha
aliipongeza TMA katika juhudi zake za
utekelezaji wa programu za WMO na
kuzisaidia nchi zingine za Afrika. Aliongeza kwa kusema kuwa TMA ni taasisi ya
mfano Afrika katika utoaji wa huduma bora za hali ya hewa
Nae
mkurugenzi mkuu wa TMA dkt. Agnes Kijazi
aliwashukuru Prof. Taalas kwa uamuzi wake wakutembelea Tanzania na
alimuahidi kuwa Tanzania kupitia TMA itaendelea kutekeleza makubaliano yote ya
kimataifa yahusuo huduma za hali ya hewa ikiwa ni pamoja na utekelezaji wa
program za WMO
Ikumbukwe kuwa WMO huratibu na kusaidia katika kuboresha huduma
za hali ya hewa katika nchi kama vile kuanzisha mitandao ya ufuatiliaji wa hali
ya hewa, kuweka miongozo inayosaidia utoaji wa huduma za hali ya hewa kwa
viwango na ubora wa kimataifa n.k
Kupitia WMO Tanzania na Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania
imenufaika na kuongezewa uwezo kupitia mafunzo, miundombinu ya hali ya hewa, hushiriki
kikamilifu katika shughuli za jopo la sayansi la kimataifa la ufuatiliaji wa
mabadiliko ya hali ya hewa (Intergovernmental Pannel on Climate Change - IPCC).
Pia, kushiriki katika shughuli za kongamano la Umoja wa Mataifa
linaloshughulikia masuala ya mabadiliko ya tabia nchi hasa masuala ya kisera
(United Nations Framework for Climate Change Conference - UNFCCC) ambapo
mabadiliko ya hali ya hewa yanayotokea Tanzania hujumuishwa katika makubaliano
ya kimataifa kwa ajili ya utekelezaji kimataifa na kitaifa kwa faida ya nchi
yetu.
Katibu Mkuu wa WMO Prof Petteri Taalas akisaini kitabu cha wageni, kukutana na wenyeji wake sambamba na picha ya pamoja na menejimenti ya TMA |
Katibu Mkuu wa WMO Prof Petteri Taalas
akipata maelezo kutoka kwa mtaalamu wa hali ya hewa kutoka TMA Bw. Chuki
Sangalugembe kuhusiana na mtambo mkubwa wa kompyuta (Computer Cluster) namna
unavyosaidia katika uandaaji wa taarifa za hali ya hewa.
Katibu Mkuu wa WMO Prof Petteri Taalas akichangia jambo baada ya kupata maelezo ya mfumo wa kisasa utoaji taarifa za hali ya hewa kwa usafiri wa anga wakati alipotemebelea ofisi za hali ya hewa zilizopo katika Uwanja wa ndege wa Kiamataifa wa Julius Nyerere. hewa.
Katibu Mkuu wa WMO Prof Petteri Taalas
akipata maelezo kutoka kwa meneja wa kituo kikuu cha utabiri Bw. Samuel Mbuya
namna ya kuandaa utabiri wa hali ya hewa
|
No comments:
Post a Comment