Monday, August 17, 2026

ATHARI ZA EL NIÑO KATIKA MVUA ZA VULI 2026: TMA YAWANOA WANAHABARI




Dar es Salaam, 17 Agosti 2026

Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imebainisha kuwa hali ya El Niño iliyoanza kujitokeza mwezi Aprili 2026 imeendelea kuimarika na inatarajiwa kuchagiza mwenendo wa mvua za msimu wa Vuli wan Oktoba hadi Disemba 2026 na kuleta vipindi vya hali mbaya ya hewa katika baadhi ya maeneo ya nchi.

 

Hayo yalisemwa na Mkurugenzi Mkuu wa TMA na Makamu Mwenyekiti wa Jopo la Kimataifa la Sayansi ya Mabadiliko ya Hali ya Hewa na Tabia Nchi (IPCC), Dkt. Ladislaus Chang'a, wakati wa warsha ya wanahabari iliyofanyika jijini Dar es Salaam. Warsha hiyo ni mwendelezo wa juhudi za TMA za kuhakikisha kuwa wanahabari wanapata uelewa wa utabiri wa hali ya hewa na tafsiri zake kabla haujatolewa rasmi ili kuifikia jamii kwa usahihi.

 

"Hali ya El Niño inatarajiwa kuendelea kuimarika na kufikia kiwango cha El Nino yenye nguvu kubwa kuelekea mwishoni mwa mawaka na hivyo kusababisha ongezeko la mvua katika ukanda wa Afrika Mashariki " alisema Dkt. Chang'a.

 

Dkt. Chang'a aliongeza kuwa, katika hatua za kuboresha Tuzo za Wanahabari Bora wa Habari za Hali ya Hewa kwa mwaka 2026, TMA na Taasisi ya Usimamizi wa Mazingira na Maendeleo ya Kiuchumi (EMEDO) wameungana ili  kuhakikisha kuwa tukio la utoaji wa tuzo hizo linakuwa kubwa na la kuvutia zaidi. Kwa sababu hiyo, aliwasisitiza wanahabari wote nchini kuwasilisha kazi zao za ushindani ili kuwania Tuzo hizo.

 

Aidha, kwa upande wao,  wanahabari, wameipongeza TMA kwa kuendelea kuboresha usahihi wa utabiri na  huduma za hali ya hewa kwa ujumla.

 

Utabiri rasmi wa Mvua za Vuli ulitolewa rasmi tarehe 18 Agosti 2026.

 

Kauli mbiu ya warsha hiyo ilikuwa: "Kupunguza Pengo la Uelewa wa Tahadhari za Hali ya Hewa kwa Pamoja."






No comments:

Post a Comment

Featured Post

DKT. KIJAZI: KIWANGO CHA USAHIHI WA UTABIRI WA MSIMU WA VULI 2019 KIWE CHA JUU ZAIDI.

Mkurugenzi mkuu wa TMA na Makamu wa Tatu wa Rais wa Shirika la Hali ya Hewa Duniani Dkt. Agnes Kijazi (katikati mwenye suti nyeusi) waka...