Mhe. Isack Kamwelwe katika picha ya pamoja na menejiment ya TMA |
Mhe. Isack Kamwelwe katika picha ya pamoja na wajumbe wa baraza la wafanyakazi wa TMA |
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Mhandisi Isack Kamwelwe
ameipongeza Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania(TMA) kwa kufanikiwa kupata sheria
mpya ya huduma za hali ya hewa nchini. Waziri Kamwelwe alizungumza hayo wakati
akilifungua rasmi Baraza la Wafanyakazi wa TMA, tarehe 22 Machi 2019.
‘Napenda kutumia nafasi hii kipekee kabisa kuipongeza Mamlaka ya Hali ya
Hewa Tanzania chini ya uongozi wa Wizara yangu kwa sheria iliyopitishwa na
Bunge la jamhuri ya Muungano wa Tanzania mwezi Januari, 2019 na kusainiwa na
Mhe. Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuri’. Alizungumza mhe. Kamwelwe
Mhe Kamwele aliongezea kwa kusema sheria hii inaipa TMA mamlaka kamili ya
kutoa huduma na kuhakiki shughuli zote zinazohusiana na hali ya hewa katika
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa TMA, Dkt. Agnes Kijazi alimshukuru mhe
waziri kwa kukubali kufungua baraza la wafanyakazi wa TMA na kuelezea madhumuni
ya baraza hilo.
‘Madhumuni makuu ya Baraza hili ni kupokea, kujadili na kupitisha
mapendekezo ya bajeti ya Mamlaka kwa kipindi cha mwaka wa fedha 2019/2020’.
Alizungumza Dkt. Kijazi
‘Aidha, mapendekezo hayo ya bajeti yanazingatia vipaumbele vitakavyo
iwezesha Mamlaka kufikia malengo yake na kuongeza ubora na ufanisi katika
utoaji wa huduma za hali ya hewa kwa
umma kwa lengo la kupunguza athari za hali mbaya ya hewa na hivyo kuchangia
katika kukuza pato la Taifa’. Aliongezea Dkt. Kijazi
No comments:
Post a Comment