Tuesday, February 15, 2022

TMA YAWATAKA WANAHABARI KUENDELEA KUWA MABALOZI WA KUSISITIZA UMUHIMU WA TAARIFA ZA HALI YA HEWA.

Mgeni rasmi, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TMA na Mkurugenzi wa Huduma za Utabiri Dkt. Hamza Kabelwa wakati akifungua rasmi Warsha ya Wanahabari kuhusu Utabiri wa Mvua za Masika (Machi hadi Mei, 2022)  kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa TMA Dkt. Agnes Kijazi katika Ukumbi wa Bandari, Tanga, Tarehe 14/02/2022.

                              Matukio kwa picha wakati waandishi wakisikiliza mada mbalimbali zilizowasilishwa katika Warsha ya Wanahabari kuhusu Utabiri wa Mvua za Masika 2022 katika Ukumbi wa Bandari, Tanga, Tarehe 14/02/2022.
 

Waandishi kutoka vyombo mbalimbali katika picha ya pamoja na mgeni rasmi katika katika Warsha ya Wanahabari kuhusu Utabiri wa Mvua za Masika 2022 katika Ukumbi wa Bandari, Tanga, Tarehe 14/02/2022. Utabiri huo unatarajiwa kutolewa rasmi Tarehe 17 Februari 2022 katika ukumbi wa mikutano wa TMA, Ghorofa ya tatu, Ubungo Plaza - Dar es Salaam, Tanzania.

 

Tanga; Tarehe 14 Februari, 2022;

Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), imewataka wanahabari wote nchini kuendelea kuwa mabalozi wa kusisitiza umuhimu wa matumizi ya taarifa za hali ya hewa nchini. Hayo yalizungumzwa na Mkurugenzi wa Huduma za Utabiri Dkt. Hamza Kabelwa wakati akifungua rasmi Warsha ya Wanahabari kuhusu Utabiri wa Mvua za Masika 2022 kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa TMA Dkt. Agnes Kijazi katika Ukumbi wa Bandari, Tanga, Tarehe 14/02/2022.

“Mamlaka inamchango mkubwa katika ukuaji wa kiuchumi kwa vile huduma za hali ya hewa ni mtambuka na zinahitajika katika kila sekta.Napenda kuwakumbusha kuendelea kuwa mabalozi wazuri wa TMA na daraja kati ya TMA na jamii katika kuelezea na kusisitiza umuhimu wa matumizi ya taarifa za hali ya hewa kwa jamii katika shughuli zetu za kila siku”. Alisema Dkt. Kabelwa.

Aidha, Dkt. Kabelwa alivipongeza vyombo vya habari nchini kwa ushirikiano wake katika kusambaza taarifa za hali ya hewa kwa usahihi na wakati, na kukiri kuwa faida ya kuendelea kufanyika kwa warsha za wanahabari kabla ya kutoa utabiri wa msimu zimeendelea kuonekana.

“Kama mnavyofahamu, warsha hii ni muendelezo wa warsha nyingine nyingi ambazo zimekuwa zikifanyika ikiwa ni juhudi za Mamlaka kutaka kuhakikisha taarifa za utabiri wa hali ya hewa zinawafikia walengwa kwa uhakika, usahihi na kwa wakati. Napenda kukiri kuwa faida za warsha hizi kwa sisi TMA tumeziona kwani mwamko wa jamii sasa hivi umekuwa mkubwa na hata taarifa zinazorushwa kupitia vyombo mbalimbali vya habari  zimekuwa katika lugha rahisi na inayoeleweka kwa jamii, hivyo kwa hatua hii napenda kuwapongeza na muendelee kuongeza bidii ili kufikia malengo ya juu na kuwafikia watanzania wote kwa wakati”. Alieleza Dkt. Kabelwa.

Kwa upande wake mwandishi wa habari kutoka gazeti la Majira, Bi. Penina Malundo alisema kuwa warsha za mafunzo kutoka TMA zimeendelea kuwajengea uwezo hivyo kuwasaidia katika uandishi wa taarifa sahihi bila kupotosha umma na kuwezesha jamii na wadau kujipanga na kuandaa shughuli za kiuchumi na kijamii katika maeneo yao.

Katika warsha hiyo, wanahabari walipata fursa ya kuona rasimu ya utabiri wa hali ya hewa katika kipindi cha mwezi Machi hadi Mei 2022, ambao ni mahsusi kwa maeneo ya Nyanda za juu kaskazini mashariki (Mikoa ya Arusha,Kilimanjaro, Manyara), Pwani ya Kaskazini (Mikoa ya Dar es Salaam, Tanga, Pwani ikijumuisha visiwa vya Mafia), Kaskazini mwa mkoa wa Morogoro pamoja na visiwa vya Pemba na Unguja, Ukanda wa Ziwa Viktoria (Mikoa ya Kagera, Mwanza, Geita,Mara, Simiyu  na Shinyanga) pamoja na Kaskazini mwa mkoa wa Kigoma. Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania inatarajia kutoa rasmi utabiri wa msimu wa mvua za MASIKA 2022 kupitia vyombo vya habari, tarehe 17 Februari 2022.


 

Friday, February 11, 2022

TMA KUENDELEA KUTOA HUDUMA MAHSUSI ZA HALI YA HEWA KWA FAIDA ZA KIUCHUMI.


Wadau kutoka sekta mbalimbali wakiwa katika picha ya pamoja na mgeni rasmi katika mkutano wa wadau, kujadili Utabiri wa Mvua za Msimu wa Masika (Machi hadi Mei, 2022) , katika Ukumbi wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT). Utabiri huo unatarajiwa kutolewa rasmi Tarehe 17 Februari 2022 katika ukumbi wa mikutano wa TMA, Ghorofa ya tatu, Ubungo Plaza - Dar es Salaam, Tanzania.


Mgeni rasmi, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TMA na Mkurugenzi wa Matumizi na Utafiti Dkt. Ladislaus Chang'a akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa TMA Dkt. Agnes Kijazi wakati akifungua rasmi Mkutano wa Wadau wa Utabiri wa Mvua za Masika (Machi hadi Mei, 2022) , katika Ukumbi wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT). Utabiri huo unatarajiwa kutolewa rasmi Tarehe 17 Februari 2022 katika ukumbi wa mikutano wa TMA, Ghorofa ya tatu, Ubungo Plaza - Dar es Salaam, Tanzania.



Mkurugenzi wa Huduma za Utabiri wa TMA, Dkt. Hamza Kabelwa  akiongea kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi Dkt. Ladislaus Chang'a kufungua Mkutano wa Wadau wa Utabiri wa Mvua za Masika (Machi hadi Mei, 2022) , katika Ukumbi wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT). Utabiri huo unatarajiwa kutolewa rasmi Tarehe 17 Februari 2022 katika ukumbi wa mikutano wa TMA, Ghorofa ya tatu, Ubungo Plaza - Dar es Salaam, Tanzania.


Mtaalam wa Hali ya hewa kutoka TMA, Bi. Rose Senyagwa akiwasilisha mada katika Mkutano wa Wadau wa Utabiri wa Mvua za Masika (Machi hadi Mei, 2022) , katika Ukumbi wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT). Utabiri huo unatarajiwa kutolewa rasmi Tarehe 17 Februari 2022 katika ukumbi wa mikutano wa TMA, Ghorofa ya tatu, Ubungo Plaza - Dar es Salaam, Tanzania.

Mtaalam wa Hali ya hewa kutoka TMA, Bw. Ramadhani Omary akiwasilisha mada katika  Mkutano wa Wadau wa Utabiri wa Mvua za Masika (Machi hadi Mei, 2022) , katika Ukumbi wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT). Utabiri huo unatarajiwa kutolewa rasmi Tarehe 17 Februari 2022 katika ukumbi wa mikutano wa TMA, Ghorofa ya tatu, Ubungo Plaza - Dar es Salaam, Tanzania.









Wadau kutoka sekta mbalimbali wakiwasilisha mada katika  Mkutano wa Wadau wa Utabiri wa Mvua za Masika (Machi hadi Mei, 2022) , katika Ukumbi wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT). Utabiri huo unatarajiwa kutolewa rasmi Tarehe 17 Februari 2022 katika ukumbi wa mikutano wa TMA, Ghorofa ya tatu, Ubungo Plaza - Dar es Salaam, Tanzania.





Wadau kutoka sekta ya mbalimbali wakichangia mada katika  Mkutano wa Wadau wa Utabiri wa Mvua za Masika (Machi hadi Mei, 2022), katika Ukumbi wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT). Utabiri huo unatarajiwa kutolewa rasmi Tarehe 17 Februari 2022 katika ukumbi wa mikutano wa TMA, Ghorofa ya tatu, Ubungo Plaza - Dar es Salaam, Tanzania.










Wataalam bingwa wa hali ya hewa pamoja na wadau kutoka sekta mbalimbali wakiwa katika makundi wakijadili athari na ushauri kwa msimu wa mvua za Masika 2022 kupitia  Mkutano wa Wadau wa Utabiri wa Mvua za Masika (Machi hadi Mei, 2022), katika Ukumbi wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT). Utabiri huo unatarajiwa kutolewa rasmi Tarehe 17 Februari 2022 katika ukumbi wa mikutano wa TMA, Ghorofa ya tatu, Ubungo Plaza - Dar es Salaam, Tanzania.





Matukio kwa picha wakati wadau wakisikiliza mada mbalimbali zilizowasilishwa katika Mkutano wa Wadau wa Utabiri wa Mvua za Masika (Machi hadi Mei, 2022), katika Ukumbi wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT). Utabiri huo unatarajiwa kutolewa rasmi Tarehe 17 Februari 2022 katika ukumbi wa mikutano wa TMA, Ghorofa ya tatu, Ubungo Plaza - Dar es Salaam, Tanzania.



Dar es Salaam; Tarehe 11 Februari, 2022;

Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), imesema itaendelea kuimarisha utoaji wa  huduma mahususi za hali ya hewa ili kuongeza tija na ufanisi katika shughuli za kijamii na kiuchumi. Hayo yalizungumzwa na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TMA na Mkurugenzi wa Matumizi na Utafiti Dkt. Ladislaus Chang’a wakati akifungua rasmi Mkutano wa Wadau wa Utabiri wa Mvua za Masika 2022 kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa TMA Dkt. Agnes Kijazi katika Ukumbi wa Chuo cha Usafirishaji (NIT), Dar es Salaam, Tarehe 11/02/2022.

“Matumizi sahihi ya taarifa za hali ya hewa na hasa katika kipindi ambapo dunia inakabiliwa na changamoto ya mabadiliko ya hali ya hewa na Tabianchi ni muhimu sana na  yatasaidia kufikiwa kwa malengo ya  mpango wa Taifa wa kujenga uchumi wa viwanda nchini na mikakati mingine ya kuleta maendeleo katika jamii na Taifa. TMA itaendelea kuimairisha utoaji wa  huduma mahsusi za hali ya hali ya hewa ili kuhakikisha malengo yanafikiwa”. Alisema Dkt. Chang’a.

Aidha, katika mkutano huo TMA ilitoa tathimini ya usahihi wa utabiri wa Msimu wa mvua za vuli 2021 zilizoisha mwezi Desemba 2021, ambapo tathmini hiyo ilionesha kuwa utabiri ulikuwa sahihi kwa asilimia 93.8, hivyo mamlaka inaendelea kuweka msisitizo wa matumizi sahihi ya taarifa za hali ya hewa kwa kila sekta ili kuongeza tija na uzalishaji.

Kwa upande wa mdau kutoka Wizara ya Kilimo, Bw. Juma Makandi alisema mara baada ya kupata taarifa za utabiri wa msimu wa mvua za Vuli, Wizara iliaandaa na kutoa  tafsiri ya utabiri huo katika shughuli za kilimo kwa mawaziri pamoja na wakuu wa mikoa kwa ajili ya kuwawezesha kuweka mipango stahiki ya kukabiliana na athari za utabiri huo..

Naye, mdau wa Kilimo kutoka Zanzibar Bw. Nasoro Mkarafuu alieleza kuwa utabiri ulikuwa kama ulivyotabiriwa hivyo mipango iliyowekwa ya kushirikisha maafisa ugani ilienda kama ilivyopangwa.

Mdau kutoka ofisi ya Waziri Mkuu, Idara ya Maafa alisema baada ya kupokea utabiri huo, idara iliandaa kikao kazi cha kujadili mpango wa dharura wa ukame unaoweza kujitokeza kutokana na utabiri uliotolewa sambamba na kuandaa vipindi vya elimu kwa umma kupitia vyombo mbalimbali va habari.

Katika Mkutano huo, wadau walipata fursa ya kuona rasimu ya utabiri wa hali ya hewa katika kipindi cha mwezi Machi hadi Mei 2022 na kuweza kutoa ushauri utaowezesha kuandaa mbinu na mipango ya kukabiliana na athari za utabiri huo. Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania inatarajia kutoa rasmi utabiri wa msimu wa mvua za MASIKA 2022 kupitia vyombo vya habari, tarehe 17 Februari 2022.




Tuesday, February 8, 2022

TMA YATAKIWA KUBUNI VYANZO ENDELEVU VYA MAPATO



                

Naibu Katibu Mkuu wa Ujenzi na Uchukuzi, Dkt. Ally Possy akizungumza wakati wa ziara ya kutembelea Makao Makuu ya TMA, katika ukumbi wa mikutano ya Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), Ubungo Plaza, Tarehe 07/02/2022.

               

Mkurugenzi Mkuu wa TMA, Dkt. Agnes Kijazi ambale pia ni Makamu wa tatu wa Rais wa Shirika la Hali ya Hewa Duniani (WMO), akifafanua jambo wakati Naibu Katibu Mkuu wa Ujenzi na Uchukuzi, Dkt. Ally Possy  alipotembelea Ofisi za TMA, Makao Makuu, Ubungo Plaza, Tarehe 07/02/2022.

             

           
                                   
                                  
         
     
      
Matukio kwa picha wakati Mhe.Dkt. Ally Possy akipata ufafanunuzi kutoka vitengo mbalimbali vya TMA wakati wa ziara ya kutembelea Makao Makuu ya TMA, Ubungo Plaza, Tarehe 08/02/2022.
 
   

Naibu Katibu Mkuu wa Ujenzi na Uchukuzi, Dkt. Ally Possy akiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi mkuu na wafanyakazi wengine wa TMA baada ya ziara yake  Makao Makuu ya Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), Ubungo Plaza, Tarehe 07/02/2022.

Dar es Salaam; Tarehe 07 Februari, 2022;

Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), yatakiwa kubuni vyanzo endelevu vya mapato ili taasisi iweze kujiendesha na kuisaidia serikali katika uendeshaji wake. Hayo yalizungumzwa na Naibu Katibu Mkuu wa Ujenzi na Uchukuzi, Dkt. Ally Possy wakati alipotembelea Ofisi za TMA, Makao Makuu, Ubungo Plaza, Tarehe 07/02/2022.

“Tusiendeshe Mamlaka kwa hasara, mnatakiwa kubuni vyanzo vya mapato ambavyo vipo “sustainable” bila kuathiri au kuidumaza taasisi, japo tusigeuke kuwa Mamlaka ya ukusanyaji mapato TRA, tutoe huduma lakini pia tukusanye mapato ili kuisaidia serikali katika uendeshaji wake”. Alisema Dkt. Possy.

Katika hatua nyingine, Dkt. Possy aliipongeza TMA kuwa ni taasisi ya tofauti inayofanya kazi kwa ushirikiano wa pamoja na kupelekea kufanya kazi nzuri ya kusaidia maendeleo ya kimkakati na kijamii nchini. Aidha, aliahidi kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi kuendelea kutoa ushirikiano mkubwa kwa TMA pale itakapohitajika.

Naye Mkurugenzi Mkuu wa TMA na Makamu wa tatu wa Rais wa Shirika la Hali ya Hewa Duniani (WMO), Dkt. Agnes Kijazi aliishukuru wizara na kumueleza Naibu Katibu Mkuu kuwa Mamlaka imeshaanza kutekeleza jukumu jipya la uratibu na udhibiti wa huduma za hali ya hewa nchini.

“ Baada ya kusainiwa kwa kanuni 7 za Sheria ya Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania Na. 2 ya mwaka 2019, miongoni mwa jitihada kubwa zilizofanywa na Mamlaka ni pamoja na kuanza utekelezaji wa kanuni hizo kwa ajili ya uratibu na udhibiti wa huduma za hali ya hewa nchini ikiwa ni jukumu jipya ambalo Mamlaka imekasimiwa”. Alisema Dkt. Kijazi.

Friday, February 4, 2022

UWEPO WA KIMBUNGA “BATSIRAI” KATIKA BAHARI YA HINDI

 



Dar es Salaam, 04 Februari 2022:

Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) inatoa taarifa ya uwepo wa kimbunga Batsirai katika maeneo ya Kusini Magharibi mwa bahari ya Hindi. Mamlaka imeendelea kufuatilia kimbunga hicho tangu kilipojitokeza katika bahari ya Hindi tarehe 27/01/2022 na kwa sasa kimesogea katika maeneo ya kisiwa cha Madagascar.

Uchambuzi wa mifumo ya hali ya hewa unaonesha kutokuwepo kwa uwezekano wa kimbunga Batsirai kufika katika Pwani ya Tanzania. Hata hivyo uwepo wa kimbunga Batsirai baharini unatarajiwa kuathiri mifumo ya hali ya hewa kwa baadhi ya maeneo hapa nchini ikiwa ni pamoja na kusababisha ongezeko la mvua; vipindi vya upepo mkali unaofika na kuzidi km 40 kwa saa na mawimbi makubwa baharini yanayozidi mita 2 hasa kwa maeneo ya ukanda wa pwani.

Maeneo yanayotarajiwa kupata vipindi vya mvua kubwa kutokana na uwepo wa kimbunga hicho baharini kati ya tarehe 04 hadi 08/02/2022  ni pamoja na mikoa ya Mtwara, Lindi, Ruvuma, Morogoro, Pwani, Singida, Dodoma, Iringa, Njombe, Mbeya, Songwe na Rukwa. Hata hivyo mvua za Msimu zinaendelea katika maeneo mengine yanayopata mvua hizo.

USHAURI: Wananchi wanashauriwa kuendelea kufuatilia na kuzingatia taarifa za utabiri kutoka Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania pamoja na kupata ushauri na miongozo ya wataalam katika sekta husika ili kupunguza athari zinazoweza kujitokeza.

Mamlaka ya hali ya hewa Tanzania inaendelea kufuatilia mwenendo wa kimbunga hicho na kutoa mrejeo kila itakapobidi.

Featured Post

DKT. KIJAZI: KIWANGO CHA USAHIHI WA UTABIRI WA MSIMU WA VULI 2019 KIWE CHA JUU ZAIDI.

Mkurugenzi mkuu wa TMA na Makamu wa Tatu wa Rais wa Shirika la Hali ya Hewa Duniani Dkt. Agnes Kijazi (katikati mwenye suti nyeusi) waka...