Matukio mbalimbali kwa picha wakati Mhe. Kamwele akitembelea vitengo mbalimbali vya Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) |
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Mhandisi. Isack
Kamwele amepongeza utendaji kazi wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA).
Mhe. Kamwele alitoa pongezi hizo wakati alipotembelea Ofisi za TMA, Ubungo
Plaza, Dar es Salaam, tarehe 27 Februari 2019 na alipata taarifa ya utendaji kazi wa
mamlaka na kutembelea baadhi ya sehemu za kazi kabla ya kuzungumza na
wafanyakazi. Mhe. Kamwele alipokelewa na uongozi na menejiment ya TMA,
ikiongonzwa na mwenyekiti wa bodi ya ushauri Dkt. Buruhani Nyenzi na kaimu
mkurugenzi mkuu Dkt. Ladislaus Chang’a.
“Nawapongeza TMA kwa umakini na utekelezaji wa majukumu yenu,
nakiri kusema ni moja ya taasisi makini kati ya taasisi zilizo chini ya wizara
yangu nilizo tembelea”. Alizungumza mhe. Kamwele
Aidha, mhe. Kamwele alisisitiza kuboresha mfumo wa
ushirikishwaji wa wadau na usambazaji wa taarifa za hali ya hewa, akitolea
mfano mafuriko yaliyo bomoa barabara eneo la Dumila, kuwa baada ya kufuatilia
taarifa za hali ya hewa waligundua TMA ilitoa taarifa hizo siku mbili kabla ya
tukio na kuonesha rangi nyekundu yenye kumaanisha tahadhari kwa maeneo ya
Kilindi lakini taarifa hiyo haikuwafikia walengwa.
Mhe. Kamwele alimalizia kwa kuahidi kutatua changamoto
zinazoikabili TMA zikiwemo uhitaji wa ongezeko la vituo vya hali ya hewa,
mitambo ya hali ya hewa, kupatikana kwa jengo la kituo kikuu cha utabiri n.k
Akitoa salamu za shukrani kwa upande wa TMA, mkurugenzi wa ofisi
ya TMA Zanzibar, Bw. Mohamed Ngwali alimshukuru mhe. Waziri kwa pongezi
sambamba na kutembelea na kuona shughuli zinazofanywa na TMA, na kuahidi
kufanyia kazi maelekezo yote aliyoyatoa .
Imetolewa:
Ofisi ya Uhusiano
Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania
(TMA)
No comments:
Post a Comment