|
Mgeni
rasmi Ndg. Amour Hamil Bakari ambaye pia ni Katibu Mkuu, Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, akizungumza na washiriki wakati akifungua rasmi kikao cha kupata maoni ya wadau kuhusiana na mapendekezo ya kusaini Katiba ya Baraza la Mawaziri wenye dhamana ya Hali ya Hewa katika Bara la Afrika, yaani 'African Ministerial Conference on Meteorology (AMCOMET)' kilichofanyika Tarehe
04 Oktoba 2021 katika ukumbi wa Jengo la malaria, Mwanakwerekwe - Zanzibar. |
|
Muwakilishi wa Katibu Mkuu, Wizara ya
Ujenzi na Uchukuzi (Sekta ya Uchukuzi) (SMT) Ndg. Biseko Paul Chiganga,
akisisitiza jambo kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi kuzungumza na washiriki wa kikao cha kupata maoni
ya wadau kuhusiana na mapendekezo ya kusaini Katiba ya Baraza la
Mawaziri wenye dhamana ya Hali ya Hewa katika Bara la Afrika, yaani
'African Ministerial Conference on Meteorology (AMCOMET)' kilichofanyika
Tarehe
04 Oktoba 2021 katika ukumbi wa Jengo la malaria, Mwanakwerekwe -
Zanzibar. |
|
Muwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania Ndg. Mohammed Ngwali, akitoa neno la shukurani kwa mgeni rasmi katika kikao cha kupata maoni
ya wadau kuhusiana na mapendekezo ya kusaini Katiba ya Baraza la
Mawaziri wenye dhamana ya Hali ya Hewa katika Bara la Afrika, yaani
'African Ministerial Conference on Meteorology (AMCOMET)' kilichofanyika
Tarehe
04 Oktoba 2021 katika ukumbi wa Jengo la malaria, Mwanakwerekwe -
Zanzibar. |
|
Washiriki wakisikiliza kwa makini hotuba ya mgeni rasmi katika kikao cha kupata maoni
ya wadau kuhusiana na mapendekezo ya kusaini Katiba ya Baraza la
Mawaziri wenye dhamana ya Hali ya Hewa katika Bara la Afrika, yaani
'African Ministerial Conference on Meteorology (AMCOMET)' kilichofanyika
Tarehe
04 Oktoba 2021 katika ukumbi wa Jengo la malaria, Mwanakwerekwe -
Zanzibar. |
|
Washiriki mbalimbali wakichangia mada katika kikao cha kupata maoni
ya wadau kuhusiana na mapendekezo ya kusaini Katiba ya Baraza la
Mawaziri wenye dhamana ya Hali ya Hewa katika Bara la Afrika, yaani
'African Ministerial Conference on Meteorology (AMCOMET)' kilichofanyika
Tarehe
04 Oktoba 2021 katika ukumbi wa Jengo la malaria, Mwanakwerekwe -
Zanzibar. |
|
Mgeni rasmi (katikati ya walioketi) akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa kikao cha kupata maoni
ya wadau kuhusiana na mapendekezo ya kusaini Katiba ya Baraza la
Mawaziri wenye dhamana ya Hali ya Hewa katika Bara la Afrika, yaani
'African Ministerial Conference on Meteorology (AMCOMET)' kilichofanyika
Tarehe
04 Oktoba 2021 katika ukumbi wa Jengo la malaria, Mwanakwerekwe -
Zanzibar. |
Katibu
Mkuu, Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji wa Serikali ya Mapinduzi
Zanzibar Ndg. Amour Hamil Bakari, amewaasa Watanzania kuchangamkia fursa
mbalimbali zitakazojitokeza baada ya Tanzania kujiunga na
“AMCOMET”. Aliyasema hayo alipokuwa akifungua rasmi kikao cha kupata maoni ya
wadau kuhusiana na mapendekezo ya kusaini Katiba ya Baraza la Mawaziri wenye
dhamana ya Hali ya Hewa katika Bara la Afrika, yaani “African Ministerial
Conference on Meteorology (AMCOMET)”
“Naomba nitumie fursa hii kupitia ufunguzi wa kikao
hiki cha kupata maoni ya mapendekezo ya kusaini katiba ya Baraza la Mawaziri
wenye dhamana ya Hali ya Hewa - Barani Afrika, kuwaasa Watanzania kutumia fursa
mbalimbali zikiwemo za ajira zitakazojitokeza baada ya kujiunga na “AMCOMET”.”
alisema Katibu Mkuu Amour Hamil Bakari.
Aidha, Ndg. Bakari aliongezea kuwa uchumi wa nchi yetu
pamoja na nchi zingine zinazotuzunguka unategemea zaidi sekta za kiuchumi na
kijamii ambazo hutegemea na kuathiriwa sana na hali ya hewa, hususan kwa
kuzingatia kuwa hali ya hewa haitambui mipaka ya kijiografia, hivyo nchi
zinazofanana katika mifumo ya hali ya hewa zimekuwa na programu za pamoja za
kikanda na kimataifa ili kupata suluhisho la kupunguza athari za majanga
yatokanayo na hali mbaya ya hewa na mabadiliko ya hali ya hewa.
Muwakilishi wa Katibu Mkuu, Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi
(Sekta ya Uchukuzi) (SMT) Ndg. Biseko Paul Chiganga, alisisitiza kuendelea kuimarisha
ushirikiano katika masuala ya muungano baina ya Wizara
ya Ujenzi na Uchukuzi (SMT) pamoja na Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi
(SMZ),
ukilenga kuweka uelewa wa pamoja na baadae kutatua changamoto mbalimbali baina
ya sekta za hali ya hewa na usafiri wa anga na sekta nyingine mtambuka.
Aidha, Muwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya
Hali ya Hewa Tanzania, Ndg. Mohammed Ngwali, alimshukuru mgeni rasmi kwa
kukubali kuwa mgeni rasmi katika ufunguzi wa kikao hicho muhimu cha kupokea maoni
ya wadau kitakachoiwezesha Tanzania kupiga hatua zaidi katika mchakato wa
kusaini katiba ya “AMCOMET”.
No comments:
Post a Comment