Friday, June 17, 2016

MJUMBE WA KAMATI KUU YA SHIRIKA LA HALI YA HEWA DUNIA DKT. AGNES KIJAZI ASHIRIKI MKUTANO WA 68 WA KAMATI KUU YA UTENDAJI YA SHIRIKA LA HALI YA HEWA DUNIANI(WMO, EC-68), GENEVA, USWISI.

Picha za pamoja wakati wa Ufunguzi wa Mkutano wa Sitini na Nane wa Kamati Kuu ya Utendaji ya Shirika la Hali ya Hewa Duniani  (WMO-EC 68), tarehe 15-24 Juni 2016, Geneva, Uswisi ambapo Dkt. Agnes Kijazi-Mkurgenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa, ambaye pia ni Mwakilishi wa Kudumu wa Shirika la Hali ya Hewa Duniani na Mjumbe wa "WMO Excecutive Council" anashiriki. Dkt. Kijazi anashiriki katika Mkutano huo pamoja na Meneja wa Mahusiano ya Kimataifa wa TMA, Bw. Wilbert Muruke.

Friday, June 10, 2016

Sensitization Workshop on the Role and Contribution of the Work of the Commission of Climatology and IPCC


Sensitization Workshop on the Role and Contribution of the Work of the WMO Commission of Climatology (CCL) and the Intergovernmental Panel on Climate Change (IPCC) in Effective Implementation of Global Framework for Climate Services (GFCS)

This workshop was held under the auspice of the Global Framework for Climate Services (GFCS) project in Tanzania entitled “Climate Services Adaptation Programme in Africa on Building Resilience in Disaster Risk Management, Food Security, Nutrition and Health”. 

Tuesday, June 7, 2016

MAMLAKA YA HALI YA HEWA (TMA) YATOA MWELEKEO WA HALI YA HEWA KWA KIPINDI CHA JUNI HADI AGOSTI 2016.



Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imetoa utabiri wa mwelekeo wa hali ya hewa kwa kipindi cha Juni hadi Agosti mwaka huu. Akizungumzia kuhusiana na mwelekeo huo kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu, Meneja Kituo Kikuu cha Utabiri Bw. Samwel Mbuya alisema “Nchi yetu inatarajia kuwa na hali ya baridi kiasi katika kipindi hiki sambamba na vipindi vifupi vya mvua vinavyotarajiwa kujitokeza katika maeneo machache hususan ya ukanda wa Ziwa Viktoria na ukanda wa pwani ya Kaskazini (Visiwa vya Unguja na Pemba). Katika kipindi cha mwezi Juni hadi Agosti 2016, maeneo mengi ya nchi yanarajiwa kuwa makavu na yenye hali ya baridi kiasi katika majira haya ya kipupwe

Mifumo ya hali ya hewa inaonesha matarajio ya hali ya joto la wastani hadi chini ya wastani katika maeneo yaliyopo Kusini-magharibi mwa nchi. Hata hivyo, katika msimu wa Kipupwe wa mwaka huu maeneo mengi ya nchi yanatarajiwa kuwa na joto la wastani hadi juu ya wastani. Aidha, izingatiwe kuwa hali ya ubaridi inatarajiwa zaidi nyakati za usiku hadi mapema asubuhi.

  “Aliendelea kueleza sababu za hali hiyo kuwa ni pamoja  na  kupungua kwa joto la bahari katika eneo la ukanda wa Tropiki la bahari ya Pasifiki sambamba na Joto la baharí katika eneo la magharibi wa bahari ya Hindi  kuwa la wastani kwa kipindi cha miezi ya Juni hadi Agosti 2016”. Aidha, joto katika bahari ya Atlantiki linatarajiwa kuwa chini ya wastani. Hali hiyo inatarajiwa kusababisha upepo kuvuma kutoka magharibi ukielekea mashariki hususan katika maeneo ya Ukanda wa Ziwa Viktoria. Joto la bahari la juu ya wastani linatarajiwa katika eneo la ncha ya kusini ya bara la Afrika hivyo kuathiri msukumo wa upepo wa kusi.

Kwa upande mwengine, Afisa Uhusiano wa TMA, Bi. Monica Mutoni alitoa msisitizo kwa wananchi kufuatilia taarifa hususan za tahadhari zinazotolewa na Mamlaka kupitia vyombo mbalimbali vya habari, tovuti ya Mamlaka n.k ili kuokoa maisha na mali. Bi. Monica alisema “Hivi karibuni TMA imekuwa ikitoa tahadhari mbalimbali ikiwa ni pamoja na za kuwepo kwa upepo mkali na mawimbi makubwa kwenye ukanda wa Bahari Hindi, Maziwa na nchi kavu hivyo ni vyema wananchi hasa wale watumiaji wa bahari na maziwa kuchukua hatua stahiki pindi taarifa kama hizo zinapotolewa”.

Aidha, TMA ilipongeza sekta mbalimbali pamoja na Taasisi, Mamlaka za Serikali na jamii kwa ujumla  kwa hatua stahiki zilizochukuliwa katika kipindi cha msimu wa mvua za Masika 2016 kwa kutumia Taarifa, Agalizo na Tahadhari za utabiri zilizotolewa na Mamlaka. Ni wazi kuwa kwa hatua hizo madhara ambayo yangeweza kujitokeza yalidhibitiwa na hivyo kuchangia katika kufanikisha mipango na utekelezaji wa shuguli za kiuchumi na kijamii katika kipindi husika.

Kwa tarifa ya kina kuhusiana na mwelekeo wa hali ya hewa kwa mkoa wako ingia kwenye tovuti ya TMA www.meteo.go.tz au tembelea ofisi zetu

IMETOLEWA NA MAMLAKA YA HALI YA HEWA TANZANIA

Monday, June 6, 2016

MHE. PROF. MBARAWA ATEMBELEA KITUO CHA HALI YA HEWA-IRINGA

Meneja wa Mamlaka ya Hali ya Hewa (TMA), Mkoani Iringa Bw. Haji Musa Usantu akifafanua jambo kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa alipokagua Mamlaka hiyo. 
 Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (Mwenye Kofia) akitazama moja ya kifaa kinachopima hali ya hewa ya udongo alipokagua kiwanja cha Ndege cha Nduli Mkoani Iringa.Kulia ni Meneja wa (TMA) Mkoani humo Bw. Haji Musa Usantu. 
 Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akitoa maelekezo kwa Meneja wa Kiwanja cha Ndege cha Iringa (Nduli), Bi. Hanna Kibupile alipokikagua. 

Picha kwa hisani ya Kitengo cha Mawasiliano- Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano

Thursday, May 26, 2016

HALI YA HEWA TUGHE YAPATA UONGOZI MPYA


Uongozi mpya wa TUGHE katika picha ya pamoja.
Baadhi ya wanachama wa TUGHE wakiomba kura ili kuweza kupata nafasi mbali mbali za uongozi sambamba na zoezi la uchaguzi.
Wanachama wa TUGHE (Pichani) wachagua viongozi wapya katika uchaguzi uliofanyika tarehe 24 Mei 2016 kwenye ukumbi wa Makao Makuu-TMA. Viongozi waliochaguliwa ni pamoja na Mwenyekiti Bi. Aurelia Mwakalukwa, Katibu Bw. Benjamin Bikulamchi, Mwenyekiti wa kinamama Bi. Zainab Gumbo, Katibu wa kinamama Bi. Hamida Hassan na wajumbe.

 Na. Monica Mutoni

Tuesday, May 24, 2016

TV JOURNALIST WEATHER TRAINING DAR ES SALAAM, TANZANIA ON 20th MAY, 2016


This Public Weather Services training for Azam Journalists aimed at strengthening the link between the providers and users of public weather services, so that individuals, communities and organizations can make effective use of the available products and services and foster a better understanding and awareness of public weather services in terms of their availability, the terminology used, the way they can be used to the greatest effect and their socio-economic benefits as well as to easier communication among societies. The training aimed to meet World Met. Organization (WMO) requirements.

Training participants were from AZAM pay TV and training facilitators were from TMA and WMO.

Wednesday, May 18, 2016

SEVERE WEATHER EVENTS- EFFECTIVE PLANNING (SWEEP) TRAINING WORKSHOP HELD FROM 16 TO 27 MAY, 2016, DAR ES SALAAM, TANZANIA


Workshop is held under the auspice of the Pilot Project called “The Multi Hazard Early Warning Service (MHEWS)” which focuses on the coastal zone of Tanzania and across sectors of Marine transport, Fishing, Agriculture, and Oil & Gas. MHEWS project is being funded by DFID trough the WISER program.

The objective of  SWEEP Workshop is to ensure all stakeholders have a shared and consistent understanding of the features and benefits of the Multi-hazard Early Warning Services to effective planning.


Expected output is to equip participants with all the necessary skills and provide information on the characteristics of the extremes and enable improved warning messages, timely and effective communication among actors which will solely serve lives and property and enhance socio-economic development in the country.

Featured Post

DKT. KIJAZI: KIWANGO CHA USAHIHI WA UTABIRI WA MSIMU WA VULI 2019 KIWE CHA JUU ZAIDI.

Mkurugenzi mkuu wa TMA na Makamu wa Tatu wa Rais wa Shirika la Hali ya Hewa Duniani Dkt. Agnes Kijazi (katikati mwenye suti nyeusi) waka...