Dar es Salaam; Tarehe 11 Februari,
2020;
Wadau kutoka sekta mbalimbali nchini wametakiwa kujenga tabia ya kufuatilia taarifa za hali ya hewa za mrejeo kutoka Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA). Wito huo umetolewa na Mwenyekiti wa Bodi ya TMA, Dkt. Buruhani Nyenzi ambaye pia alikuwa mgeni rasmi wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Wadau wa Kujadili jinsi Utabiri wa Mvua za Msimu wa Machi hadi Mei 2020 (MASIKA) utakavyotumika katika Sekta Mbalimbali, uliofanyika tarehe 11 Februari, 2020 katika ukumbi wa Taasisi ya Mafunzo ya Uanasheria kwa Vitendo Tanzania (The Law School of Tanzania), Dar es Salaam.
"Baada ya mkutano huu, natoa wito kwa wadau kujenga tabia ya kufuatilia mrejeo wa taarifa za hali ya hewa zinazotolewa baada ya utabiri wa awali kutolewa, nasema hivi kwa vile hii ni hali ya hewa, upepo ukibadilika tu na hali ya hewa inabadilika hivyo ni vyema kufuatilia taarifa hizo kwa ukaribu". Alizungumza Dkt. Nyenzi
Vile vile, Dkt. Nyenzi alionesha imani yake kwa wadau hao kwamba anatarajia matokeo ya mkutano huo, yatatoa nafasi kwa watanzania kupata utabiri uliokamilika inavyotarajiwa, matumizi yake kiuchumi na kijamii pamoja na athari zinazoweza kutokea na hivyo kuwapa wananchi wasaa wa kujipanga ili kupunguza au kuepusha kabisa madhara.

Awali, wakati
akikaribisha wadau hao, Dkt. Agnes Kijazi, Mkurugenzi Mkuu wa TMA na Makamu wa
Tatu wa Rais wa Shirika la Hali ya Hewa Duniani (WMO) aliwashukuru wadau kwa
kuitikia mwaliko wa TMA na kuwaeleza kuwa, TMA imejiwekea utaratibu wa kukutana
na wadau kipindi cha misimu wa mvua ili utabiri utakaotolewa ukatumike vizuri.
Aidha, kulingana na lengo la mkutano huo, Dkt. Kijazi alielezea kwa kina maeneo
yanayotarajiwa kupata mvua za msimu wa MASIKA, huku akisisitiza utabiri
utakaotolewa kutumika kwa faida.
Dkt.
Kijazi pia aliwajulisha wadau kuhusiana na mabadiliko ya TMA kisheria na
kufafanua jukumu jipya la Mamlaka la kudhibiti shughuli za hali ya hewa katika
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, hivyo kutokana na mabadiliko hayo, TMA
inaendelea na uboreshaji wa huduma kwa sekta mbali mbali nchini. “Wadau wote
wenye vifaa vya hali ya hew ani jukumu lao kisheria kuhakikisha vifaa hivyo
vimesajiliwa na TMA” alisema Dkt. Kijazi.
“Mkihitaji
utabiri maalum kwa ajili ya sekta zenu ni vyema wadau mkatuona ili tuweze
kuwaandalia kwa vile huduma hii ipo kwaajili ya maendeleo ya nchi yetu na ni vyema tukaitumia fursa hii, sisi pale
ofisini tunautambua kama utabiri mahususi kwa sekta mbalimbali”. Alisema Dkt.
Kijazi
Naye,
Mratibu kutoka FAO, Ndugu. Diomedes Kalisa alielezea umuhimu wa taarifa za hali
ya hewa katika sekta ya kilimo. Alisisitiza umuhimu wa kufuatilia taarifa za
mrejeo huku akitoa wa mkulima aliyebadilisha aina ya mazao ya kupanda kutokana
na taarifa za mrejeo za hali ya hewa
zilizotolewa na TMA na hatimaye alipata faida ukilinganisha na wakulima
wengine.
Mkutano
huu umeandaliwa na TMA kwa kushirikiana na Shirika la Umoja wa Mataifa la
Chakula na Kilimo (FAO) na hivyo kutoa wigo wa ufadhili wa ushiriki wa wadau kutoka ngazi ya wilaya,
ambapo maafisa kilimo kutoka ngazi ya wilaya walishiriki mkutano huo.
No comments:
Post a Comment