Dar es Salaam, 21 Aprili 2021:
Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) inatoa taarifa kuhusu kimbunga Jobo
kaskazini mwa kisiwa cha Madagascar.
Kumejitokeza mgandamizo mdogo wa hewa ambao umefikia kiwango cha kimbunga
hafifu kwa jina Jobo. Kimbunga hicho kipo kaskazini mwa Kisiwa cha Madagascar
katika Bahari ya Hindi umbali wa Kilometa 930 na kilometa 1030 kutoka pwani ya Lindi
na Mtwara. Aidha, uwepo wa kimbunga hicho unatarajiwa kusababisha ongezeko la
upepo na mawimbi katika bahari ya Hindi hususan katika Pwani ya mwambao wa mikoa ya Mtwara na Lindi.
Mamlaka inaendelea kufuatiliia mwenendo na mwelekeo wa kimbunga Jobo kwa
kuzingatia mifumo mingine ya hali ya hewa iliyo jirani zaidi na kimbunga hicho ambayo
inaweza kubadili nguvu na mwelekeo wa kimbunga Jobo katika wakati ujao.
Wananchi waendelee kuzingatia tahadhari ya upepo na mawimbi iliyotolewa na
Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania katika maeneo husika. Mamlaka ya Hali ya Hewa
itaendelea kutoa taarifa kila inapobidi.
No comments:
Post a Comment