Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania, iliandaa warsha ya siku tatu kwa wadau
wa sekta za uvuvi na Usafirishaji, iliyofanyika Kibaha, Mkoa wa Pwani, tarehe
18 – 20 Julai 2019, kuwaelimisha juu ya umuhimu wa matumizi sahihi ya taarifa za
hali ya hewa katika sekta zao, kama sehemu ya utekelezaji wa mradi wa “Weather and Climate Information services for
Africa (WISER II)”
Mkurugenzi wa Utabiri wa TMA Dkt. Hamza Kabelwa alikuwa mgeni rasmi
katika warsha hiyo. Katika hotuba yake aliwataka washiriki kutoa ushirikiano
katika kuchangia mada mbalimbali zitakazowasilishwa kwao, ili kwa pamoja kutoa
huduma bora za hali ya hewa kwa wananchi ambao ndio walengwa wakuu na kusaidia
kuokoa maisha ya watu na mali zao sambamba na kuongeza kipato katika shughuli
zao za kila siku
“Mtakapofikia mwisho wa warsha hii naamini ninyi mtakuwa mabalozi wazuri
na mtashirikiana na TMA kuhakikisha elimu mliyoipata hapa inasambaa na kuhakikisha taarifa za hali ya hewa
zinawafikia walengwa na kuzitumia ipasavyo” aliyasema hayo Dkt. Hamza Kabelwa.
Aidha, washiriki waliishukuru TMA kwa kuandaa mafunzo hayo kwa
kuwachagua wao kama wawakilishi wa wenzao, hivyo waliahidi elimu waliyoipata
wataifanyia kazi na kuisambaza katika sekta zao hususani jamii inayowazunguka.
No comments:
Post a Comment