Matukio mbalimbali kwa picha wakati wataalam wa hali ya hewa wakichambua mifumo ya hali ya hewa katika maandarizi ya utabiri wa hali ya hewa kwa msimu wa masika (Machi hadi Mei 2019) |
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania
(TMA) Dkt. Agnes Kijazi amewata wataalam wa hali ya hewa kutumia utalaam
wao walionao kuhakikisha maandalizi ya utabiri wa hali ya hewa kwa
msimu wa mvua za masika (Machi hadi Mei2019) unaendelea kuwa sahihi
zaidi katika kiwango cha juu na wenye ubora utakaosaidia maendeleo ya
kiuchumi katika taifa letu. Dkt. Kijazi alizungumza hayo wakati wa
kufungua warsha ya wataalamu wa hali ya hewa katika kuandaa utabiri
huo.
Warsha hiyo itafuatiwa na warsha ya
wataalamu mabingwa wote wa hali ya hewa pamoja warsha ya wadau wa huduma
za hali ya hewa na warsha ya wanahabari kabla ya kutoa rasmi mwelekeo
wa msimu wa mvua za MASIKA 2019 tarehe 14 Februari 2019.
No comments:
Post a Comment