Washiriki wa warsha ya
wanahabari kuhusu msimu wa mvua za masika, mwezi Machi hadi Mei 2019 katika picha ya
pamoja
Tarehe 13 Februari 2019
Ikiwa ni mwendelezo wa ushirikishwaji wa wadau mbalimbali katika
kuhakikisha huduma za hali ya hewa zinawafikia wananchi kwa wakati na kwa lugha
inayoeleweka. Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imekutana na wanahabari
kutoka vyombo mbalimbali vya habari nchini kujadili mwelekeo wa msimu wa mvua
za MASIKA kwa 2019 kabla ya kutolewa rasmi kwa umma tarehe 14 Februari 2019.
Akizungumza wakati wa
ufunguzi wa mkutano huo katika ukumbi wa mikutano wa ‘Law School’, Dkt.
Ladislaus Chang’a ambaye ni Mkurugenzi wa Utafiti na Matumizi ya tarifa za hali
ya hewa wa TMA alisema kuwa dhamira ya kukutana na wanahabari ni muendelezo wa
dhamira na utaratibu wa TMA wa kuimarisha ushilikishwaji na kuendelea
kuwajengea uwezo wanahabari ili wazielewe vizuri zaidi taaarifa za hali ya hewa
na hususani utabiri na hivyo waweze kuzifikisha taarifa, kuhabarisha na
kuelimisha jamii kwa ufasaha na ufanisi zaidi.
Aidha wanahabari
walitumia fursa hiyo kujadili na kutoa mapendekezo ya kuboresha ufungashwaji na
usambazaji wa tarifa za hali ya hewa ili ziendelee kuwafikia walengwa kwa
wakati na kwa ufasaha zaidi. Pia walielezea umuhimu wa kuwajengea uwezo
wanahabari kuzielewa kwa kina tarifa za hali ya hewa na mabadiliko yake.
Mkutano huo wa siku moja umeandaliwa chini ya mwamvuli wa Awamu
ya Pili ya Programu ya Kidunia ya Utoaji wa Huduma za Hali ya Hewa ya GFCS
yaani “Global Framework for Climate Services Adaptation Programme in
Africa (APA) II” hapa Tanzania yenye lengo la kuimarisha huduma za hali
ya hewa katika nyanja ya utoaji, usamabazaji na utumiaji wa huduma hizo.
Mkutano huu ulijumuisha wanahabari kutoka kwenye vituo vya televisheni, redio,
magazeti, blogs na mitandao ya kijamii
IMETOLEWA NA MONICA MUTONI
OFISI YA UHUSIANO
MAMLAKA YA HALI YA HEWA TANZANIA
|
No comments:
Post a Comment