Tuesday, August 21, 2018

Katibu Mkuu wa Shirika la Hali ya Hewa Duniani Prof. Petteri Taalas awasili nchini kwa ziara ya kikazi

Katibu Mkuu Shirika la Hali ya Hewa Duniani Prof. Petteri Taalas awasili nchini kwa ziara ya kikazi. Pichani akipokelewa na mwenyeji wake Mkurugenzi Mkuu wa TMA dkt. Agnes Kijazi na Mkurugenzi Mkuu wa TCAA bw. Hamza Johari.

Monday, August 20, 2018

UZINDUZI WA MFUMO WA TAIFA WA HUDUMA ZA HALI YA HEWA

Tarehe 21 Agosti, 2018 Mhe. Jenista Mhagama, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye uzinduzi wa mfumo wa Taifa wa Huduma za Hali ya Hewa, utakaofanyika katika kituo cha mikutano cha kimataifa cha Mwl. Julius Nyerere, Dar es salaam kuanzia saa saba(7) mchana.

TMA YAWA MWENYEJI WA MAFUNZO YA UTUMIAJI WA MFUMO WA TEKNOLOJIA YA KUBORESHA HUDUMA ZA UTABIRI WA HALI YA HEWA.

Washiriki wa mafunzo ya kozi ya (OSCAR/SURFACE) kwenye picha ya pamoja na Mgeni rasmi Mhe, Mr. Mrisho Gambo aliyeketi katikati (mstari wa mbele).


MAMLAKA YA HALI YA HEWA TANZANIA YAWA MWENYEJI WA MAFUNZO YA UTUMIAJI WA MFUMO WA TEKNOLOJIA YA KUBORESHA HUDUMA ZA UTABIRI WA HALI YA HEWA KWA NCHI 23 ZINAZOONGEA LUGHA YA KINGEREZA BARANI AFRIKA.

Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini (TMA) imekuwa mwenyeji wa mafunzo  ya utumiaji wa mfumo wa teknolojia ya kuboresha huduma za utabiri wa hali ya hewa kwa nchi 23 zinazoongea lugha ya kingereza barani Afrika (Observing Systems Capability Analysis and Review Tool for the  Metadata of surface - based observing systems ( OSCAR/SURFACE)). Lengo la mafunzo hayo ni kuwajengea uwezo washiriki jinsi ya kutumia  mfumo huo katika nchi zao. Akizungumza wakati wa ufunguzi wa  mafunzo, mkuu wa mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Gambo ambaye pia alikuwa mgeni rasmi, aliwashukuru Shirika la Hali ya Hewa Duniani (WMO) kwa kufadhili mafunzo hayo na kuchagua Arusha kuwa sehemu ya kufanyia mafunzo. Aidha aliwataka washiriki wote kutumia taaluma watakayoipata katika kuongeza ujuzi wa kukabiliana na changamoto zinazoikumba bara la Afrika ili kuhakikisha Afrika haiachwi nyuma katika maendeleo endelevu. Amesisitiza umuhimu wa mchango wa huduma za hali ya hewa kwa maendeleo ya kiuchumi na kijamii wakiwa pamoja na sekta za kilimo, nishati, utalii, afya n.k
Mafunzo hayo yamefanyika Mkoani Arusha kuanzia tarehe 15 hadi 17 Agosti 2018.
Imetolewa na Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania.

Tuesday, August 14, 2018

TMA YAWA MWENYEJI WA MKUTANO WA MRADI WA HIGH IMPACT WEATHER LAKE SYSTEM (HIGHWAY)”

Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imekuwa mwenyeji wa mkutano wa Mradi wa HIGH Impact Weather lAke sYstem (HIGHWAY)” unaojadili namna ya kuongeza uwezo za nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) zilizoko kwenye eneo la bonde la Ziwa Victoria katika kupima na kufuatilia mifumo ya hali ya hewa hususani ile inayosababisha hali mbaya ya hewa ndani ya Ziwa Victoria kwa lengo la kuokoa maisha ya watu na mali zao "HIGH Impact Weather lAke sYstem (HIGHWAY) Gap Analysis". Mradi wa HIGHWAY unafadhiliwa na Shirika la Maendeleo la Nchini Uingereza (DFID) kupitia program yake ya Weather and Climate Information Services for Africa (WISER)” na kutekelezwa kwa ushirikiano na Sekretariet ya EAC, Shirika la Hali ya hewa Duniani(WMO), na Taasisi za Hali ya Hewa za nchi wanachama wa EAC.  Mkutano huu unafanyika Jijini Arusha kuanzia tarehe 13 hadi 14 Agosti 2018.

Monday, August 6, 2018

DKT.TIZEBA ASISITIZA USHIRIKISHWAJI WA TMA KWENYE MIRADI MBALIMBALI YA MAENDELEO YA KILIMO

Waziri wa Kilimo Mhe. Dkt. Charles Tizeba akipata ufafanuzi kutoka kwa Meneja wa TMA Kanda ya Mashariki Bw. Nassoro Mnanike wakati alipotembelea banda la TMA kwenye maonesho ya nane nane 2018, Morogoro
Waziri wa Kilimo Mhe. Dkt. Charles Tizeba akisisitiza umuhimu wa kutumia miradi ya maendeleo kuongeza ufanisi wa kazi za Mamlaka wakati alipotembelea banda la TMA kwenye maonesho ya nane nane 2018, Morogoro
Waziri wa Kilimo Mhe. Dkt. Charles Tizeba akipata ufafanuzi kutoka kwa Meneja wa TMA Kanda ya Mashariki Bw. Nassoro Mnanike na mtaalam wa hali ya hewa Dkt. Habiba Mtongori wakati alipotembelea banda la TMA kwenye maonesho ya nane nane 2018, Morogoro

TMA YAENDELEA KUTOA ELIMU YA HUDUMA ZA HALI YA HEWA KATIKA KILIMO, MIFUGO NA UVUVI KWA MAENDELEO YA VIWANDA KUPITIA MAONESHO YA NANENANE 2018 NCHINI

Mtaalam kutoka Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania Dkt. Habiba Mtongori akitoa elimu ya sayansi ya hali ya hewa kupitia satelaiti kwenye maonesho ya Nane Nane 2018 mkoani Morogoro
Mtaalam kutoka Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania Bw. Noah Kiende akitoa elimu ya matumizi ya kifaa cha kupima nguvu ya jua kwenye maonesho ya Nane Nane 2018 mkoani Morogoro
Baadhi ya washiriki katika picha ya pamoja kwenye maonesho ya Nane Nane 2018 mkoani Morogoro
Baadhi ya wananchi katika picha  wakiendelea kufurika katika banda la Mamlaka ya Hali ya Hewa  kwenye maonesho ya Nane Nane 2018 mkoani Simiyu
Baadhi ya wananchi katika picha  wakipata elimu ya upimaji kasi na mwelekeo wa upepo  kwenye maonesho ya Nane Nane 2018 mkoani Mbeya

Sunday, August 5, 2018

MKUU WA MKOA WA SIMIYU AFURAHISHWA NA JITIHADA ZA TMA ZA KUWATEMBELEA WANAFUNZI MASHULENI MKOANI SIMIYU IKIWA NI MOJA YA MKAKATI WA KUTOA ELIMU YA HALI YA HEWA KWA JAMII KUPITIA YA MAONESHO YA NANE NANE 2018

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe. Anthony Mtaka akipata maelezo kuhusiana na huduma mbalimbali zinazotolewa na TMA alipotembelea banda la Mamlaka kwenye viwanja vya Nyakabidi, Simiyu Tarehe 05 Agosti 2018.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe. Anthony Mtaka katika picha ya pamoja na baadhi ya washiriki wa maonesho ya Nane Nane  alipotembelea banda la TMA  kwenye viwanja vya Nyakabidi, Simiyu Tarehe 05 Agosti 2018.
Mtaalam wa hali ya hewa kutoka TMA akitoa elimu kwa wananchi waliotembelea banda la TMA  kwenye viwanja vya Nyakabidi, Simiyu 
Mtaalam wa hali ya hewa kutoka TMA akitoa elimu kwa wananchi waliotembelea banda la TMA  kwenye viwanja vya Nyakabidi, Simiyu 
Wananchi mbalimbali wakiendelea kufurika katika banda la TMA  kwenye viwanja vya Nyakabidi, Simiyu 

Featured Post

DKT. KIJAZI: KIWANGO CHA USAHIHI WA UTABIRI WA MSIMU WA VULI 2019 KIWE CHA JUU ZAIDI.

Mkurugenzi mkuu wa TMA na Makamu wa Tatu wa Rais wa Shirika la Hali ya Hewa Duniani Dkt. Agnes Kijazi (katikati mwenye suti nyeusi) waka...