Washiriki wa warsha ya wadau wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania kwenye picha ya pamoja, walipokutana katika maandalizi ya utabiri wa mvua za msimu wa masika, mwezi Machi hadi Mei 2019 |
Lengo kuu la warsha hii ilikuwa
ni kuwashirikisha Wadau katika mchakato
wa maandalizi ya utabiri wa mvua za msimu wa masika na kupata maoni na michango
kuhusiana na tafsiri na matumizi sahihi ya
utabiri katika sekta husika. Aidha warsha hii pia ilikuwa ni fursa kwa Mamlaka
ya Hali ya Hewa kuendelea kuwajengea uelewa kuhusiana na mifumo ya hali ya
hewa, utabiri na umuhimu wa kuzingatia tarifa za hali ya hewa katika kupanga
mipango ya kiuchumi na kijamii.
“Ni muhimu sana kuongeza uelewa na kuimarisha matumizi
ya taarifa za hali ya hewa katika shughuli zetu za kiuchumi na kijamii hasa
katika kipindi ambapo dunia inakabiliwa na changamoto ya mabadiliko ya hali ya
hewa” alisema Dkt. Agnes Kijazi, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa,
kupitia hotuba yake ya ufunguzi iliyosomwa na Dkt. Ladislaus Chang’a,
Mkurugenzi wa Utafiti na Matumizi ya huduma za hali ya hewa wakati akifungua
warsha ya wadau wa huduma za hali ya hewa nchini uliofanyika tarehe 12 Februari
2019 katika ukumbi wa “Law School”.
Warsha hii ni mwendelezo wa jitihada za TMA za
kuimarisha ushirikishwaji wa WADAU katika mchakato wa uandaaji wa utabiri na
usambazaji wa tarifa za hali ya hewa kwa msimu wa mvua za MASIKA na VULI.
Warsha hizi zinajumuisha wadau kutoka sekta mbalimbali kama vile kilimo,
mifugo, uvuvi, afya, maji, nishati, maafa, mipango, wanahabari, usafirishaji,
ujenzi n.k
Aidha, katika hotuba yake, Dkt.
Kijazi, aliwashukuru wafadhili wa warsha ambao ni Shirika la Hali ya Hewa Duniani-World Meteorological Organization (WMO) kwa kudhamini warsha hiyo kupitia programu ya Mfumo wa
Kidunia wa Huduma za Hali ya Hewa - Global Framework for Climate Services (GFCS) ambao umewezesha kushirikisha
wadau wengi zaidi pamoja Shirika la kimataifa
la Chakula na Kilimo-Food and Agriculture Organization (FAO) kwa kuwezesha ushiriki wa wadau kutoka katika wilaya za
Mvomero, Kilosa na Uyui.
IMETOLEWA
NA OFISI YA UHUSIANO
MAMLAKA
YA HALI YA HEWA TANZANIA
No comments:
Post a Comment