Monday, November 4, 2019

TMA YATOA ELIMU YA NAMNA TAARIFA ZA HALI YA HEWA ZINAVYOWEZA KUSAIDIA KUKUZA SEKTA YA UWEKEZAJI NCHINI.

Wadau mbalimbali wakipata elimu ya hali ya hewa walipotembelea banda la TMA katika maonesho ya biashara yaliyofanyika katika viwanja vya chuo cha ualimu, Mtwara Tarehe 31 Oktoba - 02 Novemba, 2019
Kaimu meneja TMA, Mtwara Ndg. Elewa Msomba akizungumza na wananchi kupitia vyombo vya habari katika maonesho ya biashara yaliyofanyika katika viwanja vya chuo cha ualimu, Mtwara Tarehe 31 Oktoba - 02 Novemba, 2019

Mtwara, Tarehe 31 Oktoba - 02 Novemba, 2019;  TMA ilishiriki katika kongamano la uwekezaji na maonesho ya biashara yaliyofanyika katika viwanja vya chuo cha ualimu, Mtwara . Ushiriki wa TMA katika maonesho hayo ulikuwa ni kutoa elimu kwa wadau mbalimbali  walioweza kutembelea katika banda lake lililokuwa katika maonesho hayo, aidha TMA ilitumia njia ya vyombo vya habari kuwafikia wananchi wengi zaidi.



Lengo kuu la Mamlaka lilikuwa ni kuwaelimisha wananchi na wawekezaji jinsi ya kuboresha uwekezaji nchini kwa Kufanya matumizi sahihi ya taarifa za hali ya hewa.


 Kwa upande mwingine, wakati wa ufunguzi wa kongamano hilo, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa katika hotuba yake alisisitiza taasisi za serikali kushirikiana kwa karibu na kituo cha uwekezaji Tanzania kuhakikisha malengo ya kupata wawekezaji wengi hapa nchini yanafanikiwa.                                     

No comments:

Post a Comment

Featured Post

DKT. KIJAZI: KIWANGO CHA USAHIHI WA UTABIRI WA MSIMU WA VULI 2019 KIWE CHA JUU ZAIDI.

Mkurugenzi mkuu wa TMA na Makamu wa Tatu wa Rais wa Shirika la Hali ya Hewa Duniani Dkt. Agnes Kijazi (katikati mwenye suti nyeusi) waka...