Monday, October 18, 2021

MHE. KASEKENYA AELEZEA UMUHIMU WA TMA KATIKA UTENDAJI KAZI WA SEKTA MBALIMBALI HAPA NCHINI.


Dar es Salaam,  Tarehe 15/09/2021.

Mheshimiwa Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Mhandisi Godfrey Kasekenya alifungua Maonesho ya Kutangaza Kazi za Taasis za Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi kupitia Mkutano wa 14 wa Wadau Unaohusu kutathmini Utendaji wa Sekta ya Uchukuzi uliofanyika ukumbi wa Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere - Dar es salaam, Tarehe 15 Oktoba, 2021.

Akiongelea umuhimu wa huduma za hali ya hewa katika sekta mbalimbali za maendeleo Mhe. Kasekenya alisema.

 “ Moja ya sababu ya kusisitiza kuwa Taasisi ya Hali ya Hewa ni muhimu katika utendaji kazi wa sekta mbalimbali nchini, ni kwa sababu rubani hawezi kurusha ndege na Meli haiwezi kusafiri bila kupata taarifa za hali ya hewa. Pia ili kupata barabara bora inahitaji kufanya “designing” ambayo kwa kiasi kikubwa inahitaji sana taarifa za hali ya hewa, hivyo kuifanya TMA kuwa taasis muhimu sana katika utendaji kazi wa sekta mbalimbali hapa nchini”.

Mhe. Kasekenya aliongeza kusema TMA inastahili pongezi  kwa kuongozwa na na kiongozi mwanamama, mchapakazi aliyeifanya TMA kuwa moja ya taasis bora hapa nchini pamoja na Barani Afrika, iliyopelekea kuchaguliwa kwake kuwa Makamu wa Tatu wa Raisi wa Shirika la Hali ya Hewa Duniani (WMO).

Aidha, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), ambaye pia ni Makamu wa Tatu wa Rais wa Shirika la Hali ya Hewa Duniani (WMO), Dkt. Agnes Kijazi aliwakumbusha wadau mbalimbali walioshiriki katika maonesho hayo wakiwemo wadau wa maendeleo kutembelea katika banda la TMA ili kupata uelewa wa umuhimu wa kufuatilia na namna ya kuzitumia taarifa za hali ya hewa katika utendaji kazi wa shughuli zao za kimaendeleo ikiwemo utekelezaji wa miradi mikubwa ya kimkakati inayoendeshwa na Serikali.

Dkt. Kijazi alikazia kwa kuwakumbusha wadau kuwa hivi sasaTMA imeanzishwa kwa sheria Na. 2 ya mwaka 2019 inayowataka wadau kutumia taarifa za hali ya hewa ili kuhakikisha uwekezaji unakuwa endelevu hapa nchini kwa kufanya mipango mapema ya kuepusha hasara zinazoweza kujitokeza kutokana na hali mbaya ya hewa inayoweza kujitokeza hususani katika kipindi hiki ambacho Dunia inakabiliwa na mabadiliko ya hali ya hewa.

No comments:

Post a Comment

Featured Post

DKT. KIJAZI: KIWANGO CHA USAHIHI WA UTABIRI WA MSIMU WA VULI 2019 KIWE CHA JUU ZAIDI.

Mkurugenzi mkuu wa TMA na Makamu wa Tatu wa Rais wa Shirika la Hali ya Hewa Duniani Dkt. Agnes Kijazi (katikati mwenye suti nyeusi) waka...