Picha mbalimbali za waandishi wa habari walioshiriki mkutano wa wanahabari wa kutoa mwelekeo wa mvua za Msimu wa Masika Machi - Mei 2019. |
Mamlaka
ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imetoa rasmi utabiri wa msimu kuanzia mwezi Machi, 2019 hadi Mei, 2019 katika mkutano wa waandishi wa habari
uliofanyika katika Ofisi za TMA.
Taarifa inatoa uchambuzi wa mwenendo wa mifumo ya hali ya hewa na mwelekeo wa msimu wa
mvua katika kipindi cha mwezi Machi hadi Mei,
2019. Pia ushauri na tahadhari kwa wadau wa sekta mbali mbali wanaohitaji
taarifa za hali ya hewa katika utekelezaji wa majukumu yao kama vile Kilimo na Usalama
wa Chakula, Mifugo na Wanyamapori, Maliasili na Utalii, Uchukuzi na Mawasiliano,
Nishati na Maji, Mamlaka za Miji, Afya pamoja na Menejimenti za Maafa. Muhtasari
wa mwelekeo wa mvua hizo na athari zake ni kama ifuatavyo: Kusoma zaidi ingia humu http://www.meteo.go.tz/news/177
No comments:
Post a Comment