Kaimu
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) Dkt. Ladislaus
Chang’a katika picha ya pamoja na
washiriki wa warsha ya mafunzo ya mawasiliano ya kimkakati ya huduma za hali ya
hewa kwa jamii, tarehe 11/07/2019, Kibaha, Pwani
Mameneja
kutoka Ofisi za Kanda za Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) wametakiwa
kuhakikisha wanaweka mikakati bora ya mawasiliano ya huduma za hali ya hewa
katika kanda zao.
Maelekezo
hayo yalitolewa na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TMA Dkt. Ladislaus Chang’a wakati
wa ufunguzi wa warsha ya mafunzo ya mawasiliano ya kimkakati ya huduma za hali
ya hewa kwa jamii ,yaliyoandaliwa kwaajili ya kuwajengea uwezo wakuu hao wa
vituo vya kanda jinsi ya kuwasiliana kwa njia bora na rahisi. Mafunzo hayo yalifanyika
Kibaha, Pwani tarehe 10-11 Julai 2019, na kuwakutanisha mameneja kutoka ofisi
za kanda-TMA, wataalam wa hali ya hewa kutoka Kituo Kikuu cha Utabiri (CFO) na
mtaalam wa mawasiliano kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu.
‘Mtakapo
fikia mwisho wa mafunzo haya, nahitaji kupata mikakati bora ya mawasiliano ya
huduma zetu katika maeneo ya kazi (kanda) zenu yenye lengo la kuboresha
usambazaji wa taarifa za hali ya hewa na hivyo kuchangia nchi yetu kufika
malengo ya Serikali ya uchumi wa kati’, alisema Dkt. Chang’a
Aidha,
aliendelea kwa kuwataka viongozi hao wa Mamlaka kuhakikisha wanaboresha
utendaji wao wa kazi kwa kuongeza juhudi kwenye kila kinachofanyika hususani
njia mahususi za kuwafikia wadau na jamii kwa ujumla.
Warsha hiyo
ya mafunzo imeandaliwa na TMA kwa udhamini wa ‘Department for International
Development (DFID)’ kupitia mradi wa Weather
and Climate Information services for Africa (WISER), wenye lengo la
kuimarisha upatiakanaji, usambazaji na matumizi ya taarifa za hali ya hewa.
IMEANDALIWA NA;
OFISI YA UHUSIANO
MAMLAKA YA HALI YA HEWA TANZANIA (TMA)
|
No comments:
Post a Comment