Tuesday, November 19, 2019

DKT. BURUHANI NYENZI ATEULIWA KUWA MWENYEKITI WA BODI YA MAMLAKA YA HALI YA HEWA TANZANIA (TMA)


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Dkt. Buruhani Salum Nyenzi kuwa mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA).

Dkt. Nyenzi (Tanzania Bara) anashika wadhifa huo kwa kipindi cha pili.

Wakati huo huo, Rais Magufuli amemteua Dkt. Makame Omar Makame kuwa Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya TMA.

Dkt. Makame (Zanzibar) ni Mhadhiri Mwandamizi wa Jiografia katika Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA).

Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi John Kijazi imeelezea kuwa uteuzi wa viongozi hao umeanza tarehe 18 Novemba, 2019.

1 comment:

Featured Post

DKT. KIJAZI: KIWANGO CHA USAHIHI WA UTABIRI WA MSIMU WA VULI 2019 KIWE CHA JUU ZAIDI.

Mkurugenzi mkuu wa TMA na Makamu wa Tatu wa Rais wa Shirika la Hali ya Hewa Duniani Dkt. Agnes Kijazi (katikati mwenye suti nyeusi) waka...