Monday, August 20, 2018

TMA YAWA MWENYEJI WA MAFUNZO YA UTUMIAJI WA MFUMO WA TEKNOLOJIA YA KUBORESHA HUDUMA ZA UTABIRI WA HALI YA HEWA.

Washiriki wa mafunzo ya kozi ya (OSCAR/SURFACE) kwenye picha ya pamoja na Mgeni rasmi Mhe, Mr. Mrisho Gambo aliyeketi katikati (mstari wa mbele).


MAMLAKA YA HALI YA HEWA TANZANIA YAWA MWENYEJI WA MAFUNZO YA UTUMIAJI WA MFUMO WA TEKNOLOJIA YA KUBORESHA HUDUMA ZA UTABIRI WA HALI YA HEWA KWA NCHI 23 ZINAZOONGEA LUGHA YA KINGEREZA BARANI AFRIKA.

Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini (TMA) imekuwa mwenyeji wa mafunzo  ya utumiaji wa mfumo wa teknolojia ya kuboresha huduma za utabiri wa hali ya hewa kwa nchi 23 zinazoongea lugha ya kingereza barani Afrika (Observing Systems Capability Analysis and Review Tool for the  Metadata of surface - based observing systems ( OSCAR/SURFACE)). Lengo la mafunzo hayo ni kuwajengea uwezo washiriki jinsi ya kutumia  mfumo huo katika nchi zao. Akizungumza wakati wa ufunguzi wa  mafunzo, mkuu wa mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Gambo ambaye pia alikuwa mgeni rasmi, aliwashukuru Shirika la Hali ya Hewa Duniani (WMO) kwa kufadhili mafunzo hayo na kuchagua Arusha kuwa sehemu ya kufanyia mafunzo. Aidha aliwataka washiriki wote kutumia taaluma watakayoipata katika kuongeza ujuzi wa kukabiliana na changamoto zinazoikumba bara la Afrika ili kuhakikisha Afrika haiachwi nyuma katika maendeleo endelevu. Amesisitiza umuhimu wa mchango wa huduma za hali ya hewa kwa maendeleo ya kiuchumi na kijamii wakiwa pamoja na sekta za kilimo, nishati, utalii, afya n.k
Mafunzo hayo yamefanyika Mkoani Arusha kuanzia tarehe 15 hadi 17 Agosti 2018.
Imetolewa na Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania.

No comments:

Post a Comment

Featured Post

DKT. KIJAZI: KIWANGO CHA USAHIHI WA UTABIRI WA MSIMU WA VULI 2019 KIWE CHA JUU ZAIDI.

Mkurugenzi mkuu wa TMA na Makamu wa Tatu wa Rais wa Shirika la Hali ya Hewa Duniani Dkt. Agnes Kijazi (katikati mwenye suti nyeusi) waka...