|
Wadau kutoka sekta mbalimbali wakiwa
katika picha ya pamoja na mgeni rasmi katika mkutano wa wadau,
kujadili Utabiri wa Mvua za Msimu wa Masika (Machi hadi Mei, 2022) ,
katika Ukumbi wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT). Utabiri huo
unatarajiwa kutolewa rasmi Tarehe 17 Februari 2022 katika ukumbi wa mikutano wa
TMA, Ghorofa ya tatu, Ubungo Plaza - Dar es Salaam, Tanzania. |
|
Mgeni rasmi, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TMA na Mkurugenzi wa
Matumizi na Utafiti Dkt. Ladislaus Chang'a akizungumza kwa niaba ya
Mkurugenzi Mkuu wa TMA Dkt. Agnes Kijazi wakati akifungua rasmi Mkutano wa
Wadau wa Utabiri wa Mvua za Masika (Machi hadi Mei, 2022) , katika Ukumbi wa
Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT). Utabiri huo unatarajiwa kutolewa rasmi
Tarehe 17 Februari 2022 katika ukumbi wa mikutano wa TMA, Ghorofa ya tatu,
Ubungo Plaza - Dar es Salaam, Tanzania. |
|
Mkurugenzi wa Huduma za Utabiri wa TMA, Dkt. Hamza Kabelwa
akiongea kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi Dkt. Ladislaus
Chang'a kufungua Mkutano wa Wadau wa Utabiri wa Mvua za Masika (Machi hadi Mei, 2022) , katika Ukumbi wa
Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT). Utabiri huo unatarajiwa kutolewa rasmi
Tarehe 17 Februari 2022 katika ukumbi wa mikutano wa TMA, Ghorofa ya tatu,
Ubungo Plaza - Dar es Salaam, Tanzania. |
|
Mtaalam wa Hali ya hewa kutoka TMA, Bi. Rose Senyagwa
akiwasilisha mada katika Mkutano wa Wadau wa
Utabiri wa Mvua za Masika (Machi hadi Mei,
2022) , katika Ukumbi wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT). Utabiri
huo unatarajiwa kutolewa rasmi Tarehe 17 Februari 2022 katika ukumbi wa
mikutano wa TMA, Ghorofa ya tatu, Ubungo Plaza - Dar es Salaam, Tanzania. |
|
Mtaalam wa Hali ya hewa kutoka TMA, Bw. Ramadhani Omary
akiwasilisha mada katika Mkutano wa Wadau wa
Utabiri wa Mvua za Masika (Machi hadi Mei,
2022) , katika Ukumbi wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT). Utabiri huo unatarajiwa kutolewa rasmi
Tarehe 17 Februari 2022 katika ukumbi wa mikutano wa TMA, Ghorofa ya tatu,
Ubungo Plaza - Dar es Salaam, Tanzania. |
|
Wadau kutoka sekta mbalimbali wakiwasilisha mada katika Mkutano wa Wadau wa Utabiri wa Mvua za Masika (Machi hadi Mei, 2022) , katika Ukumbi wa Chuo
cha Taifa cha Usafirishaji (NIT). Utabiri huo unatarajiwa kutolewa rasmi Tarehe 17
Februari 2022 katika ukumbi wa mikutano wa TMA, Ghorofa ya tatu, Ubungo Plaza -
Dar es Salaam, Tanzania. |
|
Wadau kutoka sekta ya mbalimbali wakichangia mada katika Mkutano wa Wadau wa Utabiri wa Mvua za Masika (Machi hadi Mei, 2022), katika Ukumbi wa Chuo cha
Taifa cha Usafirishaji (NIT). Utabiri huo unatarajiwa kutolewa rasmi Tarehe 17 Februari 2022
katika ukumbi wa mikutano wa TMA, Ghorofa ya tatu, Ubungo Plaza - Dar es
Salaam, Tanzania. |
|
Wataalam bingwa wa hali ya hewa pamoja na wadau kutoka sekta mbalimbali wakiwa katika makundi wakijadili athari na ushauri kwa msimu wa mvua za Masika 2022 kupitia Mkutano wa Wadau wa Utabiri wa Mvua za Masika (Machi hadi Mei, 2022), katika Ukumbi wa Chuo cha
Taifa cha Usafirishaji (NIT). Utabiri huo unatarajiwa kutolewa rasmi Tarehe 17 Februari 2022
katika ukumbi wa mikutano wa TMA, Ghorofa ya tatu, Ubungo Plaza - Dar es
Salaam, Tanzania. |
|
Matukio kwa picha wakati wadau wakisikiliza mada
mbalimbali zilizowasilishwa katika Mkutano wa Wadau wa Utabiri wa
Mvua za Masika (Machi hadi Mei, 2022),
katika Ukumbi wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT). Utabiri huo unatarajiwa kutolewa rasmi
Tarehe 17 Februari 2022 katika ukumbi wa mikutano wa TMA, Ghorofa ya tatu,
Ubungo Plaza - Dar es Salaam, Tanzania. |
Dar es Salaam; Tarehe 11
Februari, 2022;
Mamlaka ya Hali ya Hewa
Tanzania (TMA), imesema itaendelea kuimarisha utoaji wa huduma mahususi za hali ya hewa ili kuongeza tija
na ufanisi katika shughuli za kijamii na kiuchumi. Hayo yalizungumzwa na Kaimu
Mkurugenzi Mkuu wa TMA na Mkurugenzi wa Matumizi na Utafiti Dkt. Ladislaus
Chang’a wakati akifungua rasmi Mkutano wa Wadau wa Utabiri wa Mvua za Masika
2022 kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa TMA Dkt. Agnes Kijazi katika Ukumbi wa
Chuo cha Usafirishaji (NIT), Dar es Salaam, Tarehe 11/02/2022.
“Matumizi sahihi ya taarifa za
hali ya hewa na hasa katika kipindi ambapo dunia inakabiliwa na changamoto ya
mabadiliko ya hali ya hewa na Tabianchi ni muhimu sana na yatasaidia kufikiwa kwa malengo ya mpango wa Taifa wa kujenga uchumi wa viwanda
nchini na mikakati mingine ya kuleta maendeleo katika jamii na Taifa. TMA
itaendelea kuimairisha utoaji wa huduma
mahsusi za hali ya hali ya hewa ili kuhakikisha malengo yanafikiwa”. Alisema
Dkt. Chang’a.
Aidha, katika mkutano huo TMA
ilitoa tathimini ya usahihi wa utabiri wa Msimu wa mvua za vuli 2021 zilizoisha
mwezi Desemba 2021, ambapo tathmini hiyo ilionesha kuwa utabiri ulikuwa sahihi
kwa asilimia 93.8, hivyo mamlaka inaendelea kuweka msisitizo wa matumizi sahihi
ya taarifa za hali ya hewa kwa kila sekta ili kuongeza tija na uzalishaji.
Kwa upande wa mdau kutoka
Wizara ya Kilimo, Bw. Juma Makandi alisema mara baada ya kupata taarifa za
utabiri wa msimu wa mvua za Vuli, Wizara iliaandaa na kutoa tafsiri ya utabiri huo katika shughuli za
kilimo kwa mawaziri pamoja na wakuu wa mikoa kwa ajili ya kuwawezesha kuweka
mipango stahiki ya kukabiliana na athari za utabiri huo..
Naye, mdau wa Kilimo kutoka
Zanzibar Bw. Nasoro Mkarafuu alieleza kuwa utabiri ulikuwa kama ulivyotabiriwa
hivyo mipango iliyowekwa ya kushirikisha maafisa ugani ilienda kama
ilivyopangwa.
Mdau kutoka ofisi ya Waziri
Mkuu, Idara ya Maafa alisema baada ya kupokea utabiri huo, idara iliandaa kikao
kazi cha kujadili mpango wa dharura wa ukame unaoweza kujitokeza kutokana na
utabiri uliotolewa sambamba na kuandaa vipindi vya elimu kwa umma kupitia
vyombo mbalimbali va habari.
Katika Mkutano huo, wadau
walipata fursa ya kuona rasimu ya utabiri wa hali ya hewa katika kipindi cha
mwezi Machi hadi Mei 2022 na kuweza kutoa ushauri utaowezesha kuandaa mbinu na
mipango ya kukabiliana na athari za utabiri huo. Mamlaka ya Hali ya Hewa
Tanzania inatarajia kutoa rasmi utabiri wa msimu wa mvua za MASIKA 2022 kupitia
vyombo vya habari, tarehe 17 Februari 2022.
No comments:
Post a Comment