Dar es Salaam; Tarehe 12 Februari, 2020
Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imeendelea kuwasisitiza wanahabari kuwa na ushirikiano wa mara kwa mara na TMA katika usambazaji wa taarifa za hali ya hewa ili taarifa ziweze kufika kwa wakati.
Hayo yamezungumzwa na Mkurugenzi Mkuu wa TMA na Makamu wa Tatu wa Rais wa Shirika la Hali ya Hewa Duniani (WMO), Dkt. Agnes Kijazi wakati wa Warsha ya Wanahabari kuhusu Mwelekeo wa Msimu wa Mvua za Mwezi Machi hadi Mei 2020 (Masika), iliofanyika tarehe 12 Februari, 2020 katika ukumbi wa Mikutano- TMA, Ubungo Plaza, Dar es Salaam.
“Warsha hii ni muendelezo wa juhudi za mamlaka kutaka kuhakikisha taarifa za utabiri wa hali ya hewa zinawafikia walengwa ikiwemo jamii kwa uhakika, usahihi na kwa wakati”. Alizungumza Dkt. Kijazi.
Aidha, Dkt.
Kijazi alisema taarifa za hali ya hewa zikiifikia jamii
kwa wakati, uhakika na usahihi itaisaidia jamii kukabiliana na changamoto za
mabadiliko ya hali ya hewa pia itazisaidia mamlaka zinazohusika kupanga mipango
endelevu ambayo haiwezi kuathiriwa na hali mbaya ya hewa, hivyo uelewa wa
pamoja ni muhimu ili jamii iweze kunufaika na taarifa za hali ya hewa
zinazotolewa.
“TMA
ikitoa tahadhari ya mvua kubwa na wewe mwanahabari ukakuta eneo lenye mafuriko,
stori yako ianzie kwenye tahadhari iliyotolewa na hali halisi iliyotokea na
hatua ambayo wananchi wangepaswa kuchukua na kumalizia na msisitizo wa
kuzitumia vyema taarifa za hali ya hewa. Kwa njia hiyo utakuwa hukutoa tuu
habari bali umeelimisha jamii”. Aliongezea Dkt. Kijazi
Mamlaka
imekuwa ikihakikisha inakutana na wanahabari ambao ni daraja muhimu katika
kuwafikia wananchi wote kwa ujumla ili kupata uelewa wa pamoja na namna bora ya
kusambaza taarifa za hali ya hewa ambapo katika warsha hiyo
wanahabari wanapata nafasi ya kupitia rasimu
ya mwelekeo wa mvua za masika na viashiria vilivyopelekea kupatikana kwa utabiri
wa hali ya hewa kwa msimu huo wa mwezi
Machi hadi Mei 2020.
Taarifa
rasmi ya Mwelekeo wa Msimu wa Mvua za Masika
kwa kipindi cha mwezi Machi hadi Mei 2020 itatolewa rasmi kwa vyombo vya habari,
Tarehe 13 Februari 2020, Siku ya Alhamis, Ofisi za TMA-Makao Makuu, Ubungo
Plaza, Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment